Humphrey Polepole aomba ukumbi wa LHRC afanye mkutano na waandishi wa habari Desemba 11

Ila pole pole mwanaume, hata Kama ni mnafiki Ila wenzie ndo wanafiki zaidi kina nape, ummy, etc
 
Ujinga ni kwamba ,Wana CCM huwa hawajui kama Dunia inazunguka, uliyemfinya jana leo unaweza mkuta ndio mwenye daraja unapotaka kuvuka
 
Ndio umejigeuza msemaji wa nani sasa? Samia au?

Rudi kule juu soma kila nilichoandika uelewe, usikimbilie kuni quote tu, unaoleta hapa ndio ushabiki nilioukemea kule juu.
Unamkemea nani sasa? Jikemee mwenyewe na mkurupuko wako! Hakuna popote Polepole kazuiwa kufanya hiyo press yake, yeye mwenyewe kaamua kuchagua hiyo sehemu aliyochagua! Hata kwenye tweet yake kaandika hivyo! Naona uliposoma kichwa cha habari na kuona neno "hifadhi" ukakurupuka tu na mgazeti
 

Umemaliza, nchi inatengezwa kwenye makundi badala ya kuwaunganisha wote.

Kazi ya Rais ni kuunganisha nchi wapinzani, watu waliompenda Magufuli, Wamachinga na matajiri, wafanyabiasharavna wakulima, Tanzania bara na visiwani. Yeye kwa sera zake, maneno yake anafanya kinyume chake.

Anajenga makundi, matabaka, hatari sana.
 
Ila pole pole mwanaume, hata Kama ni mnafiki Ila wenzie ndo wanafiki zaidi kina nape, ummy, etc
Huyu ni Mr. Maslahi Binafsi!! Alikuwa anaongea sana wakati wa JK kwa sababu hakuwa kwenye meza ya chakula lakini alipokaribishwa mezani na Magu, akasiliti misimamo yake yote na kuja kuibuka wakati wa SSH baada ya kupokonywa tonge!

Huyo Nape nadhani mnajisahaulisha tu!! Nape alipishana na Makonda huku akifahamu wazi kwamba Makonda ni Mtoto wa Mfalme!! Pamoja na hayo, Nape akaunda tume ya kumchunguza Mwana Mfalme. Wakati Nape anaunda tume kumchunguza Mwana Mfalme, JPM akamuita Makonda kwenye event moja pale Ubungo (siikumbuki vizuri) na akapewa Jukwaa na Rais!! Hatua ile ya Magu kutoa jukwaa kwa Makonda wakati ameundiwa tume ilikuwa ni ujumbe tosha kwamba "don't mess with Golden Boy" lakini bado Nape akaendelea na msimamo wake wa kumchunguza Makonda!

Na hata ukisoma tweets za Nape siku chache kabla ya kufutwa kazi, inaonesha wazi alishafahamu messing with Golden Boy kungem-cost!!

Hizo tweeets ni za March 21, na March 22 akapokea ripoti ya tume aliyounda na akaisoma hadharani! March 23, akatumbuliwa!!! Sikubaliana na Nape kutokana na misimamo yake kisiasa lakini kusema Polepole ana misimamo kuliko Nape, hapana mzee! Polepole ndo kubwa la Manafiki!! Yule leo akipewa cheo, utamshangaa!!
 
Unatumia dola kubaki kwenye dola. Hivi yule mtu anayetumia dola kubaki kwenye dola Yuko wapi?

Wachagga Wana msemo usemao. Siku ukiwa unatafuna nyama usifungue mdomo watu wakaona unakula nyama. Wewe bugia nyama yako taratibu ili hata kesho ukitafuna makande na kufunga mdomo watu watajua huyu Charlie ndio zake.
Jimtu limetolewa huko sijui jalalani (Ni maneno yao wenyewe) halafu anajifanya Yuko ABOVE THE LAW. Hajui kwamba KARMA is real
 
Vieite yake atakwenda nayo!!? Nataka nikaishangae
 
Yupo anatokota kwenye chungu kama makande, laana ya kumgeuka Mzee Warioba na kusema ile rasimu haikuwa ya tume ila ya Warioba na jamaa zake
 

Ameshapata kibali cha polisi ?
 
Mamlaka zimdhibiti huyu kunguru mapema.
 
Ana haki ya kutumia sehemu yoyote ya Tanzania ili mradi havunji sheria. Tabia ya kijinga aliyokuwa anashabikia Watanzania wenzake kuzuiwa kutumia Uhuru wao kutoa maoni anapaswa aachiwe ili aone madhara ya ujinga aliokuwa anafanya.
Anapaswa kuzuiwa...
 
Yupo anatokota kwenye chungu kama makande, laana ya kumgeuka Mzee Warioba na kusema ile rasimu haikuwa ya tume ila ya Warioba na jamaa zake
Yaani jamaa alikuwa nusu waziri mkuu, nusu makamu wa rais, robo rais!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…