Huu ndio ujumbe wa Wakili wa Kimataifa bwana Robert Amsterdam kwa Serikali ya CCM

Huu ndio ujumbe wa Wakili wa Kimataifa bwana Robert Amsterdam kwa Serikali ya CCM

TANZANIA: DEMOKRASIA INAANGUSHWA KIMYA KIMYA

"Huko Tanzania, jukwaa linaandaliwa.
Sauti za upinzani zimezimwa, mikutano imepigwa marufuku, viongozi wamefungwa. Kadri uchaguzi wa mwaka 2025 unavyokaribia, kinachoandaliwa si uchaguzi—bali ni maigizo, na ni mwigizaji mmoja tu anayeruhusiwa kuzungumza."

— Wakili wa Kimataifa Robert Amsterdam (tweet ya tarehe 10 Jun,2025, Muda:7:46PM)

View attachment 3363829


Wakati dunia inatazama kimya, haki ya Watanzania kuchagua viongozi wao kwa uhuru inazidi kuzimwa.
Je, tunaelekea kwenye uchaguzi wa kidemokrasia au maigizo yaliyoandaliwa kwa mtindo wa upande mmoja?
Demokrasia haiwezi kustawi penye woga, ukandamizaji na mdomo kufungwa.
Ni wakati wa kusimama, kuuliza maswali, na kutetea haki!

#Tanzania #Demokrasia #Uchaguzi2025 #RobertAmsterdam #Haki #SautiYaRaia #NOREFORMNOELECTION
So What!!!!!
 
Uchaguzi no lazima ufanyike, hakuna wa kuuzuia
Na katiba haisemi kwamba chama kimoja kati ya 20 ikisusa basi uchaguzi hautafanyika. Hiyo msimamo ya skanka na mapovu mdomoni haitaisumbua serikali
 
  • Thanks
Reactions: UCD
UKWELI AMBAO HAUFICHIKI
viongozi wa ccm na vibaraka wao hawatumi akili kuliko nguvu : hata katiba iko wazi hairuhusu mshatikiwa kupelekwa mahakamani bila ushaidi lakini leo hii lissu yuko rumande na jamuhuri inasema haijamaliza upelelezi wanapinga katiba inayo ongoza nchi yetu mbele ya macho yetu
madeni yanayo kopwa kutoka nchi za kigeni ni asilimia 2 tuu ndio inaelekezwa kwa maendeleo ya wananchi asilimia 25 inachukuliwa na viongozi asilimia 73 inashikiliwa na serekali nzima
Tunalipa Kodi tunakopa madeni ili tujaze mifuko na matumbo ya viongozi wasio jali Juu ya Wananchi ila juu ya Familia zao
CCM WANATAKA VYAMA VISHIRIKI UCHAGUZI WALA SIO KWAMBA WANATAKA VYAMA VISHINDANIE KUPITA KATIKA HUO UCHAGUZI...
WANAOMBA HAKI WANAHAMIA KWA WANAO PAMBANIA HAKI CCM MTASIMAMA WENYEWE BILA KIVULI CHOCHOTE
 
Kua mzalendo mkuu.....

October Piga kura....Kwa maendeleo yako

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Mzalendo ni kuwa Mfiraji, Mtekaji na Muuaji.
Mzalendo ni kuuza Ngorongoro kwa Waarabu.
Mzalendo ni kuuza Bandari kwa Waarabu.
Mzalendo ni kubinafsisha Mwendokasi kwa Waarabu
Mzalendo ni kuuza Uwanja wa ndege kwa Waarabu.
Mzalendo ni kufungia makanisa kwa sababu ya kukosoa utawala.
Mzalendo ni kumuweka ndani mpinzani wako, kwa kosa la Uhaini.
Mzalendo ni kukopa Tril.30 kwa mkupuo huku Gawio la Serikali kwa mwaka ni Tril 1.28
Mzalendo ni kuchezea pesa za walipa kodi na kuonga wasanii na wachezaji mpira.

Laiti mngelijua yale yaletayo amani, lakini sasa yamefichika ili msiyaone.
 
CCM ipo kwenye nyakati ngumu sana .

Mbaya zaidi imeishiwa hadi watu wema wenye sifa ya kusikilizwa wanakuzungumza .

Wale wazee wawili wapo upande wa raia , yule mmoja miongoni mwake amekosa mvuto na yule Baba wa mtoto hana alichokizungumza zaidi ya kujipaka tu kinyesi ,bora hata asingelizungumza ili kuadd value kwa mwanae .

CCM iko kwenye wakati mgumu sana .
Wamtumie mchungaji Msigwa kada wao awasemee
 
Back
Top Bottom