Humphrey Polepole: Sihami CCM labda Wanitupe nje!, Nimeitwa TCRA nijieleze. Hoja haipigwi rungu bali inajibiwa

Duuuh! Ukiona kila nyuzi ni taratibu taratibu, ujue huyu jamaa kuna sehemu aidha kawabana watu korodani au ana kitu kichwani.
 
Na Kamanda John Heche na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema:

Bora wewe @hpolepole umepigiwa simu. Unajua ni vijana wangapi wa Chadema huko mikoani walitekwa kusafirishwa usiku huku wamefungwa macho?

Nafikiri unakumbuka vijana wetu walivyopigwa na kushikiliwa kwenye mahabusu za polisi kwa siku nyingi kisa kuandika kwenye mtandao maoni yao kuhusu utawala wenu?

Nadhani hujasahau kwamba Lissu alipigwa risasi mchana kweupe akaponea tundu la Sindano, mkamvua ubunge kinyume cha sheria kisa amewambia kwamba ripoti zenu za madini chini ya Mruma na Osoro ni “professorial rubbish “?

Ben Saanane alipoandika kuchambua phd ya mtukufu alipotezwa mpaka leo hajulikani alipo..

Alphonce Mawazo alichinjwa kama kuku, Mwenyekiti Mbowe alipovunjwa mguu mkasema alikua amelewa, Akwilina Akwlini mtoto wa shule aliuwawa mkasema sisi ndio tumemuua. Matukio ya hovyo chini ya utawala wenu ni mengi hayahesabiki.

wewe umepewa heshima ya kupigiwa simu na TCRA alafu unalilia lia ungetekwa kama Roma je?

mimi ni muumini wa haki na Uhuru wa watu lakini nataka ujifunze kwamba what goes around comes around.

Wewe ni sehemu ya uchafu huu kwahiyo kaa kimya.
 
Huyu alikuwa Engineer wa kuiba kura nchi nzima, kutishia na kununua wapinzani ,leo anaongelea haki na demokrasi kwenye kashule kake fake ka uongozi, alikuwa kimya na kupongeza polisi wakati kina Lisu wanapigwa risasi na kina sugu wanafungwa kwa kubambikiwa kesi, mpuuzi sana huyu
 
WAOA USIHAME CCM, NA WALA USIKAE KIMYA, BORA HAUVUNJI SHERIA, SIMAMA HAPO HAPO. USIWAPÉ NAFASI WAHUNI WENYE NIA YA KUWAPOTOSHA WATANZANIA NA SERIKALI KWA MATUMBO YAWO. CCM NI CHAMA CHA WANACHAMA WOTE. HAKUNA MTU MWENYE CHAMA HICHO BINAFSI. WATANZANIA WOTE NI SAWA. UNA HAKI YA KUWAELIMISHA WATANZANIA NA WATANZANIA WANA HAKI YA KUELIMISHWA. WAACHE UHUNI WAWO NA UONEVU WAWO.. WATANZANIA SIO WAJINGA.
 
Huyu Nape tangu utoto wake amelishwa bure, kupitia siasa. Hana elimu, anesukumwa Kama behewa tupu. Bila kubebwa na kupewa kazi bila ujuzi asingejuwa aanzie wapi. He is an opportunist. Eti anacheza gofu tumbo mbele kama kambale kwa Kula vya dhuluma na vya wizi kuwadhulumu waliokuwa wengi. KaMa kuna wahuni Huyu ndiye kinara wa wahunu. Muongo na MUNAFIKI mkubwa . Alimpigia makofi Hayati Maguguli , na Leo anamutukana. Leo anampigia Samia makofi na Kesho atamugeuka. He is not principled, an opportunists muongo na muhuni anapigania tumbo lake. Hajuwi hata katiba ya chama inayosema watu wote ni sawa. Anamuita Polepole, aangalie tumbo lake hakuna kiroboto kama yeye kuwanyonya watanzania damu kwa kutumia mali za wote kujivimbisha kama sangara. PolePole HUNA kosa, usibabaishwe na hawa wezi waliojitajirisha bila ya viwanda
 
Polepole umenipiga block kwenye FB baada kukushahuri uanzishe chama chako chiitwe Sitaikataa Tena Katiba Mpyaa(STKM).. buraza nimekosea nini tena??? ndio maana wamekuzuia u lecturer kwenye university ya uongozi yako.....sawa Mr Vyeetiii
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…