Humphrey Polepole aomba ukumbi wa LHRC afanye mkutano na waandishi wa habari Desemba 11

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Dunia hadaa ulimwengu shujaa, Humphrey na kundi lake la mwendazake walikuwa na mkakati maalum wa kuua mashirika yanayopigania haki za binadamu, walifikia hata kufunga akaunti zao, kesho kaomba ukumbi afanye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Kuwa uyaone, si maghorofa, hana tena fursa ya kutamba katika kumbi za ofisi ndogo Lumumba wala Dodoma, anaombeleza kumbi kwa watu aliowatangazia uadui.
 
Dunia hadaa ulimwengu shujaa, humphrey na kundi lake la mwendazake walikuwa na mkakati maalum wa kuua mashirika yanayopigania haki za binadamu, walifikia hata kufunga akaunti zao,kesho kaomba ukumbi afanye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)....kua uyaone, si maghorofa, hana tena fursa ya kutamba katika kumbi za ofisi ndogo lumumba wala dodoma, anaombeleza kumbi kwa watu aliowatangazia uadui
Atazuiwa kama Nape enzi zile kuitisha press conference

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Dunia hadaa ulimwengu shujaa, humphrey na kundi lake la mwendazake walikuwa na mkakati maalum wa kuua mashirika yanayopigania haki za binadamu, walifikia hata kufunga akaunti zao,kesho kaomba ukumbi afanye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)....kua uyaone, si maghorofa, hana tena fursa ya kutamba katika kumbi za ofisi ndogo lumumba wala dodoma, anaombeleza kumbi kwa watu aliowatangazia uadui
Ana haki ya kutumia sehemu yoyote ya Tanzania ili mradi havunji sheria. Tabia ya kijinga aliyokuwa anashabikia Watanzania wenzake kuzuiwa kutumia Uhuru wao kutoa maoni anapaswa aachiwe ili aone madhara ya ujinga aliokuwa anafanya.
 
Kumba mama nae hataki kupingwa, naona ile kauli yake hatakubaki makosa ya awamu zilizotangulia atupiwe yeye imeanza kufanyiwa kazi kwa vitendo, akiongea na majirani anawalegezea sauti, akirudi kwa wapinzani wake ndani anawatumia wahuni kuwawinda.

Kama ofisi ya urais imemshinda vyema airudishe kwa watanzania kwa wenyewe uitishwe uchaguzi mkuu mwingine maisha yaendelee, Polepole anatumia haki yake kisheria kutoa maoni yake anatakiwa kujibiwa kwa hoja sio vinginevyo.

Naona wengi mnamsema Polepole badala mjiulize atakaefuatia kuwindwa atakuwa nani, alianza Mbowe, leo Polepole, kesho atakuwa nani? ajabu ushabiki umetawala vichwa vya wengi, hapa habari sio sukuma gang vs msoga au Chadema, hao wote ni watanzania, msitengeneze makundi ya kijinga ndani ya hii nchi bila kujua athari zake.

Samia ajue anajukumu la kuongoza wote kwa kufuata sheria za nchi sio kwa maoni au mapenzi yake binafsi, asitake kila mmoja ajipendekeze kwake hata kama hana sababu ya kufanya hivyo, atulie ajue namna ya kuongoza nchi.

Sio atuambie yeye ni Rais mwenye jinsia ya kike, haya maneno yalitakiwa kutumika enzi za wakoloni, asishindane na wasioshindana nae wala asitumie mamlaka yake kuumiza wengine kwa vitu vidogo.
 
Dunia hadaa ulimwengu shujaa, humphrey na kundi lake la mwendazake walikuwa na mkakati maalum wa kuua mashirika yanayopigania haki za binadamu, walifikia hata kufunga akaunti zao,kesho kaomba ukumbi afanye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)....kua uyaone, si maghorofa, hana tena fursa ya kutamba katika kumbi za ofisi ndogo lumumba wala dodoma, anaombeleza kumbi kwa watu aliowatangazia uadui
Usi tukane mamba kabla huha vuka mto.
 
Huyu huwa simsikilizi
 
Back
Top Bottom