Kumba mama nae hataki kupingwa, naona ile kauli yake hatakubaki makosa ya awamu zilizotangulia atupiwe yeye imeanza kufanyiwa kazi kwa vitendo, akiongea na majirani anawalegezea sauti, akirudi kwa wapinzani wake ndani anawatumia wahuni kuwawinda.
Kama ofisi ya urais imemshinda vyema airudishe kwa watanzania kwa wenyewe uitishwe uchaguzi mkuu mwingine maisha yaendelee, Polepole anatumia haki yake kisheria kutoa maoni yake anatakiwa kujibiwa kwa hoja sio vinginevyo.
Naona wengi mnamsema Polepole badala mjiulize atakaefuatia kuwindwa atakuwa nani, alianza Mbowe, leo Polepole, kesho atakuwa nani? ajabu ushabiki umetawala vichwa vya wengi, hapa habari sio sukuma gang vs msoga au Chadema, hao wote ni watanzania, msitengeneze makundi ya kijinga ndani ya hii nchi bila kujua athari zake.
Samia ajue anajukumu la kuongoza wote kwa kufuata sheria za nchi sio kwa maoni au mapenzi yake binafsi, asitake kila mmoja ajipendekeze kwake hata kama hana sababu ya kufanya hivyo, atulie ajue namna ya kuongoza nchi.
Sio atuambie yeye ni Rais mwenye jinsia ya kike, haya maneno yalitakiwa kutumika enzi za wakoloni, asishindane na wasioshindana nae wala asitumie mamlaka yake kuumiza wengine kwa vitu vidogo.