Huko Mahakamani Kwa Lisu wengi walienda wakiwa na Heshima, wakati wakurudi walirudi wakiwa dhalili

Huko Mahakamani Kwa Lisu wengi walienda wakiwa na Heshima, wakati wakurudi walirudi wakiwa dhalili

Tena huko mahakamani ndio kabisa.

Lisu dawa yake akamatwe na kosa. Au itafutwe siri ya zamani ambayo hataki watu tuijue. Ikibainika hiyo kwisha. Ataendeshwa kama kiberenge. Ushujaa wote kwisha.
Labda haipo ukiona hivyo, na zilizopo sio jinai, na hata ikiwa jinai unakuta haina uzito labda alimtukana mtu, mtu wa hivi dawa alikuwa nayo hayati tu 😎
 
Hamjambo wote!

Moja ya Mambo makubwa ambayo viongozi wakubwa, watu wenye Akili, na matajiri wanathamini sana ni pamoja na HESHIMA. Kwao heshima niya thamani sana.

Walitafuta vyeo na nguvu kwa NJ yoyote hata kiharamia ili wapate Heshima na kuogopwa.

Walitafuta pesa na utajiri kinamna yoyote ili wapate heshima.

Wakipita barabarani watu wengine wakae pembeni kwa adabu wawapishe.
Wakisema wengine wafyate mikia yao. Hakuna kupingwa hapa.

Ili waulize maswali na wapewe majibu wanayoyataka.
Leo uwapeleke mahakamani ukawapapase utakavyo? Ukawaulize utakavyo,

Na lazima wajibu,
Wakisema sijui kwao sio heshima. Mkubwa gani hajui? Ni aibu! Unafikiri itakuwaje. Hata mimi kwa kweli sijui kama ningekubali.

Mtu aliyezoea kupewa majibu, kutafutiwa Majawabu, leo ataulizwa maswali tena sio anaulizwa wapi. Ataulizwa mbele ya kadamnasi.

Unajua ubaya wa maswali sio tuu kutoa majibu. Bali kupima utimamu wa Akili ya muulizwa swali.
Je zimetimia? Je yuko sawasawa?

Unajua Akili ni kama Afya.
Fikiria unaulizwa swali unaboronga boronga. Nini kitafuata?

Maswali pia sio tuu yanapima Kiwango chako cha Uelewa na utambuzi. Bali pia yanapima uaminifu wako, kujiamini kwako, historia yako.

Mbaya zaidi, Ukiwa Mahakamani hutatambulika kwa cheo chako. Ingawaje yapo maswali yanayohusu cheo chako utapaswa uyajibu.

Tumemuona Heche Alivyoburuzwa na Katuga. Mahakamani kama unamambo ya chini chini sio sehemu ya kwenda. Huko kuna kuumbuka hivihivi. Yanaweza kuzuka usiyoyatarajia. Mambo ambayo hukutaka watu wayajue unaweza kupewa surprise ukabaki mdomo wazi.
Ujibu usijibu vijana wa kileo watakuambia hiyo IMEENDA.

Na bahati mbaya Lisu sio Mwoga. Hanaga woga na yeyote. Hanaga boss. Boss ni sheria basi.

Bahati mbaya pia, Lisu hanaga Staha hasa akishagundua unamakando Lando.

Kwa mtu anayependa heshima yake. Hawezi kukubali kuwa mahakamani na Lisu. Kwa sababu vyovyote iwavyo Lisu lazima awe upper hand. Lazima ataku outshine tuu upende usipende.

Mbinu ya kukabiliana na mtu kama Lisu. Ni kujifanya mpenda haki hata kinafiki ili kutomvuruga asianze kukufedhehesha.

Mbinu ya pili, Lisu usimjibu kwa majibu yaliyojifunga. Jibu majibu yenye milango ya kutokea.

Kwa sababu Lisu anapendelea HAKI. Kimedani, unapokuwa mbele yake nawe kuwa upande wa Haki na eleza jinsi haki ilivyo kwa mujibu wa kisheria.

Mfano, kama litaulizwa swali la uwajibika na maadili ya kiutumishi. Eleza kwamba sheria zinataka watu wawe waadilifu na kimsingi wapo watumishi waadilifu na ambao wasio waadilifu.

Ukiambiwa mapolisi yanaiba kura na kusaidia vyama vya siasa. Usikatae moja kwa moja. Hii itampa nguvu zaidi.
Lakini ukisema hayo ni mambo binafsi lakini hiyo sio kazi ya jeshi la polisi. Labda wapo maaskari wanaotumia sare za polisi vibaya.

Huwezi kukataa jambo ambalo lilikuwepo. Utadhalilika.

Tunataka tuone. Na natamani nione.

Nduki!!
Sana
 
Wale mashahidi wa mchongo wa jamhuri walikuwa wanapewa angalau tution na serikali jinsi ya kujibu pamoja na assistance ya jamhuri sasa Kwa hawa mashahidi watatu ambao watatakiwa upande wa LISSU watapata shida Sana kwenye kuongozwa.
Alafu Sheria ulivyokuwa haina adabu wakileta ushindi tofauti itabid wafanyiwe cross examination kwasababu ya kusaliti juu ya ushahidi wanaoutoa.

Kazi inabaki kwao wamteee lissu au wafanye usaliti( hostile witnesses) na hapa ndipo dunia itapinduka
Lissu ameiambia mahakama anahitaji muda nao ili awaandae na kupanga namna ya kuliendea hili jambo! Sijui anawaandaaje CDF, IGP na DCI Teh! 🤣🤣🤣
 
Hawawezi kwenda hao mbwa..Kuna mtego LISSU amewawekea na Dunia nzima itawasikia , na kuna uwezekano baada ya hapo wakaharakisha mchakato na wakaishia kuitwa ICC pia..Sio mchezo, ni lazima wakimbie la sivyo wangevuliwa nguo zao zote
Wanakimbia kwa muda nadhani wakijiandaa, si wamepewa siku tatu?

Kesi imeahirishwa kuwangojea Trh 18/9.
 
Jeshi linaogopa mahakama.
Kimsingi jeshini wana keywords chache mno ambazo wanatumia kila siku in their career - afande, jambo, sawa, mguu pande, mguu sawa, piga, legeza, shoto kulia shoto kulia, nyumaa geuka, mchaka mchaka jinja, bunduki, risasi, fyatua, piga,... extremely few!

Wakiwaza dictionary za mahakama zilivyosheheni maneno tena mengi ya kutegana na kudhalilishana! Doh!
 
"Ukiwa na makandokando usiende mahakamani kutoa ushahidi"

Hiyo pointi yako hapo juu nakubaliana nayo moja kwa moja.

Ndio maana tukaona wakina Golugwa, Brenda, na Mnyika hawakuwa na shida kwenye kujibu maswali yao, Katuga hakuwa na mlango wa kuwaingia.

Ila kwa Heche na yale yaliyomtokea, nadhani ilikuwa surprise hata kwa Lissu!.
 
Back
Top Bottom