Ngoja kidogo turudi kwenye historia. Miaka ya 80 katikati swali Sunna au waislamu wenye msimamo mkali ndio walianza anza Tanzania, harakati za upinzani wa Bakwata ulianza taratibu miaka hiyo, msikiti wa kwa Mtoro ukiongozwa na sheikh Kassim pamoja na mnajim sheikh Yahaya ndio walikua wakiongoza harakati, baadae walikuja kuanzisha chombo chao kingine wakikiita BARUKTA ambacho kwa mtazamo wangu, kilifanya vizuri sana kuwaunganisha waislamu; walianza kuharibu walipoanza kuingia kwenye siasa; anyway hilo sio lengo la mchango wangu; mchango wangu uko hapa; walianzisha kikundi cha vijana kinacho sema "Yesu sio mwana wa Mungu" kiongozi mmoja wapo alikua kijana mmoja wa Kitanga anaitwa Rashidi Idd Athuman Njeja, huyu jamaa ndiye alieongoza ule uvunjaji wa mabucha ya nguruwe miaka ya 90 mwanzoni, tuendelee mbele sasa. Kikundi hiki kilitembea maeneo mengi nchini, kilipata upinzani sana kwa Wakristo, serikali haikuwahi kuona madhara ya mahubiri yale, sijui kwasababu rais wa wakati huo alikua Muislam au ndio demokrasia yenyewe, that much sina hakika. Mwanzoni mwa miaka ya 90, kama sikosei was the year 1992 walifanikiwa kumsilimisha kijana mmoja wa Kinyakyusa akawa anajiita askofu Mwaipopo, dogo alikua anasoma Sekondari ya Lutheran kule Tukuyu, alikwama ADA nadhani, hawa kina Rashidi na taasisi zao walimpa msaada na hatimae akawa muislamu. Hadi hapo mimi sikuona tatizo; waliendelea na kashfa zap kwa Ukristo na Wakristo hadi katikati ya miaka ya 90 palipokuja kikundi kingine kinaitwa YESU ni JIBU, hiki kikundi (hapa ndio msingi wa hoja yangu ) kilianza kujibu kashfa zote za kile kikundi cha kina Mazinge (Rashid hakuwepo tena, nasikia alikua kaokoka na kua mlokole ) but kikundi hiki kilianza kufunua siri za Uislamu na Waislamu, kikaanza kueleza hadi maisha ya mtume Mohammed, kikundi hiki ndio kwa mara ya kwanza kulikuja kuonesha Tanzania kwamba Mohammed aliwahi kuoa mtoto wa miaka 9, wao walitamka kwamba kitendo kile walikitafsiri kwamba Mohammed alikua mbakaji. Yapo mengi, sitakwenda ndani sana. Ikumbukwe sheikh Kassim alikua ameisha kufa, baadhi ya vijana wake kama Rashid waliisha kua Walokole na wamehama Dar, vuguvugu hili lilihamia msikiti wa Mtambani Kinondoni, wakaanza pia vurugu kwa baadhi ya misikiti, nakumbuka walikwenda pale msikiti wa KIBO Dar, wakati huo askofu Gwajima ndio katoka chuo kanunua ule ukumbi maarufu wa disco unaitwa Hunters club na akaligeuza kua kanisa, msikiti wa Kibo na kanisa la Gwajima hapakua mbali sana; Gwajima alianza na vijana machachari of course nae alikua umri huo huo tu. Kikundi hiki nakumbuka kilisababisha vurugu msikitini pale na kikasababisha aliyekua sheikh wa pale Sheikh Kipindula kuondolewa, akaacha kusali pale; now Biblia ni jibu nao wakalitenga viwanja wa Msewe, wakimimina hoja zao, shida ikaanza nchini, vurugu zikaanza; hatimae mauaji ya mwembe chai yakatokea. Vikundi hivi vilipatanishwa sana na aliyekua waziri wa mambo ya ndani those times but it didn't help; yaliotokea ni historia. Mashaka yangu yapo hapa, Wakristo wakiamua kuja kuthibitisha kwamba Mohammed hakua mtume wa Mungu, Waislamu wanaweza kudhibiti hasira zao? Kama hawataweza, hakutakua na VURUGU hapo? Tusubiri.