Humu JF kuna kasumba ya kuwa dharau wale join 2020 kuendelea

Zamani ubabe ni kila sehemu, nashangaa watoto wa siku hizi wanapendana. Huenda zamani ubabe ulikuwa kama sehemu ya kupoteza muda na bururani, siku hizi watu wameangalia mpira wanasimuliana, wote wanafuatikia muziki, movies n.k. hawana muda ya kutunishiana misuli.
 

Mkuu, kulikuwa na mashambulizi toka pande zote na dharau pia zilikuwepo. Hii fact kwamba diaspora ndio walikuwa wengi toka enzi za JamboForums siipingi. Ni ya kweli, lakini disrespect ilikuwepo kati ya pande hizo.

Hoja ya juzi kuzimwa Internet itoe mkuu, haina relevance na tunachoongelea. 😊
 

Sasa siku hizi shule imeshakuwa rahisi, watoto wanaanza shule mapema. Elimu imeboreshwa mkuu.
 
Ile miaka tulipata tabu sana member wapya , wadogo na ambao sio maarufu . Nakumbuka Kuna uzi mmoja jamaa alikuwa attacked kisa umri wake wewe ukaja kuDefend kwa hoja zenye akili kumtetea yule attacked , siku hiyo nilifarijika sana na ujasiri wako , iliniongezea kujiamini na kunipa moyo wa kushiriki kwenye mijadala Jf japkuwa nilikuwa mdogo , enzi hizo umri wangu nilikuwa naficha sana sio kama sasa najiachia .

Siku hiyo ndio ilikuwa mwanzo wa kuikariri ID yako na nikakuona smart sana na ni mtetezi wa madogo wa Jf tunaodharauriwa .

Hawa joined 2020 wa sasa washukuru kuikuta Jf hivi wanapata reply na likes , zamani new members kupata reaction ilikuwa ngumu sana watu wanachat wenyewe kwa wenyewe wakongwe tupu , unakuta Uzi wako umeanzisha kinakuja kikundi kubebishana na kupiga soga , mtu una MQuote vitu vya maana anapuuza kukujibu kisa mgeni anawajibu wengine dah !
 
Mbona malijendi tupo na hatuna hizo pigo mzee.
 
Sembuse mke ana achwa ndio I'd? Nani asiye kujua siku unajiunga humu bwashee? Nani asiye jua chanzo cha utani wenu na mghayo ?tukisema madgo acheni ujuaji tunawajua bwashee 🤣
Kumbe ulikuwa active humu kipindi najiunga !

Usikute nyinyi ndio wale mliokuwa mnadharau new members, madogo na watu ambao sio famous kipindi kile mpaka kukuanzishwa makapuku forum humu .

Enzi hizo Beira Boy alikuwa na nyuzi za kitoto za kuwala walimu shuleni sasa hivi Saint
 

Tujadili hoja, tusijikite sana kumjadili mtoa hoja.

Kujadili mtoa hoja sana badala ya hoja ndiyo mwanzo wa kufanya ad hominem logical fallacy.

Hoja ni hoja tu, bila kujali umri wa mtu, au kajiunga lini.

Pia, watu wapya/wadogo nao wana nafasi kubwa ya kuonesha mambo ambayo wakongwe tunayofanya vibaya kwa mazoea tu. Kutufundisha.

Hili somo kubwa sana nilifundishwa na Robert Rubin, former US Secretary of The Treasury, mtu aliyewahi kuwa na saini yake kwenye US dollar, nilipokuwa naanza kazi Wall St. miaka mingi nyuma.

Nilijifunza kitu kikubwa sana yule mkongwe hakuwekea mkazo kusisitiza mafunzo ya kutupa kutoka miaka yake alipokuwa Waziri wa Fedha wa Marekani. Yeye alisisitiza sisi vijana tuliokuwa tunatoka vyuoni, tutoe uzoefu wa dunia mpya, tukosoe wakongwe waliokuwa wanafanya kazi kwa mazoea kwa miaka mingi, bila woga. Kwenye dunia ya teknolonia inayobadilika kwa kasi sana mawazo mapya ni muhinu sana.

Baada ya kusema hayo, kuna changamoto upande wa pili pia.

Kiujumla zamani kuwa na mtandao ilikuwa kitu adimu. Ilibidi uwe mtu fulani kuwa na mtandao. Umesoma, umesafiri, una exposure fulani.

Kwa hiyo tulikuwa tunakutana watu wenye upevu fulani wa mawazo, mazungumzo yalikuwa ya kuelewana zaidi.

Siku hizi, teknolojia imekuwa rahisi, kila mtu ana mtandao, of course utakutana na watu wengi wa kajamba nani ambao hawaelewi mambo mengi, hawajui mantiki, hawana ustaarabu, hawajui tofauti ya hoja na kiroja,

Of course kujadiliana nao hao ni kazi sana.
 
Nimeokoka kaka kwa sasa nguvu zangu nimewekeza kutafuta pesa kwanza, naona mambo si mbaya kwa sasa pesa inaingia
 
Nzunya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…