Huku ndoa yake ikipumulia mashine, Jack Wolper apata bwana mpya!

Huku ndoa yake ikipumulia mashine, Jack Wolper apata bwana mpya!

View attachment 2831270Ndoa ndoano! Mambo sio mambo!

Muigizaji aliyegeukia biashara, mwanadada Jackline Wolper Massawe ‘Wolper’ inaripotiwa kupata bwana mpya baada ya ndoa yake kukumbwa na sintofahamu nyingi.

Ikumbukwe Wolper alifunga ndoa takatifu na aliyekuwa baba wa mtoto wake Richard ‘Rich Mitindo’ 19/11/2022.

Wawili hao walioonekana kuwa na huba la moto, shatashata lililokolea nazi enzi za uchumba wao uliopelekea Wolper kufikia uamuzi wa kumzalia kabisa mtoto Rich hata kabla ya kufunga ndoa.

Mara nyingi walionekana wenye furaha na mapenzi tele, wakipop champagne kila uchwao na kushona sare!
Wambea na wenye husda walinyanyasika vya kutosha!

Jinamizi liliyasogelea mapenzi yao baada ya kufunga pingu za maisha, na Wolper kubarikiwa mtoto wa pili.

Ilianza kuripotiwa ndoa kuingia mdudu baada ya mumewe kuonekana akila maraha China, mbaya zaidi kwa kipindi kirefu aliendelea kubaki huko bila kurejea nchini ilipo familia yake kitendo kilichozua minong’ono!

Wolper alishindwa kujizuia, akaanza kuongea mengi ya uchungu hata alipopata nafasi ya kuhojiwa na waandishi aliongea ambayo wengi waliyatafsiri kama alama nyekundu ktk ndoa yao.

Baada ya kipindi kirefu cha mumewe kuwa nje ya nchi, ni wazi Wolper uvumilivu umemshinda nae kaamua kujipa ‘raha’ kwa kutoka kimapenzi na mwanaume anayefahamika kama Vincent Azrone almaarufu G Nex.

Mwanaume huyo imebainika kuwa ni meneja katika ukumbi maarufu wa starehe, Havoc Night Spot uliopo Masaki jijini Dar Es Salaam.

Wapenzi hao wameonekana mara nyingi pamoja, hadi katika sherehe ya kuzaliwa kwa mwaume huyo, wawili hao walikaa pamoja bila kificho!

Taarifa za uhakika ni kwamba G Nex yeye bado hajaoa, na kiumri anaonekana mdogo kuliko Wolper.
Mara nyingi ameonekana akiwa anaendesha gari yake Toyota Crown nyeusi.

My take; Wolper, najua ilivyo vigumu kuishi ktk stress za mapenzi na ndoa kwa mwanaume asiyeeleweka.

Sitaki kukuhukumu kwamba ulikosea kuolewa na kijana mdogo kwako kiumri ambaye damu bado ya moto anahitaji kufanya mengi kama ambavyo wewe ulifanya kwa wakati wako…

Nakuombea kheri, haya yawe ni mapito mpate kuyaweka sawa na mumeo, ndoa na iheshimiwe na watu wote!

Pichani ni mpenzi mpya mjini wa Jack Wolper, Vincent Azrone ‘G Nex’

Wenu katika ubuyu,

Nifah.
Maokoto
 
ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya mapenzi ya leo yanashikiliwa na pesa. Na hii ni kwa rika zote. Bila pesa ni ngumu mahusiano kudumu hata kama mngekuwa mnapendana vipi. Ni wachache sana tena sana wanaweza kushindana na tamaa ya pesa. Ndo maana wadada kwa wakaka, pesa ikishaingia kweny equation, penzi lipo hatarini.
mwenyezi Mungu atusaidie.
Kizazi chetu hiki kinacho endekeza sana pesa ila wazee wetu ni tofauti kabisa. Nimeshuhudia wazee wengi kitaa wakiwa pamoja kwenye nyakati zote na still bado wanapendana.
 
Nimekuja kugundua Wopler anapenda vivulana vidogo, wakubwa huwa ni madanga tu.

Refer Harmonize, kale kavulana sijui brown, mume Rich ndio hivyo nae mdogo…
Wolper hakuolewa Kwa mapenzi,aliolewa ila awakomeshe mtaa Wa Saba
Richie alioa kukurupuka (sijui NAE ni Mchaga yule)mara nyingi hawatelekezi watoto Wao Wana mapenzi Kwa watoto,mwisho wamejikuta hawapendani hapo mfarakano lazima
 
Wolper hakuolewa Kwa mapenzi,aliolewa ila awakomeshe mtaa Wa Saba
Richie alioa kukurupuka (sijui NAE ni Mchaga yule)mara nyingi hawatelekezi watoto Wao Wana mapenzi Kwa watoto,mwisho wamejikuta hawapendani hapo mfarakano lazima
Mbona kama alionesha kumpenda sana Rich? Ukisema alikuwa anataka watoto zaidi nitakubali.

Rich kumpenda Wolper sina uhakika, sijawahi kumuona deep kihivyo.
 
cocastic, hebu fanya uje huku! Kuna ubuyu wako bado wa moto kabisa umeletewa!! Sisi wengine tuko Kijijini huku, na huu umri wetu; tunaona [emoji294][emoji93][emoji92][emoji94] tu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] uduguu nna majukumu lukukii, sasa mda wa kushusha gazeti la udakuu nakosaa.

Mwakani kila exclusive naiweka hapaa
 
Nifah inasemekana Wolper aliwahi kukuta meseji richi anabebishana na kidume mwenzie...baby baby nyingi. Inasemekana [emoji2]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila watu jamaniii, mbna yeye mama mnuko anabebishana na wanawake wenzie.

Cha ajabu nn wote wanajuana.
 
Alikuaga na nenga tayari ndo wakaachiaga na koneksheni ya kile kyupi....haya kaenda kwa marehemu huku wapenzi watazamaji tunajua kabisa "kosa la marehemu" halafu tena akarudi kwa nenga, ina maana hapo wote....aaahhh au basi tu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila wee eve utakufa umechoka sana wallah
 
Heshima yako Mwenyekiti gelofriend.

Kipindi cha koneksheni ya kyupi; mama Naya alikuwa na jasiri muongoza njia. Yaani koneksheni ilitoka baadaye wakiwa wameshaachana. Baba Naya mwenyewe alisema alihisi kwa influence ya jasiri; ile issue ingeweza kumaliza career yake kabisa. Lakini jasiri alimsaidia sana hadi wakapata source ya koneksheni; na akawaomba tu wamsamehe aliyewavujishia video yao. Walikuja kurudiana baadaye sana after jasiri kufafiki, na mama Naya alipambana sana kurudi kwenye maisha ya baba Naya as tayari alikuwa na binti mwingine. Those two; mimi huwa naona wanapendana kweli
Kwan umesahau giggy alisemaje ktk kuwapatanisha nenga na nandy kule bukoba kwa jasiri?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom