Huku ndoa yake ikipumulia mashine, Jack Wolper apata bwana mpya!

Huku ndoa yake ikipumulia mashine, Jack Wolper apata bwana mpya!

Laki si pesa kaingia 🤣🤣🤣🤣

Mbona mzuri tu jamani na anajua kutafuta hela mchagga yule?
Kuliko hata huyo K-Lyn uzuri wa bure!
Unaoa mwanamke ambae mpaka ndugu na wazazi wako wanawajua wanaume zaidi ya 10 waliolala nae? Hivi ndoa mnaichukulia poa poa ? Unadhani wazazi watakubali mtoto wao aoe mwanamke malaya anaejulikana na kila mtu? Hata mimi nikisikia ndugu yangu kaoa kahaba nitaenda kumchapa makofi
 
Ile kipindi anakaa kwenye benchi la wajane pale msibani (wakawa wamejipanga wajane wanne sijui watatu) si alikua na nenga 😁
Hapana, ilikuwa bado dear.

Alimuacha Nenga akafuata maokoto, jasiri alipotutoka ndio akarudi kwake sasa japo alipata shida maana Nenga hakumpokea kirahisi alimkazia kwanza.
 
Unaoa mwanamke ambae mpaka ndugu na wazazi wako wanawajua wanaume zaidi ya 10 waliolala nae? Hivi ndoa mnaichukulia poa poa ? Unadhani wazazi watakubali mtoto wao aoe mwanamke malaya anaejulikana na kila mtu? Hata mimi nikisikia ndugu yangu kaoa kahaba nitaenda kumchapa makofi
Hapa umeongea kama mwanaume, na mbaya zaidi mwanamke huyo awe kakuzidi umri kwa mbali!

Sijui Rich kilimkuta nini? Ndio mapenzi tena.
 
Hapana, ilikuwa bado dear.

Alimuacha Nenga akafuata maokoto, jasiri alipotutoka ndio akarudi kwake sasa japo alipata shida maana Nenga hakumpokea kirahisi alimkazia kwanza.
Alikuaga na nenga tayari ndo wakaachiaga na koneksheni ya kile kyupi....haya kaenda kwa marehemu huku wapenzi watazamaji tunajua kabisa "kosa la marehemu" halafu tena akarudi kwa nenga, ina maana hapo wote....aaahhh au basi tu
 
Sema ukweli Mkuu, wewe ungepewa Wolper kama mke ungekataa?
Nakataa ....ilishanitokea kwa wanawake wawili wote wake za watu na nilichomoa,mmoja huyo ni mweusi na kafungasha haswa mwengine alikuwa ana miliki grocery,huyu alikuwa mwembamba ana kababy face.

Mimi kwanza mke wa mtu na muogopa,kwenye makuzi yangu nilisha shuhudia jamaa wawili wakichapiwa wake zao, honestly niliwaonea huruma kwani walikuwa wanapitia magumu sana.
 
🤣🤣🤣🤣 kumbe una vituko hivi?

Mimi katika wadada maarufu namkubali sana Maua Sama, kanajielewaaa.

Alipewa somo na Vanessa hajamwangusha, kanakula kimyakimya!
vituko..!!🤭🙈

ukiwa na 'umaarufu' ama 'uzuri', hakikisha unakuwa 'smart', hapo ndiyo utaona matunda ya hiyo 'zawadi', different from that my dear you'll be pathetically doomed...!!
 
Nimekuja kugundua Wopler anapenda vivulana vidogo, wakubwa huwa ni madanga tu.

Refer Harmonize, kale kavulana sijui brown, mume Rich ndio hivyo nae mdogo…
Bila shaka moyo wake unastahimili sana dhoruba za mapenzi. Kama Zari mama Tiffa.
 
View attachment 2831270Ndoa ndoano! Mambo sio mambo!

Muigizaji aliyegeukia biashara, mwanadada Jackline Wolper Massawe ‘Wolper’ inaripotiwa kupata bwana mpya baada ya ndoa yake kukumbwa na sintofahamu nyingi.

Ikumbukwe Wolper alifunga ndoa takatifu na aliyekuwa baba wa mtoto wake Richard ‘Rich Mitindo’ 19/11/2022.

Wawili hao walioonekana kuwa na huba la moto, shatashata lililokolea nazi enzi za uchumba wao uliopelekea Wolper kufikia uamuzi wa kumzalia kabisa mtoto Rich hata kabla ya kufunga ndoa.

Mara nyingi walionekana wenye furaha na mapenzi tele, wakipop champagne kila uchwao na kushona sare!
Wambea na wenye husda walinyanyasika vya kutosha!

Jinamizi liliyasogelea mapenzi yao baada ya kufunga pingu za maisha, na Wolper kubarikiwa mtoto wa pili.

Ilianza kuripotiwa ndoa kuingia mdudu baada ya mumewe kuonekana akila maraha China, mbaya zaidi kwa kipindi kirefu aliendelea kubaki huko bila kurejea nchini ilipo familia yake kitendo kilichozua minong’ono!

Wolper alishindwa kujizuia, akaanza kuongea mengi ya uchungu hata alipopata nafasi ya kuhojiwa na waandishi aliongea ambayo wengi waliyatafsiri kama alama nyekundu ktk ndoa yao.

Baada ya kipindi kirefu cha mumewe kuwa nje ya nchi, ni wazi Wolper uvumilivu umemshinda nae kaamua kujipa ‘raha’ kwa kutoka kimapenzi na mwanaume anayefahamika kama Vincent Azrone almaarufu G Nex.

Mwanaume huyo imebainika kuwa ni meneja katika ukumbi maarufu wa starehe, Havoc Night Spot uliopo Masaki jijini Dar Es Salaam.

Wapenzi hao wameonekana mara nyingi pamoja, hadi katika sherehe ya kuzaliwa kwa mwaume huyo, wawili hao walikaa pamoja bila kificho!

Taarifa za uhakika ni kwamba G Nex yeye bado hajaoa, na kiumri anaonekana mdogo kuliko Wolper.
Mara nyingi ameonekana akiwa anaendesha gari yake Toyota Crown nyeusi.

My take; Wolper, najua ilivyo vigumu kuishi ktk stress za mapenzi na ndoa kwa mwanaume asiyeeleweka.

Sitaki kukuhukumu kwamba ulikosea kuolewa na kijana mdogo kwako kiumri ambaye damu bado ya moto anahitaji kufanya mengi kama ambavyo wewe ulifanya kwa wakati wako…

Nakuombea kheri, haya yawe ni mapito mpate kuyaweka sawa na mumeo, ndoa na iheshimiwe na watu wote!

Pichani ni mpenzi mpya mjini wa Jack Wolper, Vincent Azrone ‘G Nex’

Wenu katika ubuyu,

Nifah.
Wolper na Rich mitindo hata hawaendani couple yao sikuwahi kuipenda.
 
Back
Top Bottom