ksny
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 1,704
- 1,694
Ni kweli nchi za magharibi zimekuwa zikitoa misaada, lakini hiyo missada inatolewa na msharti ambayo mwisho mnufaika mkubwa anakuwa ni mtoaji msaada. Kumbuka nchi kama Kenya ilipata uhuru 1962. Tanzania ilipata uhuru 1961. Mwaka 1962 uchumi wa Kenya ulikuwa unalingana na wa Korea ya kusini. Uchumi wa TZ uliukaribia ule wa Vietnam (kabla haijachakazwa na Maarekani). Leo nchi hizo mbili zina uchumi wa juu sisi bado maskini wa kutupwa. Misaada mingi ililenga kututia ganzi tuendelee kuwa tegemezi. Na tumerudi huko na sasa tunapewa mikopo left and right bila kukumbuka tunakiwa kuilipa.Hakuna msaada wa bure, wao wanakomba mara kibao ya wanavyoleta.
Mfano mzuri Magufuli alipigwa biti asiwaguse Barrick la sivyo wanasitisha misaada.
Baada ya kuanza kushambuliana kuhusu misaada fikirieni ni vipi mtaji toa kwenye budget deficit,
Sio sifa kujisifia misaada.
Tunapopata mikopo toka magharibi au mashariki tunawakaribisha kchimba madini yetu bure, kwa sababu tunakubali mikataba mibovu ambayo ukifurukuta unafirisiwa. Kwanza unatupiwa chambo (msaada), alafu wanakuja kuchimba madini kwa mkataba waliyoandika wao. Misaada mingi tunaipokea bila kufikiria, hela ya msaada itakapokoma kilichoanzishwa kitaendelezwa vipi. Je kuna mpango mzuri wa takeover toka msaada. Kama huna njia ya kuendesha mradi baada ya hela ya msaada kukauka, itakuwa sawa na bure. Lakini mwenye msaada alishapata mgodi atakaochimba kwa masharti yake kwa miaka 50. Baada ya miaka 50 unaachiwa shimo, michanga, na kemikali (enironmental hazards)