Huko USA huwezi kutenganisha haki za binadamu na haki za mashoga/LGBT!

Mimi kama sishiriki mambo ya ushoga ya nin inisumbue hakiri sioni haja ya kupoteza mda kujadili mambo haya kila cku
 
hili suala linaenda kdg kdg lkn ,baada ya muda fulani tutakuwa tushalielewa,,ni kama UKMWI NA CONDOM wakati ,wanaanza kuelimisha ilikua kama ngumu hv ,ila baadae sasa... MUHIMU jamaa wametia mzigo, na wabongo wenye NGOs wanavyopenda hela mbn wataziomba na kutetea ushoga kwa mwavuli wa HAKI ZA KIBINADAMU
 
Hilo zee ni puuzi sana.
 
Utakuwa mganga wa kienyeji mpiga ramli, unayejidai kujua vichwa vya wengine vinafikiria kitu gani bila wewe kuambiwa, hopeless old man!.

Tell us, wapi na lini Lissu na Lema waliwahi support ushoga?
 
Mkuu tatizo viongozi wa wadanganyika wanajizima data kujifanya hawajui marekani na mabeberu wote wa ulaya huwa wanamaanisha nini wanapoongelea kuhusu haki za binadamu.........na huu unafiki ni kutokana na kutegemea kupata favour na misaada kutoka kwa hao mabeberu.......hii ni moja ya laana za umaskini.
 
Ni kweli mkuu ni swala la muda tu, Tena the more wanalijadili ndio wanalipa mileage na watu kuwa curious zaidi. They call it Streisand Effect!!
 
Mmarekani huwa anakuja Kufukuwa ?....msijifiche kwenye kivuli cha Mmarekani
Zameni kwenye Tafiti mje na Majibu Kamili
Kuna Tabaka linajihami .....
 
Shida sio demokrasia imeanzia wapi. Hayo mambo ya history yatupilie mbali, tuzungumzie dunia hii ya leo, tunayoishi sasa.
Kwa sasa U.S.A ndio father of democracy
Sasa kwanini unafungamanisha demokrasia na ushoga? Ni hivi mashoga wote wanapenda demokrasia ila SIO wanademokrasia wote wanapenda ushoga. Kama tu useme wasagaji WOTE ni wanawake ila SIO wanawake WOTE ni wasagaji?

Hapo umenielewa
 
Hii tabia imezuka sana, utasikia "tungekua na upinzani imara kusingekuwepo mgao wa umeme"..... Sasa unajiuliza anayekata umeme ni Mbowe ama Serikali?
 
Hizo sheria hata kama zipo mbona bado tunatongozwa na misaada yao na tumekaa kimya, kwanini tusiwaambie sheria zetu zinakataza? jana Samia kagoma maswali ya waandishi, unajua alikimbia nini pale?
Wapi Mama Samia hajasema sheria zinakataza? Wapi tumepewa misaada kwa kigezo Cha kulinda haki za mashoga? Mie nakumbuka tumewahi nyimwa pesa kwa kuzuia mabinti wajawazito kurudi shule na pia kuiba kura uchaguzi wa 2015 ila sijawahi sikia tumenyimwa msaada kisa sijui Kuna sheria ya kupinga ushoga.

So tusifungamanishe.... Hata Biblia ya King James tunatumia wakristo ni zao la James V aliyekua shoga. Je Ina maanisha sisi wakristo tuna support ushoga? Same to Wanao print bible za NIV inayotumika zaidi kwa Sasa ni Zondervan or Harper-Collins ambao Wana support ushoga pia ila sijawahi sikia tumeambiwa tusisome biblia kisa zimechapishwa na printer za mashoga!!

Huu unafiki ni kwa faida ya nani? Why tufungamanishe demokrasia na ushoga au misaada na ushoga?
Cc Proved mtu chake Kalamu
 
Duh!
Nimejifunza jambo jipya hapa mkuu 'zitto junior', juu ya hiyo "Biblia ya King James". Nilikuwa sijui hili.

Bila kutaka kuingia zaidi kwenye mjadala huu, niseme tu kwamba hii misaada tunayopewa ina lengo (au malengo) kwa anayetupa hiyo misaada. Siyo kweli kurahisisha tu kwamba "wazungu wanatupenda" hiyo si kweli.
Kinachosikitisha ni kwamba sisi tunaopokea misaada hii hatuitumii kikamilifu kutujengea uwezo wa kuondokana na utegemezi kwa hao wanaotupa hii misaada yao ili kukidhi malengo yao. Matokeo yake tunaendelea kuwa wapokea misaada na kuendelea kuwa uwanja wa wakubwa kutanua 'influence' zao.

Hawa wakubwa wanauza 'values' zao zienee hata huku kwetu, tuwe kama wao, hata katika mambo ambayo kwetu tunaona hayatufai; kama hilo la ushoga. Mama akitaka kunyonyesha mtoto, akajifiche mahala, kwa sababu kwao kuonyesha titi tu ni kuwa uchi,; lakini kutembea mitaani amevaa kichupi ni sawa kabisa! Ukiwa na wake wawili, au zaidi, wewe upo nje ya 'values' zao, hujastaarabika, na ukiomba hata kwenda kuwatembelea tu huko kwako hupewi makaratasi, lakini kama wewe ni shoga huna tatizo nao.
haya ndiyo yanayopiganiwa sasa hivi na hizi 'demokrasia' tunazohimizwa tuzitekeleze kama tunataka kuwa 'wastaalabu' kama wao.

Laa, naona nitaandika gazeti humu. Inatosha mkuu 'zitto junior', nashukuru kwa kunikumbuka na kuniita nichangie humu. naona mada hii nishachangia sana.
 
Jitahidi ufungue mabano, jamaa wanatoa misaada kwa kigezo cha "haki za binadamu" na huo ushoga ndio unaingilia huko, wala usisubiri kumsikia Samia sijui anasema/atasema nini..

Unaonekana hujaelewa/ umeisahau title ya huu uzi, soma tena ujikumbushe..
 
Jitahidi ufungue mabano, jamaa wanatoa misaada kwa kigezo cha "haki za binadamu" na huo ushoga ndio unaingilia huko, wala usisubiri kumsikia Samia sijui anasema/atasema nini..

Unaonekana hujaelewa/ umeisahau title ya huu uzi, soma tena ujikumbushe..
Mkuu it doesn't matter Mama Samia aseme au asiseme the thing is sheria imekataza maadam bunge ndio limeitunga maoni ya Mama Samia whether akubali au akatae hayawezi affect msimamo wa nchi. Ipo clear ukikamatwa ni miaka kadhaa jela sasa mnataka asemeje wakati hajaulizwa Hilo swali? Au ulitaka ashike mic aseme Kamala hatutaki ushoga bila kuulizwa?? Huko si kujishtukia bila sababu
 
Shida itakua ulafi wa vigogo kwani wametegwa. Hela za demokrasia na haki za binadamu ni hongo kwa vigogo. Ni hela za kuliwa na vigogo huku kiasi kikubwa kikipitishwa kwa ngos kwa lengo na masharti ya kueneza na kukuza ushoga. Marekani walaaniwe kwa hili.
Kwa hivyo kinachotakiwa ni kuachana na hiyo misaada ya demokrasia na eti kukuza haki za binadamu kwani kwa uroho wa vigogo wataipokea huku masharti yake ni kuleta uchafu mtupu kwa jamii yetu.
 
""Ninacheka" na "Kushangaa" kuhusu andiko lako hili; kwa bahati mbaya JF hawaruhusu yote mawili kwa pamoja kuonyeshwa.
 
Ukiheshimu haki za binadamu automatically lazima uheshimu haki za mashoga. Maana nao ni binadamu.
Ushoga siyo haki bali ushoga ni ukosefu wa maadili na ni dhambi!!! Lazima nyeusi tuiite nyeusi na nyeupe tuiite nyeupe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…