Humphrey Polepole: Mambo ya machifu hayana msaada kwa taifa, yanaweza kuleta ukabila na mgawanyiko, yanapaswa kupingwa

Humphrey Polepole: Mambo ya machifu hayana msaada kwa taifa, yanaweza kuleta ukabila na mgawanyiko, yanapaswa kupingwa

CCM wote mnaokosa fursa ndio mlivyo, hata nape na January walitoswa na jiwe walianza nongwa.
Mjifunze nyie watu wa ccm
Usinijumuishe,mimi sijafungwa nyororo na chama chochote ndio maana nakosoa na kupongeza kadri ninavyoona inafaa.
 
Polepole Yuko sahihi maana tunaelekea kwenye shimo la ukabila tena refu kwelikweli
 
Angekuwa smart hata kidogo angefahami Tanzania ina dini zaidi ya hizi mbili za Ukristo na Uislamu, wapo Wahindu, Wabudha n.k pia wapo wasiokuwa na dini kabisa.
Wewe katika maisha yako uliwahi kukutana na mBudha wapi?
 
Humphrey Polepole amesema kuwa

"Mambo ya Machifu yanatusaidia nini kama taifa?nasema jambo hili sio jema,naliona linadhoofisha Utanzania wetu,likiendelea bila kukemewa litaibua tuliyoyazika ya hisia za ukabila, usisi na uwao, Mwalimu Nyerere aliona mbali kukataa haya mambo kwani yataligawa taifa"

"Yapo maeneo uchifu ulishaondoka,haupo. Tulishakubaliana uchifu ni ukoo wenu, mna kiongozi wa ukoo mnazungumza mambo yenu binafsi ya kifamilia leo serikali ikizungumzia uchifu hawa nao wataomba kiongozi wao (wa ukoo) atambulike na apate nafasi huko serikalini"

"Mwalimu Nyerere alikataa jambo hili (uchifu), lina faida gani. Uchifu unataka kutuibulia zile hisia kwamba tuna ukabila kama hakuna wazee wataliona hili jambo, basi mawe yataona"

"Nchi yetu ina wakristo na waislamu, ikitokea mvua imechelewa kiongozi wa serikali huwa anawaomba wakristo kanisani wakaombe na waislamu msikitini wakaombe mvue zinyeshe, lakini huwezi kusikia kiongozi wa serikali akiwaomba washirikina eti wafanye namna mvua inyeshe"

"Kwenye shughuli za serikali ushawahi kuona tunawaita wanaoabudu miti waje kuomba kabla ya shughuli? sasa uchifu wa nini?. Hawa machifu walishafutwa kisheria, tunapowarudisha tunapanda nini?"

"Nenda pale Kilimanjaro, utasema Mareale ndio chifu wao, hapana wako wengi. Kwa hiyo nao wafanye uchaguzi kisha waje kumpata chifu wao wa wote. Kweli tunaenda hivi katika maendeleo"

View attachment 2104792
Wanafiki katika ubora wao, Angekuwa ni hayati JPM anayafanya haya wala wasingefungua midomo yao.
 
Leo mkiwapa nguvu Machifu na Watemi pia tuwe tayari kupoteza baadhi ya vita kama vita dhidi ya Ukeketaji wa Watoto wa kike, Chanjo, Ndoa za wake wengi , kurithi Wake, Ndoa za utotoni, Nafasi ya Wanawake kurithi mali au kufanya maamuzi, matambiko, marufuku za kimila kama usioe kule, kutelekeza/kuua Mlemavu n.k.

Hebu mtuambie ni mila ngapi mnataka zidumishwe na zipi zitokomezwe...nina wasiwasi tunataka kuwasha moto utakaotushinda kuuota.

Hao Machifu na Watemi ndio walikuwa Waanzilishi wa vita dhidi ya kabila na kabila au koo na koo...sasa siku kunachafuka Kijijini utampeleka DC akaongee na Jamii inaomuamini Chifu wao kuliko Mtu mwingine?.

Mpaka wa leo kuna imani za kishirikina nyingi tu zinazoonekana zinatushinda nguvu na Watu wanauana hovyo kila kukicha...leo Machifu wakitaka kudumisha mila na sheria zao mtawadhibiti vipi?.

Itafika mahali Jamii haitojua imsikilize Chifu wa kabila lake au Serikali/Mtaalamu.
 
kwa uoga wa mambo tusiyoyajua.
thinkstupid.png
 
Kila afanyacho Rais kwake polepole ni kibaya tu, polepole unataka nini?. Umefanyika uhuni tu ukapewa ubunge bado huridhiki unataka nini?. Acha ulafi sio wewe tu unapaswa kuwa kiongozi kubali yaishe huo ndio uungwana yasijeyakakupata ukapoteza hata huo umaarufu mdogo ulionao. Urais ni taasisi kubwa acha kushindana nayo.
 
Polepole unaweza kuwa na point nzuri nyingi tu, ila uwanja (room) wa kuisema CCM hauna na hapa ndipo wasiwasi wangu ulipo.
 
Huyu jamaa ni boya sana ana very low IQ.

Ni fact ya wazi kwamba ma-chief walikuwepo kabla ya Tanzania na bado wapo. Hatuwezi kukataa ukweli kwa uoga wa mambo tusiyoyajua. Iko bayana relevance yao sasa ipo kwenye kuifadhi na kudumisha mila na tamaduni zetu nzuri.
He is right! Ukiwadekeza wanasiasa wataturudisha kwenye upumbav! Machifu wapo, wapo wapi? Kwa kazi ipi? Ni hivi hivi kwa tamaa za kupata kila kura na kuungwa mkono, ulaya na US walijikuta wanashambikia ushoga. Siyo kila kitu kilichopo kinastahili kushabikiwa na serikali.
 
Humphrey Polepole amesema kuwa

"Mambo ya Machifu yanatusaidia nini kama taifa?nasema jambo hili sio jema,naliona linadhoofisha Utanzania wetu,likiendelea bila kukemewa litaibua tuliyoyazika ya hisia za ukabila, usisi na uwao, Mwalimu Nyerere aliona mbali kukataa haya mambo kwani yataligawa taifa"

"Yapo maeneo uchifu ulishaondoka,haupo. Tulishakubaliana uchifu ni ukoo wenu, mna kiongozi wa ukoo mnazungumza mambo yenu binafsi ya kifamilia leo serikali ikizungumzia uchifu hawa nao wataomba kiongozi wao (wa ukoo) atambulike na apate nafasi huko serikalini"

"Mwalimu Nyerere alikataa jambo hili (uchifu), lina faida gani. Uchifu unataka kutuibulia zile hisia kwamba tuna ukabila kama hakuna wazee wataliona hili jambo, basi mawe yataona"

"Nchi yetu ina wakristo na waislamu, ikitokea mvua imechelewa kiongozi wa serikali huwa anawaomba wakristo kanisani wakaombe na waislamu msikitini wakaombe mvue zinyeshe, lakini huwezi kusikia kiongozi wa serikali akiwaomba washirikina eti wafanye namna mvua inyeshe"

"Kwenye shughuli za serikali ushawahi kuona tunawaita wanaoabudu miti waje kuomba kabla ya shughuli? sasa uchifu wa nini?. Hawa machifu walishafutwa kisheria, tunapowarudisha tunapanda nini?"

"Nenda pale Kilimanjaro, utasema Mareale ndio chifu wao, hapana wako wengi. Kwa hiyo nao wafanye uchaguzi kisha waje kumpata chifu wao wa wote. Kweli tunaenda hivi katika maendeleo"

View attachment 2104792
Uchifu mafiiii
 
Mama Samia nyie huyu hapo ubunge vitimaalumu akose mbwa huyo
 
Taifa lako wewe na nani? Mkuu utahamishiwa Burundi
machifu si ndo hao hao walioshirikiana na wakoloni kuzinyonya nchi za kiafrika kwa leo bado tunataka kurudi kwenye uchifu ili utusaidie nn.wenzetu wanakimbizana na mifumo ya kisasa ambayo pia ni ya kinyonyani ss tunawaza machifu.tujikite kwenye sayansi na teknolojia yake ili taifa liondokane na unyonyaji wa mifumo kutoka nje.machifu hawana tija,tuna mambo mengi ya kitaifa tunatakiwa kuyajadili ili tutoke hapa tulipo na tusonge mbele.tuachane na hizi minor issues.tuna mambo lukuki ya kujadiliwa kwa sasa lkn machifu si kipaumbele cha taifa letu.
 
Salaam Wakuu,

Polepole ameandika hivi:

"Mambo ya Machifu yanatusaidia nini kama taifa? Nasema jambo hili sio jema,naliona linadhoofisha Utanzania wetu,likiendelea bila kukemewa litaibua tuliyoyazika ya hisia za ukabila,usisi na uwao, Mwalimu Nyerere aliona mbali kukataa haya mambo kwani yataligawa taifa".
View attachment 2104958
MY TAKE:
Urais ni Taasisi. Polepole hauna ubavu wa kushindana na taasisi.

Samia ni Mwenyekiti wa Chama cha CCM, na anachofanya Mwenyekiti ndio maamuzi ya Chama. Polepole huwezi shindana na Chama Ukanshinda.
Ujinga huu unaoandika hapa wa kumuabudu mwenyekiti wa chama, ndio hasa kiu yetu kwamba uishe hapa Tanzania
Chama ni jumuia ya wengi, haiwezekani mmoja afanye Jambo na wote mulibebe eti ni mwenyekiti kaamua,
No sense!
Maamuzi ya chama yanafanywa na chama, sio mwenyekiti wa chama!
Polepole sio mbumbumbu, analijua hilo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom