Hukumu Kesi ya Ponda, ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje

Hukumu Kesi ya Ponda, ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje

Status
Not open for further replies.
Muda huu hukumu ndio yasomwa...Mawakili wa utetezi ndio wamechelewa...mmoja yuko kwenye matibabu na mwenzake amechelewa kufika mahakamani. All in all haki na amani kwa pamoja vitaonekana ama kutoonekana...Tuwe na subira na muda mchache ubashiri utakoma na kweli kuwekwa wazi.
 
Mliopo eneo la tukio vp hukumu inaendelea je?
 
BAKWATA msijidanganye kumfunga Sheikh Ponda ndiyo kuendelea na dhulma yenu kwenye mali za waislamu na ndiyo mwanzo wa kuwatumikia viongozi wenu MAGAMBA bila wasiwasi!! Nawahakikishieni kuwa siku zenu zinahesabika laanakum nyie!!!

Bakwata ni kanisa la Mtumishi nani... maana najua wanaowaonea waislamu ni wakristo tuuu.. na Mwislamu hawezi kumuonea mwislamu mwenzake??...
 
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="class: sqtdq, bgcolor: #EDF1F7, colspan: 2"]“More people have been slaughtered in the name of religion than for any other single reason. That, my friends, that is true perversion.”[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]
as4.gif
Harvey Milk quotes
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Leo ndio tarehe iliyopangwa kusikilizwa kwa kesi ya katibu wa Jumuiya na mihadhara ya kiislam sheikh Issa Ponda baada ya kuhairishwa kwa jaji kutofika mahakamani.

Swali la msingi kama wafuasi wake wamefungwa miaka kadhaa jela je huyu kiongozi atasalimika?

Updates:

Ulinzi imeimalishwa mtaa wote naona askari kanzu ndio wengi na wale wa FFU kama vile wanaenda vitani
Yani mnashusha hadhi ya Majaji kiasi hiki? kesi ya mpumbavu kama Ponda ipangiwe Jaji wakati Mahakimu wapo? hivi wewe Great Thinker gani usiyejuwa kwamba Majaji wanapatikana Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa peke yake? Mahakama za chini zina Mahakimu tu.
 
Lema Kesi ya Uchochezi alipewa dhamana,mbona Ponda hapewi kesi hiyo hiyo?Huu ni uonevu na double standard

Mkuu nilikua kwenye mkutano wa Lema wa juzi ngarenaro arusha, Lema aliwaambia wakazi wa arusha wasishangilie Sheikh Ponda kunyimwa dhamana, Lema alisisitiza na kusema kuwa kwa sheria halali inayojali haki za mtuhumiwa sheikh Ponda anapaswa kuwa nje kwa dhamana wakati kesi inaendeleaa.
So nakubaliana na wewe kabisa huu ni uonevu kama alivyosema Lema pia.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kamuwekee dhamana wewe basi mbona unaongea kwa mbali sana wala hujajitokeza kwenda kumdhamini

Lema anadhaminika hebu kamdhamini Ponda uone kama hutaachiwa vumbi halafu ukafungwe wewe kiherere
Kwa hiyo tatizo ni kwamba Ponda haaminiki, hana watu wa kumuwekea mdhamana siyo kweli? na unapo mwambia Ben akamuwekee mdhamana kwani ni lazima awekewe na Ben? kwani Lema aliwekewa mdhamna na Lema? tunacho zungumza hapa ni haki itendeke na siyo magumashi ya CCM angekuwa ni baba yako au mmeo anagombania shamba kisha kakamatwa na kubakiziwa kesi ya ugaidi ungekuwa unaongea huu upuuzi wako...
 
Mdini ni wewe ambaye uko busy na makanisa na parokia..Kwamba hayapo tena endeleeni kujidanganya kuwa yatafutika....Anyway....mimi siko huko nimekuuliza Ponda ana hati ya hicho kiwanja? Jibu ni jepesi tu ndiyo au hapana. Pili Nondo za wenyewe mlipeleka wapi? Haya mengine tusubirie hukumu ila hoja mbili hizo zinahitaji majibu murua.

Issue ya kunyimwa dhamana ilikuwa ni muhimu kwasababu hana kazi aliyokuwa akiifanya mbali na uchochezi na maandamano yasiyo na kichwa wala miguu...Angalau tulipumua na kufanya kazi zetu kwa A mani maeneo ya Kariakoo kila ijumaa.

Kwa hiyo ili udai haki lazima uwe na hati?, kwa hiyo mtu asiekuwa na kazi ni haki kumbabikizia kesi ili akose mdhamana...hivi unatumia akili kweli kufikilia!?
 
Kama Wabunge wangeingilia uhuru wa mahakama kama walivyofanya kwenye kesi ya gaidi LWAKATARE angeweza kutoka, lakini lolote laweza kutokea tusubiri.

inatakiwa Afungwe kabisa maisha, kuwaonea haya watu kama hawa ndo kumetufikisha hapa tulipo. lazma tuitunze amani ya nchi yetu coz ikitoweka hakuna atakaye salimika
:angry:
 
Alikuwa na hati ya hicho kiwanja ? Nondo za wenyewe mlipeleka wapi?


Je unajuwa kuwa kuna mahakama huko Tanzania zinazoshughulikia masuala ya ardhi? Je mahakama ya kisutu ndio yene dhamana hiyo?

usikurupuke katika hili hebu pitia hati ya mashitaka uone ameshitakiwi kwa lipi?

Pole sana
 
Ndugu usiseme wakristo ni wakoloni wa waislamu, hapo utakuwa unakosea, kutumia makandamizo yaliyotokea kwa baadhi ya waislamu isiwe ni chanzo cha fikra yako, kufanya hivyo ni chanzo kingine cha kutofikia muafaka wa maswala kereketwa kwa waislamu (au baadhi ya waislamu)
Utakubaliana nami kuwa kuna baadhi waislamu wanaoishi maisha mema (yasiyo na bughudha) kama vile ilivyo kwa baadhi ya wakristo au baadhi ya watu kutoka tabaka jingine.

Hivi karibuni nimekuwa mfuatiliaji wa masuala ya dini, haswa kusikiliza upande wa waislamu (malalamiko ya video kutoka kwa baadhi ya masheikh) maana huu ni wajibu wa kila raia mwema. Mimi nawapenda waislamu sawa na navyowapenda wakristo wenzangu, Tanzania ni yetu sote bila kujali dini, itikadi, kabila, ukanda, jinsia na tabaka lolote lile, katika hayo masikilizo nimekubali kuwa kuna baadhi ya waislamu walinyanyaswa kutokana na dini yao na hii ni uvunjifu wa katiba (naomba nikiri sijasikiza upande wa pili). Serikali inahitaji kutolea majibu (tafadhali si majibu mepesi)

Utakuabliana nami kuwa suala la Sheikh Ponda ni la kihistoria, na lahitaji hekima katika kulitatua ambayo naamini litawezekana nje ya mahakama. Sababu sheria haingalii kama Ponda anawakilisha watu ambao wanahisia za uonevu bali inaangilia vifungu vinazungumza nini kuhusu suala linalomkabili. Rais ameshakutana na upande wa wakristo, upande wa waislamu utakapofika moja ya agenda iwe suala la Sheikh Ponda hapa ndo mwanzo wa kuanza kulizungumza nje ya mahakama, wawakilishi wa waislamu wasiwe BAKWATA tu bali wale wanaolalamika napenda na Sheikh Ilunga awe mmojawapo

Hitimisho waislamu wa Tanzania waendeleze mapenzi kwa nchi yao hivyo hivyo kwa tabaka lolote lile, tukitumia hekima tutapata majawabu sahihi, kuliko jazba, chuki, na kuendekeza udini

Wenu mpenzi wa nchi ya Tanzania
Heshima Kwako kajima na Usabahia kwa wanaJF;
Uliyosema yana msingi na mwelekeo mzuri, yaleiti kuwa waTanzania wajue nchi hii ni yetu sote na siyo ya Waumini tu.
Kwani imani na uzalendo ni vi vitu tofauti... Ukichambua kwa utulivu na hekima utaelewa.

Mungu ibariki Tanzania na Uinusuru imani za watanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom