Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Ni mjinga tu ndio anaweza kudharau hili lakini ukweli
Ni mjinga tu ndio anaweza kudharau hili,lakini hili jambo linawezekana sana maana halina madhara kama kuandamana.

Sio lazima nitume hela kwa simu,ivyo inawezekana njia hii ikawa safer kuliko maandamano,KUSUSA HUDUMA NA BIDHAA NI SUALA LA KUBADILI TABIA TU IVYO NI NJIA NZURI SANA NA SALAMA SAAANA TU.

Nimejifunza kuwa huwezi kumdhibiti mwanadam.
 
Hivi huko mtaani mnakokuzungumziaga ni wapi? Maana sisi tuliopo humu ndo hao hao tunaoishi mtaani.
Upo sahihi!

Lakini inakuwaje joto la mtaani ni tofauti na joto la kwenye mitandao hususani suala ambalo linajadiliwa kwenye huu Uzi?
 
Kwanini halotel, airtel na tigo wao wapate faida wakati ughali wa vifurushi ulikuwa kwenye makampuni yote?
Hazijawahi kufanana! Mfano halotel elfu 1 unapata gb 1 na madakika kibao wiki nzima wakati voda hiyo elfu 1 hata mb 500 hupati.

Au kama unafikiri yakishuka sababu ya chadema kususia, mbona viongozi wako wote mpaka leo wanatumia voda?

Na hata pale makao makuu ya chama ukitaka kuwapata kwa simu moja ya namba za kuwpata ni voda.
 
Kinachonisikitisha ni pale wajinga wanaposhindwa kuweza kufanya vitu vinavyowezekana kirahisi kufanyika, wanakimbilia mambo magumu na hatawezekani kufanyika, eti wataweza!

Mnashindwa kuandamana, manashindwa kupeleka mazimio ya kulishitaki bunge kwa kukiuka katiba, mmeshindwa kufanya mikutano ya hadhara, mmeshindwa kushinikiza kupata tume huru, mje kuweza suala la kususa bidhaa, kitu ambacho kinafanyika pasipo video, nachokifanya mimi huku ng'wanh'uzi hawezi kukiona mtu aliyeko makambako ila tukikutana kwenye mitandao tunakubaliana tu kwamba, hatutonunua bidhaa fulani fulani, Chadema kichwa chenu sasa kina majimaji aisee
 
Basi siyo tu wapumbavu ila ni malofa
 
Kwasabu chadema wapo wachache hawatofanikiwa ,labda wananchi kwa ujumla bila kujali vyama ndio hiyo kitu itawezekana kumbuka walisusia voda mpaka sasa inadunda
Umewahesabu?
 
Ni njia nzuri sana na ina manufaa yafuatayo:

Inaondoa stress kwa wenye ndugu zetu walioteswa na mfumo wa CCM,eg. Nikikumbuka utesaji na unyanyasaji wa policcm naondoa stress kwa kutotumia Mpesa.

Nikikumbuka gharama kubwa za kodi na maisha,sinywi pombe ila situmii mifumo ya kifedha ya simu.

Inasaidia kupunguza gharama sana.

Ni mbadala wa maandamano...what a brilliant idea!
 

Sio hao uliowataja tu boss, ni wengi sana nafananishwa nao. Tena naona kama hii mbinu nimechelewa kuitumia. Una swali, hoja au maoni kwa msaada zaidi?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Nmecheka ila kiukweli nmekuonea huruma!
 
Hivi voda ilivyo sasa ndivyo ilikuwa miaka 5 iliyopita? Unajua voda imetengeneza hasara ya billion 60 mwaka Jana

Unafikiri ni kwanini wametengeneza hasara wakati

Airtel, Tigo na halotel wametengeneza faida?
Danganya wajinga, hakuna kampuni iliyohangaika kama halotel ni miezi kama miwili imepita Sasa tangu wafanye mabadiliko na Sasa ndo wameanza kurudi mdogomdogo.

Linapokuja swala la Vodacom huwezi kuilinganisha na watumiaji wa mitandao mingine, ukitaka kuamini angalia watu wanaodaiwa NIPIGE TAFU, SONGESHA na MPAWA, si ajabu hata humu wamo wengi tu.πŸ˜‚
 
Ni mbadala wa maandamano maana huku hawawezi kuja na wataomba poo very soon, ngoja tuonyeshane makali kwanza...

No salary for policcm

No payment for mataga

No harrassments..Hooray!
 
Vipi msiba wa kaka yake Mbowe, ulihudhuria?

Kwa hicho ulichoandika, nakuhurimia sana πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Good watu wasusie huduma mbovu za CCM
 
Vipi msiba wa kaka yake Mbowe,ulihudhuria?

Kwa hicho ulichoandika, nakuhurimia sana πŸ˜‚πŸ˜‚

Nihudhurie kwani nina ukaribu wa hivyo na Mbowe? Mwanaccm yoyote aliye karibu na mimi akifiwa au kuwa na hafla sihudhirii, na nitahamasisha hilo tena hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…