Huko USA huwezi kutenganisha haki za binadamu na haki za mashoga/LGBT!

Huko USA huwezi kutenganisha haki za binadamu na haki za mashoga/LGBT!

Mimi kama sishiriki mambo ya ushoga ya nin inisumbue hakiri sioni haja ya kupoteza mda kujadili mambo haya kila cku
 
hili suala linaenda kdg kdg lkn ,baada ya muda fulani tutakuwa tushalielewa,,ni kama UKMWI NA CONDOM wakati ,wanaanza kuelimisha ilikua kama ngumu hv ,ila baadae sasa... MUHIMU jamaa wametia mzigo, na wabongo wenye NGOs wanavyopenda hela mbn wataziomba na kutetea ushoga kwa mwavuli wa HAKI ZA KIBINADAMU
 
Lini lissu na lema waliuunga mkono ushoga kama sio uongo, ulivyokua na akili fupi sasa umlaumu lissu na lema wao ndo chama tawala au wasimamiz wa sheria

Lawama lazima ziende kwa samia na serekali ya ccm wao ndo wako wengi bungeni na wanaweza pitisha sheria alafu unakuja kulaumu lisu na lema si uwendawazimu

Ccm walichofanikiwa ni kuaminisha watanzania wao sio responsible kwa matatizo ya Tanzania bali ni chadema
Hilo zee ni puuzi sana.
 
Wewe huwajui watu wanafiki..
Walichotaka wao ni Samia awashambulie USA kwenye media ikiwezekana akatae ziara ya Kamala ..
Ili halafu tukipigwa vikwazo wake tena kumshambulia Samia Kwa kuharibu diplomasia......

We hushangai watu ambao Viongozi wao WA kisiasa kina Lema na Tundu Lissu wanaunga mkono haki za Mashoga waziwazi ..lakini wanataka Samia apinge ...Hulu wako kimya Kwa Lema na Lissu??...we huoni ajabu hii??
Utakuwa mganga wa kienyeji mpiga ramli, unayejidai kujua vichwa vya wengine vinafikiria kitu gani bila wewe kuambiwa, hopeless old man!.

Tell us, wapi na lini Lissu na Lema waliwahi support ushoga?
 
Mkuu tatizo viongozi wa wadanganyika wanajizima data kujifanya hawajui marekani na mabeberu wote wa ulaya huwa wanamaanisha nini wanapoongelea kuhusu haki za binadamu.........na huu unafiki ni kutokana na kutegemea kupata favour na misaada kutoka kwa hao mabeberu.......hii ni moja ya laana za umaskini.
 
hili suala linaenda kdg kdg lkn ,baada ya muda fulani tutakuwa tushalielewa,,ni kama UKMWI NA CONDOM wakati ,wanaanza kuelimisha ilikua kama ngumu hv ,ila baadae sasa... MUHIMU jamaa wametia mzigo, na wabongo wenye NGOs wanavyopenda hela mbn wataziomba na kutetea ushoga kwa mwavuli wa HAKI ZA KIBINADAMU
Ni kweli mkuu ni swala la muda tu, Tena the more wanalijadili ndio wanalipa mileage na watu kuwa curious zaidi. They call it Streisand Effect!!
 
Mmarekani huwa anakuja Kufukuwa ?....msijifiche kwenye kivuli cha Mmarekani
Zameni kwenye Tafiti mje na Majibu Kamili
Kuna Tabaka linajihami .....
 
Shida sio demokrasia imeanzia wapi. Hayo mambo ya history yatupilie mbali, tuzungumzie dunia hii ya leo, tunayoishi sasa.
Kwa sasa U.S.A ndio father of democracy
Sasa kwanini unafungamanisha demokrasia na ushoga? Ni hivi mashoga wote wanapenda demokrasia ila SIO wanademokrasia wote wanapenda ushoga. Kama tu useme wasagaji WOTE ni wanawake ila SIO wanawake WOTE ni wasagaji?

Hapo umenielewa
 
Lini lissu na lema waliuunga mkono ushoga kama sio uongo, ulivyokua na akili fupi sasa umlaumu lissu na lema wao ndo chama tawala au wasimamiz wa sheria

Lawama lazima ziende kwa samia na serekali ya ccm wao ndo wako wengi bungeni na wanaweza pitisha sheria alafu unakuja kulaumu lisu na lema si uwendawazimu

Ccm walichofanikiwa ni kuaminisha watanzania wao sio responsible kwa matatizo ya Tanzania bali ni chadema
Hii tabia imezuka sana, utasikia "tungekua na upinzani imara kusingekuwepo mgao wa umeme"..... Sasa unajiuliza anayekata umeme ni Mbowe ama Serikali?
 
Hizo sheria hata kama zipo mbona bado tunatongozwa na misaada yao na tumekaa kimya, kwanini tusiwaambie sheria zetu zinakataza? jana Samia kagoma maswali ya waandishi, unajua alikimbia nini pale?
Wapi Mama Samia hajasema sheria zinakataza? Wapi tumepewa misaada kwa kigezo Cha kulinda haki za mashoga? Mie nakumbuka tumewahi nyimwa pesa kwa kuzuia mabinti wajawazito kurudi shule na pia kuiba kura uchaguzi wa 2015 ila sijawahi sikia tumenyimwa msaada kisa sijui Kuna sheria ya kupinga ushoga.

So tusifungamanishe.... Hata Biblia ya King James tunatumia wakristo ni zao la James V aliyekua shoga. Je Ina maanisha sisi wakristo tuna support ushoga? Same to Wanao print bible za NIV inayotumika zaidi kwa Sasa ni Zondervan or Harper-Collins ambao Wana support ushoga pia ila sijawahi sikia tumeambiwa tusisome biblia kisa zimechapishwa na printer za mashoga!!

Huu unafiki ni kwa faida ya nani? Why tufungamanishe demokrasia na ushoga au misaada na ushoga?
Cc Proved mtu chake Kalamu
 
Duh!
Nimejifunza jambo jipya hapa mkuu 'zitto junior', juu ya hiyo "Biblia ya King James". Nilikuwa sijui hili.

Bila kutaka kuingia zaidi kwenye mjadala huu, niseme tu kwamba hii misaada tunayopewa ina lengo (au malengo) kwa anayetupa hiyo misaada. Siyo kweli kurahisisha tu kwamba "wazungu wanatupenda" hiyo si kweli.
Kinachosikitisha ni kwamba sisi tunaopokea misaada hii hatuitumii kikamilifu kutujengea uwezo wa kuondokana na utegemezi kwa hao wanaotupa hii misaada yao ili kukidhi malengo yao. Matokeo yake tunaendelea kuwa wapokea misaada na kuendelea kuwa uwanja wa wakubwa kutanua 'influence' zao.

Hawa wakubwa wanauza 'values' zao zienee hata huku kwetu, tuwe kama wao, hata katika mambo ambayo kwetu tunaona hayatufai; kama hilo la ushoga. Mama akitaka kunyonyesha mtoto, akajifiche mahala, kwa sababu kwao kuonyesha titi tu ni kuwa uchi,; lakini kutembea mitaani amevaa kichupi ni sawa kabisa! Ukiwa na wake wawili, au zaidi, wewe upo nje ya 'values' zao, hujastaarabika, na ukiomba hata kwenda kuwatembelea tu huko kwako hupewi makaratasi, lakini kama wewe ni shoga huna tatizo nao.
haya ndiyo yanayopiganiwa sasa hivi na hizi 'demokrasia' tunazohimizwa tuzitekeleze kama tunataka kuwa 'wastaalabu' kama wao.

Laa, naona nitaandika gazeti humu. Inatosha mkuu 'zitto junior', nashukuru kwa kunikumbuka na kuniita nichangie humu. naona mada hii nishachangia sana.
 
Wapi Mama Samia hajasema sheria zinakataza? Wapi tumepewa misaada kwa kigezo Cha kulinda haki za mashoga? Mie nakumbuka tumewahi nyimwa pesa kwa kuzuia mabinti wajawazito kurudi shule na pia kuiba kura uchaguzi wa 2015 ila sijawahi sikia tumenyimwa msaada kisa sijui Kuna sheria ya kupinga ushoga.

So tusifungamanishe.... Hata Biblia ya King James tunatumia wakristo ni zao la James V aliyekua shoga. Je Ina maanisha sisi wakristo tuna support ushoga? Same to Wanao print bible za NIV inayotumika zaidi kwa Sasa ni Zondervan or Harper-Collins ambao Wana support ushoga pia ila sijawahi sikia tumeambiwa tusisome biblia kisa zimechapishwa na printer za mashoga!!

Huu unafiki ni kwa faida ya nani? Why tufungamanishe demokrasia na ushoga au misaada na ushoga?
Cc Proved mtu chake Kalamu
Jitahidi ufungue mabano, jamaa wanatoa misaada kwa kigezo cha "haki za binadamu" na huo ushoga ndio unaingilia huko, wala usisubiri kumsikia Samia sijui anasema/atasema nini..

Unaonekana hujaelewa/ umeisahau title ya huu uzi, soma tena ujikumbushe..
 
Mkuu it doesn't matter Mama Samia aseme au asiseme the thing is sheria imekataza maadam bunge ndio limeitunga maoni ya Mama Samia whether akubali au akatae hayawezi affect msimamo wa nchi. Ipo clear ukikamatwa ni miaka kadhaa jela sasa mnataka asemeje wakati hajaulizwa Hilo swali? Au ulitaka ashike mic aseme Kamala hatutaki ushoga bila kuulizwa?? Huko si kujishtukia bila sababu
 
Hivi watanzania wanaelewa maana ya demokrasia na haki za binadamu kama zinavyofahamika na marekani? Kwa marekani demokrasia na haki za binadamu zinaambatana na haki za mashoga almaarufu kama LGBT!! Ukikubali demokrasia na haki za binadamu zinazoigiwa debe na marekani duniani kote maana yake ni kukubali haki za mashoga! Misaada hii iliyoahidiwa ya mamilioni ya dola za marekani itatekelezeka kwa masharti ya uhuru wa haki za binadamu ikiwemo ya LGBT! Hii ni hatua ya kwanza ambayo lugha ya awali inayotumika hadharani ni DEMOKRASIA NA HAKI ZA BINADAMU!! Wakati wa kutaka kupokea hiyo misaada ndio ufafanuzi wa demokrasia na haki za binadamu kwa mujibu wa marekani hufuata na hapo ndio suala la haki za mashoga/LGBT hujitokeza!! Je tutakua na ubavu wa kukataa misaada hii lukuki?? Yetu macho!! Ila Malawi walishindwa wakajikuta wanahalalisha ushoga rasmi!!

Taarifa ya Marekani iliyotolewa rasmi kuhusu makubaliano ya demokrasia na haki za binadamu hapa Tanzania wakati wa ziara ya makamu wa rais wa Marekani hapa nchini ni hii hapa:

• Kuimarisha Haki za Kidemokrasia na Utawala Bora:
Katika maombi yake ya bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024, utawala wa Biden-Harris umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 kugharimia programu zinazohusu demokrasia, haki na utawala nchini Tanzania. Hili ni ongezeko kubwa la msaada kwa jitihada za Tanzania katika eneo hili. Zaidi ya hayo, USAID imeichagua Tanzania kama nchi itakayopokea usaidizi kusaidia jitihada zake za kukuza ushiriki wa wanawake na wasichana katika uongozi wa kiraia na kisiasa, hivyo kutoa takriban Dola za Kimarekani Milioni 1 za ziada kugharimia programu hizi kuanzia mwaka huu.

Huko GHANA Makamu wa rais wa Marekani ambako ndiko alikoanzia ziara yake barani afrika hakumung'unya maneno kuhusu mfungamano wa demokrasia na haki za mashoga-LGBT. Huu hapa msimamo wake wakati anaongea na Rais wa GHANA:

In a joint press conference with President Nana Akufo-Addo on Monday, Harris did not directly address the bill, but affirmed that LGBT rights were “an issue that we consider to be a human rights issue, and that will not change.”
Last week, National Security Council spokesman John Kirby told reporters at the White House that LGBT rights were “something that’s a core part of our foreign policy, and it will remain so.”

Tusijidanganye kuwa msimamo huo wa Marekani kuhusu haki za binadamu na ushoga utabadilika hapa Tanzania tofauti na kwingineko!! Wamesema kabisa kuwa hilo halitabadilika na ni sehemu muhimu sera ya nchi za nje ya marekani!!

Watanzania tusije tukajikuta tumeingia mikataba kama enzi za kina MANGUNGU!! Tutaambiwa ukipenda boga penda na ua lake!!! Kwa mujibu wa Marekani huwezi ukatenganisha haki za binadamu na haki za mashoga!! Marekani ikiongea haki za binadamu ujue inaongea haki za mashoga. Tafadhali tusijitoe ufahamu tukajifanya hatujui Marekani anamaanisha nini anaozungumza habari ya demokrasia na haki za binadamu!!
Shida itakua ulafi wa vigogo kwani wametegwa. Hela za demokrasia na haki za binadamu ni hongo kwa vigogo. Ni hela za kuliwa na vigogo huku kiasi kikubwa kikipitishwa kwa ngos kwa lengo na masharti ya kueneza na kukuza ushoga. Marekani walaaniwe kwa hili.
Kwa hivyo kinachotakiwa ni kuachana na hiyo misaada ya demokrasia na eti kukuza haki za binadamu kwani kwa uroho wa vigogo wataipokea huku masharti yake ni kuleta uchafu mtupu kwa jamii yetu.
 
Mkuu it doesn't matter Mama Samia aseme au asiseme the thing is sheria imekataza maadam bunge ndio limeitunga maoni ya Mama Samia whether akubali au akatae hayawezi affect msimamo wa nchi. Ipo clear ukikamatwa ni miaka kadhaa jela sasa mnataka asemeje wakati hajaulizwa Hilo swali? Au ulitaka ashike mic aseme Kamala hatutaki ushoga bila kuulizwa?? Huko si kujishtukia bila sababu
""Ninacheka" na "Kushangaa" kuhusu andiko lako hili; kwa bahati mbaya JF hawaruhusu yote mawili kwa pamoja kuonyeshwa.
 
Ukiheshimu haki za binadamu automatically lazima uheshimu haki za mashoga. Maana nao ni binadamu.
Ushoga siyo haki bali ushoga ni ukosefu wa maadili na ni dhambi!!! Lazima nyeusi tuiite nyeusi na nyeupe tuiite nyeupe.
 
Back
Top Bottom