Huku ni kukomoana, sijawahi kuona wala kusikia kama hili duniani, TRA mjiangalie

Yaani ni kuviziana na kukomoana. Umesahauvku file kikodi cha 500,000/- utapigiwa hesabu na interest tangu 2015 uliyisahau ku file. Sasa huu kama sio uchawi ni nini? Yaani nikiona hawa watu najisikia kutapika kabisa.
 
Hivi mnadhani wanapojisifu kuvuka lengo la makusanyo inakuwaje? ni kukamua haswa na kudhurumu ndani kwa ndani ,yaani punda afe mzigo ufike
 
Nafunga biashara kihalali, naenda kufanya biashara kitaalamu kama wafanyavyo wengi halafu tuone nani atapata na nani atakosa, hii tra imezidi sana kuonea wanyonge,

Nilienda mwenyewe tra na kurasimisha biashara ya mtaji wa mil saba ndio nipigwe faini kubwa kuliko deni?
Uzalendo huo umenishinda

Asante kwa ushauri
 
Sawa kila la heri ila kuna level ukifika tu utajikuta uko mikononi mwao
 
Yaani ni kuviziana na kukomoana. Umesahauvku file kikodi cha 500,000/- utapigiwa hesabu na interest tangu 2015 uliyisahau ku file. Sasa huu kama sio uchawi ni nini? Yaani nikiona hawa watu najisikia kutapika kabisa.
Hahaha
 
Mkuu pole sana.
Umejaribu kulima mahindi kijijini?
Kule hakuna kodi za mjini.
 
Ccm wezi, wafanyakazi wa serikali wezi, wafanyakazi wa TRA ndio majizi makubwa unawalipa kodi ya nini hao wangese, dawa ni kukwepa mpaka wakukamate...
 
Je, ilitoka Taarifa Kwa mamlaka husika juu ya Madhira yako ya kiuchumi na mategemeo yako ya uchelewaji Wa ulipwaji Wa Deni???

Sasa umepangwa nyumba ya Mtu, Mda Wa kulipa na tarehe zinakaribia Mpaka zimepita umwvunga Tu kana Kwamba nyumba ni Yako, mwenye nyumba kaamua kukurushia Vitu nje unaanza kulalamika kuwa ni mbaya.

Watanzania tunatabia ya kuchukulia Vitu poapoa...

Tanzania ni nchi salama Kwa Uwekezaji, Biashara na ujasiliamali tena Kwa Kodi nafuu.

Nchi zingine za watu, Sasa hivi ungekuwa unaangaika na kutafuta mawakili. Na wakati huo Kodi ni 35% bado mapenati.

Tusikimbilie Tu kulalamika, Je, tulijaribu kutimiza wajibu itupasvyo??
 
Shida ni kujazana ujinga, mada za kodi zinataka uelewa wa sheria za kodi.

TRA awawezi amka asubuhi na kuamua wanakudai kiasi gani, sheria lazima itasema ukichekewa kulipa how much they can charge you.

Laki nne kwa mwaka, wewe ni mlipa kodi wa aina gani?

Kodi zipo tofauti VAT na income tax.

VAT Tanzania ulipi kama una mauzo ya tsh 200 million. Income Tax uwezi pangiwa it’s based on percantage.

Mada ni hadithi tupu.

Labda elezea hiyo kodi gani ambayo TRA wanaweza panga.

Uongo mtupu
 
Hii taasisi for the most part inaendeshwa ki unprofessional sana. Kuna mwaka nilienda kumsajilia jamaa yngu biashara yake. Nikafika nikawaelezea vizuri kabisa hawa maafsa mchongo nao wakajidai wamenielewa. Sasa baada ya kuwakabidhi nyaraka zote za mshkaji wakaziingiza kwenye system dakika za mwisho wakaniambia sasa unatakiwa uweke kidole gumba hapo mimi nikashangaa sana!
Nikawauliza hii inakuwaje taarifa za mtu mwingine then mimi niweke biometric zangu si italeta shida? Wakasema hapana haina shida kuthibitisha akaniita kwenye screen kabisa kunionyesha taarifa za jamaa kila kitu kimekamilika..... Kishingo upande nikapunch japo nilikuwa na mashaka sana akilini WTF mistake??
Siku naenda kufungua tin yangu sasa nikiwa wilaya nyingine kabisa ofsa anaangalia kwenye system akaniambia wewe kupata tin kuna changamoto mfumo unakataa namuuliza sababu nini akasema ata yeye hajui. Hangaika sana pale ikabidi nimweleze ile scenario miaka kadhaa nyuma ya jamaa yangu akaniambia nimtajie hiyo tin ya jamaa yalaaaah!.... System inaonesha picha yangu na fingerprint ila majina na taarifa zingine zote za jamaa dah nikasema hii nilijua tu ni bomu hili ila ms*nge yule dada nikamwambia akajifanya hamna tatizo lolote we punch tu kumbe wakati napanch akanipiga na picha aisee

Wenzetu mbele taasisi kama hizi zina WELEDI sana nashangaa huku kwetu sijui ni kama tumerogwa vile... Hii kitu imeniletea shida sana dah sitamani kabisa kukumbuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…