Na,
in fact,
hukumu hiyo itachochea siasa za kistaarabu zaidi majukwaani miongoni mwa wanasiasa wa vyama mbalimbali vya siasa na kutokomeza kabisa siasa za uropokaji, porojo, uongo, uzushi, fujo, uchochezi, ukiukaji sharia na upotoshaji Tanzania.
Huenda Tanzania ikaanza kushuhudia siasa za kimkakati zenye agenda na nguvu ya hoja na hivyo kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kwenye maisha ya waTanzania wote. Vibaraka, vibaka na vibwengo wa kisiasa nchini, watatambua sasa, kwamba siasa ni sayansi na sio kubwekabweka tu porojo za kuchochea ghasia, uharibifu na maafa.
Una maoni gani kuhusiana na jambo hili la maana sana kisiasa nchini?🐒
Mungu Ibariki Tanzania