Humphrey Polepole aomba ukumbi wa LHRC afanye mkutano na waandishi wa habari Desemba 11

Humphrey Polepole aomba ukumbi wa LHRC afanye mkutano na waandishi wa habari Desemba 11

Na walifungia billion 4 za LHRC kwa madai zitatumika kusaidia wapinzani
Ngoja na yeye watafreez account zake ndo atatia akili,, asione watu wanamtizama tu akadhani wamelala,,, wanampimia tu,, soon ataanza kusaka vibarua hata vya kupinda kokoto[emoji23][emoji23]
 
Ubunge wake utenguliwe, hatufai kwenye chama chetu
 
Dunia hadaa ulimwengu shujaa, Humphrey na kundi lake la mwendazake walikuwa na mkakati maalum wa kuua mashirika yanayopigania haki za binadamu, walifikia hata kufunga akaunti zao,kesho kaomba ukumbi afanye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Kua uyaone, si maghorofa, hana tena fursa ya kutamba katika kumbi za ofisi ndogo Lumumba wala Dodoma, anaombeleza kumbi kwa watu aliowatangazia uadui.
Pale ni kwa wanasheria.so ni mahali salama zaidi kwake.sema ajenda bado sijaweza bashiri au anaachia ubunge na kuingia kwenye uanaharakati rasmi
 
huyu jamaa namkubali sana.mtu mwenye msimamo NI heri,kuliko Yule ambae ana siasa za umalaya umalaya hivi(in mwal.voice).
Mtu Gani unayemzungumzia wewe ana msimamo? Kama ni huyu Slouli sloule hapana kumbuka yule aliyekuwa kwenye tume ya walioba na huyu wa unaijua vieiti? Wewe unaona wako sawa?
 
Kumba mama nae hataki kupingwa, naona ile kauli yake hatakubaki makosa ya awamu zilizotangulia atupiwe yeye imeanza kufanyiwa kazi kwa vitendo, akiongea na majirani anawalegezea sauti, akirudi kwa wapinzani wake ndani anawatumia wahuni kuwawinda.

Kama ofisi ya urais imemshinda vyema airudishe kwa watanzania kwa wenyewe uitishwe uchaguzi mkuu mwingine maisha yaendelee, Polepole anatumia haki yake kisheria kutoa maoni yake anatakiwa kujibiwa kwa hoja sio vinginevyo.

Naona wengi mnamsema Polepole badala mjiulize atakaefuatia kuwindwa atakuwa nani, alianza Mbowe, leo Polepole, kesho atakuwa nani? ajabu ushabiki umetawala vichwa vya wengi, hapa habari sio sukuma gang vs msoga au Chadema, hao wote ni watanzania, msitengeneze makundi ya kijinga ndani ya hii nchi bila kujua athari zake.

Samia ajue anajukumu la kuongoza wote kwa kufuata sheria za nchi sio kwa maoni au mapenzi yake binafsi, asitake kila mmoja ajipendekeze kwake hata kama hana sababu ya kufanya hivyo, atulie ajue namna ya kuongoza nchi.

Sio atuambie yeye ni Rais mwenye jinsia ya kike, haya maneno yalitakiwa kutumika enzi za wakoloni, asishindane na wasioshindana nae wala asitumie mamlaka yake uumiza wengine kwa vitu vidogo.

Kinachomuumiza leo Polepole ndio mbegu aliyoipalilia wakati wa Magufuli. Kisu alichokinoa ili kuumiza wapinzani sasa ndio kinamkata yeye. Wala usidhani hatujui tunasimamia nini. Mtu yoyote aliyefanikisha utawala wa mabavu wa Magufuli, hata kama anaonewa tutafarijika, na wala hatuungani na Watesi wetu kuwaunga mkono, bali tunafurahia muosha akioshwa. Kwa taarifa yako huyo Polepole hata aje na hoja ya msingi, sio rahisi kupata uungwaji mkono tena kwa wapenda haki, kwani ni mtu anayetaka huruma ya watu baada ya kukosa ulaji. Hakuna mtu atatumika na muhuni kama hiyo Polepole.
 
Kijitu cha hovyo kabisa, anadhani atatikisa dola, noo! Yeye ndiye atatikisika na kung'oka mizizi

Hatuwaungi mkono hiyo dola ya kunyima haki za watu, bali tuna furaha ya ajabu huyo Polepole kukutana na ukandamizaji alioona sawa wengine kufanyiwa kipindi cha utawala wa kidhalimu wa Magufuli.
 
jibu unalo mkuu,hukuona Hadi baadhi ya wabunge wenzie wakawa wanamnanga kisa jamaa,hajapepesa macho kasimamia anachoamini na kinachompa faraja hata uraiani!! msimamo humpa mtu heshima !!
Kwa mara ya pili, umeingia lini mjini?
 
Dunia hadaa ulimwengu shujaa, Humphrey na kundi lake la mwendazake walikuwa na mkakati maalum wa kuua mashirika yanayopigania haki za binadamu, walifikia hata kufunga akaunti zao,kesho kaomba ukumbi afanye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Kua uyaone, si maghorofa, hana tena fursa ya kutamba katika kumbi za ofisi ndogo Lumumba wala Dodoma, anaombeleza kumbi kwa watu aliowatangazia uadui.
Matusi ya nini? Huo ukumbi si atalipia?
 
Kwa maoni yangu hawa wenye madaraka/mamlaka kwa sasa wajifunze kwa Polepole kwamba "Hakuna Marefu Yasiyokuwa na Ncha"
Kama Polepole hakujifunza kwa Membe, Lowasa, Sumaye, Nape, Makamba basi usitarajie na wao walio madarakani watajifunza kwa Polepole. Huyo alikuwa muovu tena aliyekuwa akijisifu kwa naibu hayo.
 
Back
Top Bottom