Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Kama serikali inaweza kununua mahindi kwa bei ya juu ili kunusuru walaji, kwa nini isitumie pesa hizo hizo kuwapa ruzuku wakulima ili walime kwa bei nafuu na kuuza kwa bei nafuu?
Wakulima wanalima kwa ukiwa na shida tele , wanakuja kuonekana na serikali wanapouza mazao yao tu.
 

Chakula sio mahindi na mchele peke yake kuna mihogo na viazi pia
 
Hamna jomba mbona sukari ipo bei juu lakini hamuililii ishuke mmeshupalia wakulima wa mpunga na mahindi tu mnawaombea bei ziporomoke
 

Jomba walaji hatutaki mpange bei tunachotaka bei ya soko ndio iamue
 
Simtamsahau huyo mzee na udikteta wake alinitia hasara mbaya kidogo niugue presha,,,nilinunua mahindi nikaweka stoo Mara paap nikaskia linaropoka hakuna kuuza mahindi nje hata kusafirisha nje ya wilaya hakuna aisee nilipata hasara mbaya gunia nikawa nauza 36,000 wakat nilinunua 60,000 kumpata mteja nayo ikawa shughuli,,,yule mtu mungu amuweke mahali anapostahili
 
Kwa longe term, kuruhusu mahindi kutoka ni dawa

Kuyazuia ni kufubaza ukuaji wa sekta
 
Usiwapangie wakulima wapi wauze mazao yao, ardhi kanunua mwenyewe, mbolea kanunua mwenyewe, kaotesha na kupalilia mwenyewe, kavuna mwenyewe halafu baada ya kuvuna unataka umpangie wapi pa kuuza, hii sio akili.
Majibu kama haya niliyategemea
 
Kumudu bei za sokoni kwani hao wasiomudu wamezuiwa na nani kulima mazao yao?
Kwenye population ya 60 million Tanzanians. 30% sio wakulima na wanaishi mijini.

Hayo mazao ya shambani mengi yanauzwa magengeni hakuna cha VAT huko serikali aipati makusanyo ya hivyo.

Ilhali mpaka sasa huyo kichaa Bashe ameshapewa zaidi ya trillion moja kufanya upuuzi wake huko kwenye kilimo. Hiyo 30% ni sawa na 18 million people wakubwa na vichanga kwa wastani kila mtu kachangia tsh 55 elfu, hao wakulima waweze pata mbolea za ruzuku, Bashe afanye experiment za kipumbavu za kilimo.

Bado ujaweka mchango wa watu mijini kwenye kujenga hizo barabara zinazoenda mpaka kijijini na kuwafungulia masoko hao wakulima, mchango wao kufikishiwa umeme vijijini na mambo luluki.

Wanastahili zote kuangaliwa kwenye bei himilivu ya chakula; hizo hela zinazoenda huko azitoki mfukoni kwa baba yake Bashe ni kodi za watu wa mjini; bila ya wao hakuna mkulima wala watu wakwenda kununua hayo mazao.

Mkulima hana mchango wowote kwenye kodi ni kupe anaetegemea hela za walipa kodi mjini ili aishi; halafu mnasema watu wa majini hawana mchango kwa mkulima. Hizo sijui akili za wapi.
 
Nenda kalime na wewe ili uje uwauzie wanaoshinda kwenye betting wakisubiri bashe afunge mipaka
Muwe waelewa pia pale Serikali itakapofungua mipaka yake kuruhusu chakula kutoka nje, kuuzwa nchini. Maana na sisi ambao siyo wakulima, tunachoka kununua chakula kwa bei isiyo na uhalisia.
 
Aliyetoa jasho kuzalisha mahindi asipangiwe pa kuuza - ni jasho lake. Sawa na jasho la mfanyakazi, yaani mshahara, hapangiwi jinsi ya kuutumia.

Mambo ya food security katika taifa ni issue ya serikali. Iyanunue mazao kwa bei shindani na kuyahifadhi. Sio kumzuia mkulima kuuza atakapo.
 
Kumudu bei za sokoni kwani hao wasiomudu wamezuiwa na nani kulima mazao yao?
Siyo lazima kila mtu alime! Mfanyakazi analipwa mshahara, ambao atatumia sehemu ya huo mshahara kununulia chakula kutoka kwa mkulima.

Na mkulima akipata hiyo pesa, atanunulia mahitaji yake ya msingi. Maisha siku zote hutegemeana. Hatuwezi wote kuwa wakulima.

Na mfahamu fika hii biashara ya mazao mnayofanya na Wakenya hao na Wasomali, siyo endelevu! Siku wakiamua kununua hayo mazao yenu sehemu nyingine; mtalia na kusaga meno.

Lakini pia tusiwaone mkilalamika pale serikali itakapo ruhusu chakula kutoka nje, kuingizwa nchini ma kuuzwa kwa bei nafuu. Nyinyi wauzieni Wakenya na Wasomali hico chakula chenu kwa bei nafuu!! Na wakati huo huo Serikali iruhusu wafanyabiashara kuingiza chakula kutoka nje ili kupunguza mfumuko wa bei ya chakula.

Nadhani hamtalalamika. Maana kila mtu atakuwa ameshinda mechi zake.
 

Kwa nini sasa iwe lazima mkulima apangiwe wa kumuuzia mazao yake?
 
Muwe waelewa pia pale Serikali itakapofungua mipaka yake kuruhusu chakula kutoka nje, kuuzwa nchini. Maana na sisi ambao siyo wakulima, tunachoka kununua chakula kwa bei isiyo na uhalisia.

Kalime upate ya kwako ya bei ya uhalisia halafu uuze kwa bei ya uhalisia kama na wewe hutauza kama wakulima leo hii unavyolalamika wanauza
 
Lima wewe ubakize ndani ...unafikiri wakulima ni manamba wa kujaza tumbo lako ukajaze choo!?
 
Kalime upate ya kwako ya bei ya uhalisia halafu uuze kwa bei ya uhalisia kama na wewe hutauza kama wakulima leo hii unavyolalamika wanauza
Ushauri wangu kwenu ni huu hapa; kama serikali inaruhusu wakulima/wafanyabiadhara kuuza chakula nje ya nchi kwa bei nzuri, basi iruhusu pia wafanyabiashara wengine kuingiza chakula nchini na kukiuza kwa bei nafuu.

Au unaonaje. Maana hakuna sababu ya haya malalamiko! Lakini pia kulazimisha Watanzania wote kuwa wakulima.
 
Kalime uuze Bei nafuu ...hamkawii kuwadharau wakulima,huu ni wakati wa mkulima kuheshimiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…