Huu mfumo wa utawala tuuchukue ndio uwe mfumo rasmi wa uongozi na utawala

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !.

Naomba niweke mawazo yangu hapa jukwaani.

Ikiwapendeza nawaomba mtumie huu mfumo ili mfanikiwe maendeleo;

1. Madiwani ndio waiongoze halmashauri;
(a) Mwenyekiti na Msaidizi wake wa Halmashauri wawe raia wa kawaida wasomi ngazi ya Shahada moja na kuendelea asitokane na udiwani.
(b) Hii itachochea maendeleo haraka vibaya mno. Pia itaondoa kuzorota kwa maendeleo mengi ndani ya halmashauri.

2. Spika wa bunge na naibu wake wasiwe wabunge kabisa yaani asitokane na kuchaguliwa na Rais au kuchaguliwa kuwa muwakilishi wa jimbo lolote Tanzania;.
(a) Spika na Naibu wawe wataalamu wa masuala ya Uongozi, Utawala, Uchumi na Maendeleo katika Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Hawa wataalamu wawe rasmi kutoka Vyuo vikuu hivi vifuatavyo (University of Dar es Salaam, Sokoine University na Muhimbili University pekee).
(b) Elimu zao kuanzia shahada ya kwanza katika fani za Maendeleo, Utawala na Uchumi.

3. Rais wa nchi asitokane na chama chochote cha kisiasa. Bali awe ni mgombea ambaye atafanyiwa usaili na vyuo vikuu vitatu (University of Dar es Salaam, Sokoine University na Muhimbili University) na akipitia vyama vya siasa vitachagua mtu wa kumnadi kama mtu wa mlengo wao na kupeleka ushawishi kwa wananchi nje na hapo tuachane na mfumo wa kizamani.

N.B
Karibu
Asante.
 
Hizo nafasi spika wa bunge na naibu wake watazipata vipi? Kama hawachaguliwi na rais wala wananchi?
Wanaomba kugombea na watasailiwa na hivyo vyuo vikuu vitatu. Maana hivyo vyuo ndio uti wa mgongo wa elimu na ukuaji wa maendeleo yetu. Lazima apitie tanuru la moto hapo. Sifa asiwe mwanachama wa chama chochote na asiwe na mahusiano ya moja kwa moja na vyama vya siasa kabisa.
 
Kwa ccm hii inayowaanda wanawe na wanawe nao waje kuingiza huo mfumo sijui utaitoa wapi?. Bahati mbaya hakuna mfumo wowote mzuri wa kuichomoa,uwe wa kura,maridhiano zaidi ya kuichomoa kwa nguvu ya umma
 
(a) Spika na Naibu wawe wataalamu wa masuala ya Uongozi, Utawala, Uchumi na Maendeleo katika Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Hawa wataalamu wawe rasmi kutoka Vyuo vikuu hivi vifuatavyo (University of Dar es Salaam, Sokoine University na Muhimbili University pekee).
Mimi alumni wa UDSM Ila huu upendeleo napinga.
Vipi kuhusu vyuo vingine vya ndani na wale waliosoma vyuo bora kabisa nje ya nchi?
Huoni unaweza kuacha watu wenye sifa nzuri?
 
Mimi alumni wa UDSM Ila huu upendeleo napinga.
Vipi kuhusu vyuo vingine vya ndani na wale waliosoma vyuo bra kabisa nje ya nchi?
Huoni unaweza kuacha watu wenye sifa nzuri?
Hapa sina maana ya kunadi vyuo. Bali nazungumzia uhalisia na uhakika wa kupata maendeleo kwa kasi na utayari wa nchi. Hivyo vyuo kwa macho ya mzaha ni vyuo vya kawaida ila rejea majukumu yao kwa taifa ndio utajua kwanini nimependelea kuviweka hapo.
 
Kwa ccm hii inayowaanda wanawe na wanawe nao waje kuingiza huo mfumo sijui utaitoa wapi?. Bahati mbaya hakuna mfumo wowote mzuri wa kuichomoa,uwe wa kura,maridhiano zaidi ya kuichomoa kwa nguvu ya umma
Hayo mambo yenu mbaki nayo. Eneo nalopendekeza mie ni maendeleo katika taifa letu. Hii ni kubwa zaidi kuliko kuwa wabinafsi na kunyoosheana vidole.
 
Hapa sina maana ya kunadi vyuo. Bali nazungumzia uhalisia na uhakika wa kupata maendeleo kwa kasi na utayari wa nchi. Hivyo vyuo kwa macho ya mzaha ni vyuo vya kawaida ila rejea majukumu yao kwa taifa ndio utajua kwanini nimependelea kuviweka hapo.
Kwa hivyo tuache wahitimu Yale University, MIT, Cambridge, Salford, Havard, .......
 
Hivyo ni vyuo vizuri sana huko ng'ambo; ulimwengu unajua hivyo. Isipokuwa sio vyuo bora katika taifa letu na ndio maana sijajikwaa hata kusemea kwa bahati jina lolote. Tukiamua hata sasa vyuo hivi 3 vinauwezo wa kufanya mapinduzi makubwa sana.
 
Utopo
Habari Tanzania !.

Naomba niweke mawazo yangu hapa jukwaani.

Ikiwapendeza nawaomba mtumie huu mfumo ili mfanikiwe maendeleo;

1. Madiwani ndio waiongoze halmashauri;
(a) Mwenyekiti na Msaidizi wake wa Halmashauri wawe raia wa kawaida wasomi ngazi ya Shahada moja na kuendelea asitokane na udiwani.
(b) Hii itachochea maendeleo haraka vibaya mno. Pia itaondoa kuzorota kwa maendeleo mengi ndani ya halmashauri.

2. Spika wa bunge na naibu wake wasiwe wabunge kabisa yaani asitokane na kuchaguliwa na Rais au kuchaguliwa kuwa muwakilishi wa jimbo lolote Tanzania;.
(a) Spika na Naibu wawe wataalamu wa masuala ya Uongozi, Utawala, Uchumi na Maendeleo katika Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Hawa wataalamu wawe rasmi kutoka Vyuo vikuu hivi vifuatavyo (University of Dar es Salaam, Sokoine University na Muhimbili University pekee).
(b) Elimu zao kuanzia shahada ya kwanza katika fani za Maendeleo, Utawala na Uchumi.

3. Rais wa nchi asitokane na chama chochote cha kisiasa. Bali awe ni mgombea ambaye atafanyiwa usaili na vyuo vikuu vitatu (University of Dar es Salaam, Sokoine University na Muhimbili University) na akipitia vyama vya siasa vitachagua mtu wa kumnadi kama mtu wa mlengo wao na kupeleka ushawishi kwa wananchi nje na hapo tuachane na mfumo wa kizamani.

N.B
Karibu
Asante.
Utoporo mtupu ..niliwaambia watu hapa jf ..mambo ya kuandika katiba au sheria niachiwe mimi kutoa muongozo ..hakuna mtanzania mwenye kufikia uwezo wangu hata kwa salimia 2% nasema hayupo..uliyo andika yote ni bure tu na logic yake ni potovu .

Matatizo ya nchi yetu na dunia kwa sasa kimfumo yanatokana na makosa haya..
1)kanuni mbovu za uraia
2)kudhani kuwa na elimu ndiyo kuwa na akili.
3)kosa kubwa sana la kuruhusu wanasiasa kuwa wapiga kura.
4)kusema bunge siyo serikali.
5)kupinga ujamaa au kupinga ubepari (hapa kuna kosa)
6)kuruhusu wanawake kuwa viongozi
7)kuruhusu dini au mambo ya dini kwenye serikali.
8)mfumo mbovu wa ajira serikali unao zingatia 'INTERVIEW" TU NA KUPUUZA "INVIEW"

HAYA NI BAADHI YA MAMBO AMBAYO USIPO YAELEWA NA KUYAZINGATIA KWENYE KUUNDA KATIBA AU SHERIA BASI TAIFA LITAKUWA LA KISHENZI TU KAMA TULIVYO SASA..JE WAKENYA WALIZINGATIA HAYA NILIYO ANDIKA HAPA KWENYE KATIBA YAO MPYA ? JIBU NI HAPANA hii ndiyo imesababisha Kenya kuwa na shida hadi sasa licha ya kuwa na katiba mpya hakuna cha maana sana walicho pata.

HIPO SIKU NITALETA UZI NITAELEZA KATIBA INATAKIWA IUNDWE VIPI ...WENGI MTASHANGAA NITAKAYO ELEZA NA MTAGUNDUA UWEZO WENU MDOGO WA KUTAMBUA CHANZO CHA MATATIZO YA DUNIA KWA SASA ...HATA KATIBA ZA ULAYA NI MBOVU HATA USA WANA KATIBA MBOVU INAYO ZALISHA VIONGOZI WAPUMBAVU.
 
Hivyo ni vyuo vizuri sana huko ng'ambo; ulimwengu unajua hivyo. Isipokuwa sio vyuo bora katika taifa letu na ndio maana sijajikwaa hata kusemea kwa bahati jina lolote. Tukiamua hata sasa vyuo hivi 3 vinauwezo wa kufanya mapinduzi makubwa sana.
Mohamed Dewj, na wengine wengi mfano mzuri wa watu waliosoma hivyo vyuo na kuja kufanya vema kwenye mazingira yetu.
 
Haaaaaaaahaaaaaaaaa !.
Tunataka tuonje radha ya chakula chetu tuone uhalisia wa uwezo wetu.
 
Back
Top Bottom