HURUMA: Mdude Nyagali awatoa machozi wajumbe wa Kongamano la Katiba Mpya

Katiba ya nchi haijaruhusu MATUSI NA DHARAU kwa Rais wa nchi.....

Nipe kipengele kinachoruhusu hayo.....

Hivi kuidai haki yako ndio kuwadhihaki na kuwatusi wengine?!!! Tena Rais wa nchi?!!!!
Alipaswa kushitakiwa kwa matusi na si kesi ya uongo ya madawa ya kulevya
 
Naona makamanda wamepata upenyo sasa...paka ametoka vipanya vinaanza kusumbua huku na kule....

Mdude mumpime akili anaweza akawa sio mzima...kama ni mzima basi mpelekeni shule angalau ajifunze ustaarabu na kujua walau basics ya nini maana ya siasa, serikali na dola ni nini, Rais wa nchi ni nani pia.m
Kwani Mdude kusema wembe ni uleule kaanza yeye kusema, au umeusahau wimbo ule wa TOT ya CCM unaosema: WAPINZANI WEMBE NI ULE ULEE.
 
Katiba ya nchi haijaruhusu MATUSI NA DHARAU kwa Rais wa nchi.....

Nipe kipengele kinachoruhusu hayo.....

Hivi kuidai haki yako ndio kuwadhihaki na kuwatusi wengine?!!! Tena Rais wa nchi?!!!!
Mkuu hebu tuoredheshee matusi na dharau alizomfanyia rais wa nchi?
 
Mfungwa wa Kisiasa aliyeishinda Serikali ya Tanzania Mahakamani , baada ya kupangua mashitaka ya uongo yaliyotungwa na RPC wa Mbeya Ulrich Matei na washirika wake ya kusafirisha na kusambaza Madawa ya kulevya , leo amehudhuria Kongamano muhimu la Katiba (Katiba day) ambapo wameonekana watu mbalimbali wengi wakiwa ni akina mama Wakitokwa na Machozi , ikiwa ni ishara ya kumhurumia .

Mdude au Martin Luther kama anavyoitwa na vijana wa kileo , ambaye amepewa nafasi ya kusalimia Wajumbe hao aliwekwa selo kwa siku 414 kwa kesi ya uongo ili kumkomesha kutokana na itikadi yake ya kisiasa .

View attachment 1837101
View attachment 1837115
View attachment 1837117
View attachment 1837118
Haya Kongamano limefanyika kwa mafanikio makubwa sana bila vurugu wala makwazo Serikali imepoteza nini? Mambo mengine serikali huwa inapenda kujitia stress.
 
Ngoja tuone mama naye akizingua kama ataanza kuporomosha matusi. Mdude ni mwanaharakati mzuri lakini sijui alikuwa anapata faida gani kuporomosha matusi non stop. Kwa matusi yale hata sasa akianza kumtukana mama laivu namna hiyo watamkamata tena.
Nipe mfano wa matusi matatu tu kati ya hayo unayotaka kudanganya umma.
 
Sasa hivi hao jamaa mataga huwa wanaongea tu
Mdude kama angekamatwa kwa kosa la kutukana hapo tungesema amestahili lakini unamtumia watu wamteke na kumtesa kisha unambambikia kesi ya uongo ni ujinga wa hali ya juu wa Dikteta yule
Na hili ndio kosa la serikali ya Dikiteta uchwara na wafuasi wake. Pengine wangemstaki kwa kosa la kumdhalilisha Rais huenda wangemtia hatiani. Alivyokuwa hawana akili na roho mbaya wakataka kumsingizia kosa kubwa zaidi. Mwisho wa siku wameambulia aibu
 
Mfungwa wa Kisiasa aliyeishinda Serikali ya Tanzania Mahakamani , baada ya kupangua mashitaka ya uongo yaliyotungwa na RPC wa Mbeya Ulrich Matei na washirika wake ya kusafirisha na kusambaza Madawa ya kulevya , leo amehudhuria Kongamano muhimu la Katiba (Katiba day) ambapo wameonekana watu mbalimbali wengi wakiwa ni akina mama Wakitokwa na Machozi , ikiwa ni ishara ya kumhurumia .

Mdude au Martin Luther kama anavyoitwa na vijana wa kileo , ambaye amepewa nafasi ya kusalimia Wajumbe hao aliwekwa selo kwa siku 414 kwa kesi ya uongo ili kumkomesha kutokana na itikadi yake ya kisiasa .

View attachment 1837101
View attachment 1837115
View attachment 1837117
View attachment 1837118
Hili kongamano lilikuwa Pambe. Kumbe inawezekana aisee
 
Mdude kapata huruma wa huu utawala, asijisahau hawezi kutukana viongozi wa nchi kwa namna yake, akitaka kujaribu moto amtukane mbowe,...keep the respect in place Raisi is not your father hata kama kakuuzaa, Raisi ndio alama ya Taifa ya kwanza huwezi kuchafua tuu eti demokrasia, ajaribu kumchafua mwenyekiti wake..
 
Stress zitawaua.
 
Ngoja tuone mama naye akizingua kama ataanza kuporomosha matusi. Mdude ni mwanaharakati mzuri lakini sijui alikuwa anapata faida gani kuporomosha matusi non stop. Kwa matusi yale hata sasa akianza kumtukana mama laivu namna hiyo watamkamata tena.
Mkuu niamin hatorudia tena kuwa mpumbavu saivi amebaki na ujinga unaoelimishika.
 
Back
Top Bottom