2) Kwa kawaida msichana wa miaka 9 ni mdogo sana - kwa maana hiyo bila shaka alikuwa akishiriki nae tendo?
Majibu tafadhali [emoji1431]
Swali la pili lina sehemu kuu mbili, sehemu ya kwanza inaungana na swali la 3 na sehemu ya pili inaungana na swali la kwanza
Sehemu ya kwanza: Kwa kawaida msichana wa miaka 9 ‘AISHA’ ni mdogo sana.
Swali hili linajibiwa na Imaam At-Tirmidhiy alipoinukuu kauli ya A’ISHA aliposema “Mtoto wa kike akifika umri wa miaka 9 ni mwanamke”. Inafahamika kwamba katika historia ya mwanadamu alama kuu ya kuingia katika utu uzima “ukubwa” ni balehe “buligh” “kupevuka”. Na hili limekuwa likifanyiwa kazi katika zama zote na katika jamii zote isipokuwa katika karne hii ambapo wanaharakati wa haki za watoto wamelivalia njuga kwa kuzitaka mamlaka ziweke sheria za ukomo wa umri katika masuala ya ndoa na mahusiano.
Miaka ya nyuma katika jamii ya wayahudi “JEWS”; walikuwa wanaonelea ni vema kwa mwanamke kuingiliwa baada tu ya kupata hedhi yake ya kwanza, na baadhi yao walikuwa na utamaduni wa kuwaingilia wanawake hata ambao hawajapevuka “hawajapata hedhi”.
Kwa miaka ya nyuma kwa jamii ya wamongolia “MONGOLS” kuoa au kuolewa katika umri mdogo ilikuwa ni jambo la kawaida, mfano: GHENGHIS KHAN alioa akiwa na umri wa miaka 9, vilevile aliyemuoa alikuwa na umri mdogo; miaka 12.
Ama kwa tamaduni za waarabu; kuoa/kuolewa katika umri mdogo lilikuwa ni jambo la kawaida sana, mfano: AMR IBN AL AS alioa katika umri mdogo kiasi cha kuwa na tofauti ya miaka 10 - 13 na mwanaye ABDULLAH IBN AMR, halikadhalika AISHA kabla hajaolewa na MTUME alikuwa tayari ameshachumbiwa na JUBAIR IBN MUT’IIM ambaye kwa wakati huo hakuwa ameingia kwenye uislamu. Hivyo ilikuwa ni mambo ya kawaida kwao.
Inafahamika wazi kwamba kuwahi au kuchelewa kupevuka kunatofautina kutokana na zama, vinasaba, jiografia/mazingira, hali ya hewa “joto au baridi”, jamii na sababu nyinginezo. Kwa zama zetu imezoeleka watoto wa kike hupevuka wakiwa na umri kati ya miaka 8 – 12.
Sheri’ah ya kiislamu inazingatia “balehe” kama kigezo kikuu na kama ishara ya mtu kuingia katika ukubwa (manageable/adolescent age) na ndoa. Na katika kuliendea tendo la ndoa mambo mengine muhimu yatazingatiwa kama “ukubwa wa kimaumbile”, “kujitambua”, “uwezo” nakadhalika.
Wanahistoria wanaeleza kwamba kama katika karne ya 7 ndoa ya MTUME kwa A’SHA ingekuwa ni jambo la kushangaza kwa jamii yake basi kungepatikana/kungekuwepo hata nukuu moja hasi yenye kunyooshea kidole hilo. Kukosekana kwa pingo “objection” la ndoa yake kutoka kwa maadui/ndugu/jamaa/marafiki zake kunatoa picha kwamba lilikuwa ni jambo la kawaida na haifai kulihukumu/kulikosoa kwa kufananisha na utamaduni wa kileo wa magharibi.
Swali: Hivi binti wa miaka 10 aliyeishi miaka 2000 iliyopita ni sawa na binti wa kileo wa miaka 10?
Tafiti: Jaribu kutafiti kwa kina kuhusu umri wa MARIAM alipokuwa na ujauzito wa YESU, na umri wa MARIAM alipoolewa na YUSUPH
Tofauti na hawa tuliowataja, je historia haijaeleza watu wengine mashuhuri waliooa mabinti katika umri mdogo?
Sehemu ya pili: Je, AISHA alipokuwa na miaka 9 alikuwa akishiriki naye tendo 'jimai'?
Hili limeelezwa na AISHA mwenyewe kwa uwazi kwenye baadhi ya hadithi tulizotaja kwenye swali la kwanza na nyinginezo
1. Sahih Al Bukhari, Kitab Al-Nikaah – Ndoa, Hadithi Namba 69, Daraja la Hadithi: Authentic “Sahih”
2. Sahih Al Bukhari, Kitab Al-Nikaah – Ndoa, Hadithi Namba 70, Daraja la Hadithi: Authentic “Sahih”
Pia hadithi zifuatazo ambazo hatukuzitaja
“zinajibu swali hili na la kwanza”
1. Sunan Abu Dawood, Kitab Al-Nikaah – Ndoa, Hadithi Namba 76, Daraja la Hadithi: Authentic “Sahih”
2. Sunan An Nasai, Kitab Al-Nikaah – Ndoa, Hadithi Namba 60, Daraja la Hadithi: Authentic “Sahih”
3. Sunan Ibn Majah, Kitab Al-Nikaah – Ndoa, Hadithi Namba 33, Daraja la Hadithi: Authentic “Sahih”
4. Sahih Al Bukhari, Kitab Al-Nikaah – Ndoa, Hadithi Namba 93, Daraja la Hadithi: Authentic “Sahih”
5. Sunan An Nasai, Kitab Al-Nikaah – Ndoa, Hadithi Namba 61, Daraja la Hadithi: Authentic “Sahih”
6. Sahih Al Bukhari, Kitab Al-Nikaah – Ndoa, Hadithi Namba 121, Daraja la Hadithi: Authentic “Sahih”