Humu JF kuna kasumba ya kuwa dharau wale join 2020 kuendelea

Mkuu hii issue unapotosha au hukuielewa,

Humu zamani kulikua na nyuzi zinaibuka kutuponda wabeba box,mtu anafungua uzi kuponda wabeba box mpaka unamshangaa,unahisi labda ni stress za maisha tu,ndio anatafuta faraja,

Ila siku hizi badala ya kuponda wabeba box,wao ndio wanaomba connection! Kumbuka kua,hii JF wakati ina anza,member wengi walikua ni diaspora coz ndio walikua na internet connection kabla ya simu kusambaa huko,

Wakati mmezimiwa Internet huko kwenye uchaguzi,humu tulibaki member kama 10 au 15 tu ndio tulikua active,

Diaspora hawakuwahi kumdharau mtu ila watu waliopo huko ndio walikua wanafungua nyuzi za kuwadhihaki diaspora ili pengine wapate faraja tu.
 
Mtu ana haki ya kujisifu, lakini kujisifu na kuwatweza watu wengine ni ulimbukeni, labda kama ni utani.

Juzi kuna jamaa ali-comment kwenye Uzi fulani, comment ilikuwa nzuri tu lakini mwenye Uzi akasema, "joined 2026", hapo tayari hajapima hoja, amepima mtu kajiunga lini πŸ˜‚
 

Disrespect inakuja kwa namna nyingi, wakati mwingine inakuja kama utani mkuu. Utani unaficha vitu vingi wakati mwingine.
 
Disrespect inakuja kwa namna nyingi, wakati mwingine inakuja kama utani mkuu. Utani unaficha vitu vingi wakati mwingine.
Tena usipokuwa makini utani ndiyo njia ambayo watu wanatumia kuonesha dharau, hasa kwenye maisha ya kawaida. Mtu mwenye akili timamu lazima atambue tofauti kati ya utani na dharau.
 
Miaka ya nyuma, wakati tunasoma kwenye shule za wahuni, mwanafunzi wa form four ukimkanyaga wa form two hakurupiki, utasikia anasema, "uwe mtukufu, umeweka mguu wako juu ya wangu", kwa sauti ya unyenyekevu 🀣

Kulikuwa na ubabe wa kifala mashuleni, mi nakumbuka 2003 naanza form one, Kantalamba Boys. Kuna jamaa mmoja wa form six akaja kukagua tranka langu, akakuta kuna blueband, tomato sauce bimkubwa kanipa kutoka home. Akachukua, basi ndio siku nikawa maarufu pale shule. 😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…