Habari Tanzania !.
Naomba niweke mawazo yangu hapa jukwaani.
Ikiwapendeza nawaomba mtumie huu mfumo ili mfanikiwe maendeleo;
1. Madiwani ndio waiongoze halmashauri;
(a) Mwenyekiti na Msaidizi wake wa Halmashauri wawe raia wa kawaida wasomi ngazi ya Shahada moja na kuendelea asitokane na udiwani.
(b) Hii itachochea maendeleo haraka vibaya mno. Pia itaondoa kuzorota kwa maendeleo mengi ndani ya halmashauri.
2. Spika wa bunge na naibu wake wasiwe wabunge kabisa yaani asitokane na kuchaguliwa na Rais au kuchaguliwa kuwa muwakilishi wa jimbo lolote Tanzania;.
(a) Spika na Naibu wawe wataalamu wa masuala ya Uongozi, Utawala, Uchumi na Maendeleo katika Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Hawa wataalamu wawe rasmi kutoka Vyuo vikuu hivi vifuatavyo (University of Dar es Salaam, Sokoine University na Muhimbili University pekee).
(b) Elimu zao kuanzia shahada ya kwanza katika fani za Maendeleo, Utawala na Uchumi.
3. Rais wa nchi asitokane na chama chochote cha kisiasa. Bali awe ni mgombea ambaye atafanyiwa usaili na vyuo vikuu vitatu (University of Dar es Salaam, Sokoine University na Muhimbili University) na akipitia vyama vya siasa vitachagua mtu wa kumnadi kama mtu wa mlengo wao na kupeleka ushawishi kwa wananchi nje na hapo tuachane na mfumo wa kizamani.
N.B
Karibu
Asante.