Huku ni kukomoana, sijawahi kuona wala kusikia kama hili duniani, TRA mjiangalie

Itakuwa figisu tuu mara ya mwisho nimeomba Tax clearance na kampuni ilikuwa na deni la 140mio plus na wakanipa mbona
 
Ungeuliza watu kwanza. Ohh ona sasa kimekulamba.
 
Mbona unakuwa kama Mkopo 😅
 
Reactions: apk
Ila naona serikali wanazingua sana kazi tu kujifungia maofisini, unajua nini, unaweza kuongea mengi mwisho wa siku ukawa unapigia mbuzi gitaa. Tutaenda nao hivyo hivyo wanavyo taka. Hii nchi watu wake wamezoea wizi.
 
Reactions: apk
Halafu eti Huwa wanashangaa kwanini nchi hii walipa Kodi ni 9% tu ya watanzania wote... Hawajui kwamba tatizo la idadi ndogo ya walipa Kodi linaanzia kwao.
Hivi mtu na akili zake na usomi wake na unakuta katokea maisha ya chini utasema wanashangaa kwamba hawajui, wanaelewa sana kodi wanazo kadiria wananchi sio rafiki kabisa
 
Ndio maana nafunga biashara nianze kukimbizana nao na mie angalau nitajirike sasa
Kwa nini ufunge biashara? Hapa kilichotokea ni kukiuka sheria kwa kutolipa tarehe husika. Hesabu hiyo ni hasara lipa hiyo fine pamoja na wanachostahili.

Cha kukushauri kwa kuwa tayari una faini kwa kuwa umevusha mwezi Unaweza amua kuizungusha hiyo pesa mpaka tarehe 28 huko ndio uwalipe pmoja na fine ila usivushe kwenda mwezi wa pili utakutana na penalty nyingine. Huenda ndani ya wiki mbili inaweza kuwa imekuletea hata 40,000 au zaidi ikitegemea biashara yako.

Kufunga biashara kwa changamoto ya siku moja utakuwa uzembe wa hali ya juu.
 
Kaka ukiwakuta hao wakusanya Kodi walivyo na juhudi za kukerembesha watu hili walipe Kodi, unaweza ukasema ni watu wenye uchungu sana na taifa hili... Kumbe ni majizi tu yanayotumia uniform za utumishi kuwaibia wanainchi... Na pesa yote inayokusanywa inaibwa kimatabaka, kwanzia Kwa Mwigulu nchemba mpaka Kwa vidagaa wa chini(Tax officers).

Halafu Huwa wanafikiria kumfungia mtu biashara ndio sululisho sahihi, hawajui kwamba waathirika wakubwa ni wenyewe Kwa kukosa mapato na pesa za kuiba
 
Na wewe unakadiriwaje kodi kubwa unakubali kulipa? Hio kodi kwa hio biashara ni kubwa
 
Tra inasababisha wananchi wanakua wajanja,mambo yanayofanyika na vijana wa tra ni balaa,kodi inaumiza
Double taxation nayo ni tatizo
TRA kuweni na mipango mizuri ya kuwasaidia wafanyabiashara ili mkusanye mapato mengi zaidi na si kukandamiza,
Kuna ujinga mwingi sana unafanyika na kina zakayo na tunajua ,na mpaka kwa majina lakini jirekebisheni
 
HAWA JAMAA NI BURE KABISA KWANZA HAWAKUPI ELIMU ILI UWEZE FANYA BIASHARA NA KULIPA KODI KIRAHISI WANACHOTAKA WAO NI UKOSEE ILI WAKULIME

HAWA JAMAA NI BURE KABISA KWANZA HAWAKUPI ELIMU ILI UWEZE FANYA BIASHARA NA KULIPA KODI KIRAHISI WANACHOTAKA WAO NI UKOSEE ILI WAKULIME
Mkuu Mimi Niko kwenye biashara na mwaka wa 3 huu Mimi nachojua kwenye makadirio inategemeana na wewe kwenye maelezo yako na jamaa anaekukadiria una haki ya kukataa kama umekadiriwa kodi kubwa ambao huwezi kulipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…