Huu mdahalo lengo ni nini? Mdahalo unaitwa “Jesus and Mohammed”

Hapana bwana acheni uchonganishi

KAMA KITU HUKIJUI NYAMAZA
ULE SIYO MDAHALO BALI NI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KIISLAMU AMBALO LITAJIKITA KATIKA MANENO YA AMANI. DR ZAKIR NAIK NA MWANAE WATAKUJA TANZANIA KUZUNGUMZA NA WAISLAMU LAKINI PIA WANAKARIBISHWA WAUMINI WA DINI ZOTE

KITU ULICHOONA WEWE NI MANENO YA KWENYE BANGO AMBAYO HATA NAYO HUJAYAMALIZA YOTE. KUMEANDIKWA "JESUS AND MUHAMMAD THE BROTHERS IN FAITH" IKIMAANISHA WAISLAMU NA WAKRISTO NI NDUGU KATIKA IMANI NA NDIYO MAANA KONGAMANO LIKAWAKARIBISHA WOTE (ASILIMIA KUBWA TANZANIA NI WAISLAMU NA WAKRISTO).

HIYO KAULI SIYO KWAMBA INATUNGWA TU BALI NDANI YA UISLAMU (YAANI QURAN) TUNAAMBIWA TUWAITE WAKRISTO NA WAYAHUDI TUZUNGUMZE KWA PAMOJA JAMBO AMBALO TUNAFANANA AMBALO NI LA KUMWABUDU MOLA MMOJA TU KWA HAKI

HAYA TUAMBIE HIYO YA MDAHALO UMEITOA WAPI?
 
Katika uislamu tofauti yetu ni ndogo sana,kiasi kwamba haiwezi kuleta athari yoyote na mtu wa nje hawezi kuiona abadani, muislamu anaweza kuswalia msikiti wowote ule bila tatizo,lkn kwenu si hivyo.
 
Nakubaliana na wewe 100% katika haya.
 
Kwa hiyo unakubaliana na Yesu kuwa Mungu anaitwa Baba? Ndivyo Uislamu unasema hivyo kwamba Mungu ni Baba?
 
Kasikilize kwanza pengine hizo propaganda za akina Gwaji zitaondoka
 
Tunapaswa kuwa watu wema na wenye roho nzuri, upendo, kusaidia wenye shida mbalimbali pasipo kujali kama unaenda katika nyumba za ibada ama la..
 
Katika uislamu tofauti yetu ni ndogo sana,kiasi kwamba haiwezi kuleta athari yoyote na mtu wa nje hawezi kuiona abadani, muislamu anaweza kuswalia msikiti wowote ule bila tatizo,lkn kwenu si hivyo.
Wacha uongo wewe. Nani anakataa kusali kanisa lolote? Je kwanini mnauana wenyewe kwa wenyewe? Usitifanye sisi wote matutusa we dogo.

Madhehebu mengi ya Kiksrito wana msingi mmoja tu ambao ni Kristo. Utofauti wao ni kwenye mapokeo ya kibinadamu tofauti na nyie huko.
 
Tusubiri kwanza hata siku ya kwanza ya mdahalo tuone. Sidhani kama Azam ni wajinga kiasi hicho mpaka waruhusu promo ya mdahalo kama ile ya miaka ile mitaani.

Inawezekana hawa wahubiri wana mrengo tofauti na wana mpango wa kuunganisha hizi dini mbili ili tuishi kwa umoja na mshikamano. Kuna muda Papa alikutana na viongozi wa Waislamu. New World Order!
 
Sawa tutaona
 
Katika uislamu tofauti yetu ni ndogo sana,kiasi kwamba haiwezi kuleta athari yoyote na mtu wa nje hawezi kuiona abadani, muislamu anaweza kuswalia msikiti wowote ule bila tatizo,lkn kwenu si hivyo.
Kwahiyo una uhakika kuwa Mkristo haingii Kanisa lolote lile la dhehebu lolote lile?
Jambo usilo lijua asiwe unaliongea.
 
Sasa kivipi Yesu awe muislamu wakati Quran inasema Allah sio baba wa yeyote. Au kiarabu ni dhambi kumuita Allah baba lakini lugha zingine ruksa?

Kwani Islam maana yake ni nini kwa unavyofahamu wewe ????

Kwani wapi yesu alisema kuwa yeye ni mwana wa mungu ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…