Huko Mahakamani Kwa Lisu wengi walienda wakiwa na Heshima, wakati wakurudi walirudi wakiwa dhalili

Huko Mahakamani Kwa Lisu wengi walienda wakiwa na Heshima, wakati wakurudi walirudi wakiwa dhalili

Ndio maana tukaona wakina Golugwa, Brenda, na Mnyika hawakuwa na shida kwenye kujibu maswali yao, Katuga hakuwa na mlango wa kuwaingia.

Ila kwa Heche na yale yaliyomtokea, nadhani ilikuwa surprise hata kwa Lissu!
Heche hajatokewa na chochote udukuzi wa Account zake bila Account za katuga na mawakili wenzake kuletwa mahakani wakajua Account za katuga binafsi haifanyi katuga kuwa bingwa, sana sana katuga kaonekana ni wakili wa mchongo na wakili mzushi kanjanja bush Loyer
 
Njia sahihi na bora ni kuwahi kuifuta kesi ya Lisu akaachiwa huru haraka kabla ya kuileta Aibu ya Taifa
 
Mkuu wa majeshi na waovu wenzie wameweka kende mfukoni. Wamezama ndichi, wameogopa dodosa za mwanasheria msomi..Hakika cross examination ya msomi Lissu ni zaidi ya kisu cha labour !..Lazima wangetoa maboko mbwa hao
Mahakamani kuna majibu yake.


Kwa mfano unaulizwa ulishawahi kuona mtu ametekwa? Heche anajua watu wametekwa tena watu wake wa karibu kama kina Ben Saanane , Mdude ,Soka etc lakini mbele ya Jaji kasema sijawahi lakini haindoi uhalisia kwamba watu wametekwa.
 
Wakithubutu kwenda mahakamani itakuwa Aibu kubwa kwao kwani maswali ya Lisu yatawavua nguo na kuwachakaza vibaya hadi kuugua pressure na moyo
Wkienda ni aibu, na wakikwepa ni aibu. Hii inaitwa ukichimama nchale, uk8kaa nchale.

Ila ukweli ni kuwa aibu ya kukwepa ni bora mara elfu kuliko kwenda kuvaana na TAL.
 
Tena huko mahakamani ndio kabisa.

Lisu dawa yake akamatwe na kosa. Au itafutwe siri ya zamani ambayo hataki watu tuijue. Ikibainika hiyo kwisha. Ataendeshwa kama kiberenge. Ushujaa wote kwisha.

..Lissu hana hayo mambo ndio maana Magufuli akaona bora amuuwe.
 
Hamjambo wote!

Moja ya Mambo makubwa ambayo viongozi wakubwa, watu wenye Akili, na matajiri wanathamini sana ni pamoja na HESHIMA. Kwao heshima niya thamani sana.

Walitafuta vyeo na nguvu kwa NJ yoyote hata kiharamia ili wapate Heshima na kuogopwa.

Walitafuta pesa na utajiri kinamna yoyote ili wapate heshima.

Wakipita barabarani watu wengine wakae pembeni kwa adabu wawapishe.
Wakisema wengine wafyate mikia yao. Hakuna kupingwa hapa.

Ili waulize maswali na wapewe majibu wanayoyataka.
Leo uwapeleke mahakamani ukawapapase utakavyo? Ukawaulize utakavyo,

Na lazima wajibu,
Wakisema sijui kwao sio heshima. Mkubwa gani hajui? Ni aibu! Unafikiri itakuwaje. Hata mimi kwa kweli sijui kama ningekubali.

Mtu aliyezoea kupewa majibu, kutafutiwa Majawabu, leo ataulizwa maswali tena sio anaulizwa wapi. Ataulizwa mbele ya kadamnasi.

Unajua ubaya wa maswali sio tuu kutoa majibu. Bali kupima utimamu wa Akili ya muulizwa swali.
Je zimetimia? Je yuko sawasawa?

Unajua Akili ni kama Afya.
Fikiria unaulizwa swali unaboronga boronga. Nini kitafuata?

Maswali pia sio tuu yanapima Kiwango chako cha Uelewa na utambuzi. Bali pia yanapima uaminifu wako, kujiamini kwako, historia yako.

Mbaya zaidi, Ukiwa Mahakamani hutatambulika kwa cheo chako. Ingawaje yapo maswali yanayohusu cheo chako utapaswa uyajibu.

Tumemuona Heche Alivyoburuzwa na Katuga. Mahakamani kama unamambo ya chini chini sio sehemu ya kwenda. Huko kuna kuumbuka hivihivi. Yanaweza kuzuka usiyoyatarajia. Mambo ambayo hukutaka watu wayajue unaweza kupewa surprise ukabaki mdomo wazi.
Ujibu usijibu vijana wa kileo watakuambia hiyo IMEENDA.

Na bahati mbaya Lisu sio Mwoga. Hanaga woga na yeyote. Hanaga boss. Boss ni sheria basi.

Bahati mbaya pia, Lisu hanaga Staha hasa akishagundua unamakando Lando.

Kwa mtu anayependa heshima yake. Hawezi kukubali kuwa mahakamani na Lisu. Kwa sababu vyovyote iwavyo Lisu lazima awe upper hand. Lazima ataku outshine tuu upende usipende.

Mbinu ya kukabiliana na mtu kama Lisu. Ni kujifanya mpenda haki hata kinafiki ili kutomvuruga asianze kukufedhehesha.

Mbinu ya pili, Lisu usimjibu kwa majibu yaliyojifunga. Jibu majibu yenye milango ya kutokea.

Kwa sababu Lisu anapendelea HAKI. Kimedani, unapokuwa mbele yake nawe kuwa upande wa Haki na eleza jinsi haki ilivyo kwa mujibu wa kisheria.

Mfano, kama litaulizwa swali la uwajibika na maadili ya kiutumishi. Eleza kwamba sheria zinataka watu wawe waadilifu na kimsingi wapo watumishi waadilifu na ambao wasio waadilifu.

Ukiambiwa mapolisi yanaiba kura na kusaidia vyama vya siasa. Usikatae moja kwa moja. Hii itampa nguvu zaidi.
Lakini ukisema hayo ni mambo binafsi lakini hiyo sio kazi ya jeshi la polisi. Labda wapo maaskari wanaotumia sare za polisi vibaya.

Huwezi kukataa jambo ambalo lilikuwepo. Utadhalilika.

Tunataka tuone. Na natamani nione.

Nduki!!
Natambua wanafuatilia kwa makini kesi za Lissu, wanakumbuka vizuri sana cross-examination ya Bwana Jela, pale alipoambiwa kwa watu wengine anawaambia waache kiherehere, ila anasita kufanya hivyo kutokana na wadhifa wake.
 
Heche hajatokewa na chochote udukuzi wa Account zake bila Account za katuga na mawakili wenzake kuletwa mahakani wakajua Account za katuga binafsi haifanyi katuga kuwa bingwa, sana sana katuga kaonekana ni wakili wa mchongo na wakili mzushi kanjanja bush Loyer
you are very right
 
Natambua wanafuatilia kwa makini kesi za Lissu, wanakumbuka vizuri sana cross-examination ya Bwana Jela, pale alipoambiwa kwa watu wengine anawaambia waache kiherehere, ila anasita kufanya hivyo kutokana na wadhifa wake.

Hata ingekuwa ni mimi nisingeenda, na kama ningeenda ningefanya kama Kingai tuu. Hakuna zaidi ya hivyo
 
Back
Top Bottom