HURUMA: Mdude Nyagali awatoa machozi wajumbe wa Kongamano la Katiba Mpya

HURUMA: Mdude Nyagali awatoa machozi wajumbe wa Kongamano la Katiba Mpya

Mdude akiweza kuacha matusi na lugha za kuudhi kwa viongozi wakuu wa serikali anaweza kuja kuwa mwanasiasa mzuri
Viongozi wakuu wa serikali msioweza kuvumilia lugha za maudhi achieni ngazi mkafanye shughuli zenu binafsi, mtaani kuna kundi kubwa la vijana kwa wazee walio tayari kuwa viongozi wakuu wa serikali na wakavumilia lugha za maudhi.
 
CHADEMA
ni imani
ni fikra
ni falsafa
Kwa mbinyo ule awamu ngumi ( 👊,5) ,bado wamo.
Kama wamegoma kuchukua ruzuku,shughuli hizo nani anagharimikia.
 
Kwakweli Mdude alitekwa mara kadhaa kabla ya kubambikiwa kesi ya kutoa Madawa ya kulevya Afghanistan na kuja kuyasambaza Mkoa wa Mbeya

Kama Nchi Huru tulifika pabaya sana Mungu katuletea Raisi Samia tunamuona kama Lulu ing'arayo.
Weka akiba ya maneno
 
CHADEMA
ni imani
ni fikra
ni falsafa
Kwa mbinyo ule awamu ngumi ( 👊,5) ,bado wamo.
Kama wamegoma kuchukua ruzuku,shughuli hizo nani anagharimikia.
Nguvu ya umma,kwa umoja wao kwa imani yao na kwa falsafa yao ya kizalendo tena uliokuwa halisi, Bila maslahi binafsi ndani yake.
 
Katiba Mpya ni muhimu sana, uwepo wa Mdude kwenye hilo kongamano ndio kunachagiza zaidi upatikanaji wa Katiba Mpya.

Hatuwezi kama taifa kuendelea kuishi kwa kutegemea hisani za viongozi wa CCM, akiwepo mbaya aonee raia, akiwepo mwenye huruma ndio raia wapate afadhali, hili lazima liondoshwe.

Tujiulize, kama leo Magufuli bado angekuwa Rais wa hii nchi, Mdude angekuwa wapi kwa jinsi mahakama zetu zilivyokuwa zimeshikwa na ikulu? ni wazi, Mdude angekuwa anatumikia kifungo wakati huu tena kwa makosa ya kubambikiwa.

Tuamke sasa, wakati ndio huu, Katiba Mpya ni lazima ipatikane ije kutuweka huru kwenye nchi yetu, irudishe usawa wa raia kwenye taifa letu bila kujali itikadi, rangi, wala dini zetu, na rasilimali za nchi yetu zitunufaishe sote sio kikundi kidogo cha watu pekee wanaolindana.

Wale wote wanaopinga upatikanaji wa Katiba Mpya ni wanyonyaji wanaoishi kwa kunywa damu za watanzania wenzao (zombies), akili zao bado zimelala, tusichoke tuendelee kuwaamsha wala tusiogope eti tutalala sisi, wataamka tu, kwa sababu Katiba Mpya itakuwa kwa manufaa yao pia.

Watu kama mdude wangeachiwa kwa kuandika tu yale mavitu yao ambayo hayana msingi basi kuna siku tungekuta hata ww na mke wako mmeanikwa tu mitandaoni

Hatakama kuna uhuru wa Habari ila sio kwa kumwandika rais vile
 
Wengi humu ndani wanaongelea matusi ya Mdude wakati alishtakiwa kwa madawa ya kulevya, ambapo imeonekana ni ya kubambika. Ilishindikana vipi kumfungulia kesi ya matusi kama ushahidi ulikuwepo?
 
Wengi humu ndani wanaongelea matusi ya Mdude wakati alishtakiwa kwa madawa ya kulevya, ambapo imeonekana ni ya kubambika. Ilishindikana vipi kumfungulia kesi ya matusi kama ushahidi ulikuwepo?
Hawana ushahidi ni uonevu tu
 
Hata waswahili walitunga methali kuwa Asiye sikia la mkuu,uvunjika mguu.Unawezakuwa mwanasiasa bora basipo matusi,akina Slaa,Mbowe, Zito,wamekuwa wanasiasa mashuhuri nchi pasipo kutukanana,na watu tuliwaelewa,Siasa ni hoja sio matusi,kumbuka huyo unayendhalilisha kwa matusi ni mkuu wa nchi,pia anafamilia,
Hakuna Mtu anayekataa lakini si angefunguliwa mashtaka ya kumdhalilisha Raisi sasa jiwe amemteka mara mbili na kumbambikia kesi ya Madawa.
 
Hakuna Mtu anayekataa lakini si angefunguliwa mashtaka ya kumdhalilisha Raisi sasa jiwe amemteka mara mbili na kumbambikia kesi ya Madawa.
Hiyo ndio dawa ya njinga kama yule, maana alikuwa anajificha kwenye chaka,hata wangelimpeleka mahakamani wasingempata,hiyo ndio ilikuwa dawa yake.Hata . hivo amejifunza kitu,sidhani kama atarudia tena.
 
Kwahiyo kwanini usishauri muswaada usipelekwe Bungeni ili tuwe na Sheria ya kuteka wapinzani wa mitandaoni na wanaomdhalilisha Raisi ili iwe Dawa komesha ya Chadema?
 
Back
Top Bottom