Huu ni ushamba, kupanga mstari kumsindikiza Rais akienda Ulaya

Huu ni ushamba, kupanga mstari kumsindikiza Rais akienda Ulaya



Nilidhani huyu mama yenu atakuwa tofauti na waliomtangulia.

Kwamba hatoendeleza huu ushamba wa viongozi mbalimbali wa serikali na idara kwenda uwanja wa ndege kumsindikiza aendapo safari na pale arudipo toka safarini.

Yaani majitu yote hayo, kuanzia makamu wa Rais, mawaziri, sijui mkuu wa mkoa, mkuu wa jeshi la polisi, mkuu wa jeshi la wananchi, viongozi wengine waandamizi wa kijeshi na kiaskari [nadhani nimemuona na wa magereza hapo], na chawa wengine.

Si ajabu hata yale Maharage ya Tanesco yalikuwepo hapo.

Huu ushamba ni matumizi mabaya ya muda wa uzalishaji.

Badala ya kuwa maofisini huko na sehemu zingine za kazi, majitu yote hayo yanaenda kurundikana na kupanga mstari kumsindikiza Rais akienda Ulaya.

Ushamba na ujuha wa kiwango cha juu kabisa.

Na Rais naye hana busara ya kuwaambia hakuna haja ya kunisindikiza wala kunipokea uwanja wa ndege, na badala yake endeleeni kupiga kazi.

Sisi bado sana aisee!

Mbona ameonekana akipanda gari hapo ni wapi
 

Kuna tofauti kubwa sana
  1. Huku kwetu angetandikiwa zuria jekundu lakini kwao hawana huo muda
  2. Huku kwetu uwanja wa ndege ungefungwa, lakini kwano nimeona ndege kwa mbali ina takeoff
  3. Huku kwetu tungeona mabunduki ya kila aina kumlinda kiongozi lakini wao wamevaa suti as if wote bu waheshimiwa
 
Kwamba wanachezea kodi?
Hiyo ni shida,
Ila kusindikizana na kuagana sioni ubaya,
Ikiwa wapo free
 
Wengi humu ni wanafiki na unafiki umewazidi ni aibu sana kwani juzi tu tulikuwa tunamsema Magu asafiri tulifikia hadi hatua ya kutaka kumsafirisha kwa nguvu kwenda hata kanchi kokote Ulaya lakini alikataa kata mpaka Sugu akawaka sana lakini alikataa wacha mama aende na asindikizwe hata akikaa huko huko kama Lisu akirudi 2025 kuchukua urais wake poa.
 
Tanzania chini ya CCM Rais ni zaidi ya Mungu.

Hapa ni Bwana Chato alikuwa anaambiwa kuwa ni mkubwa na mkuu kuliko Mungu,Yesu na Mtume🐒🐒🐒
 
Kuna tofauti kubwa sana
  1. Huku kwetu angetandikiwa zuria jekundu lakini kwao hawana huo muda
  2. Huku kwetu uwanja wa ndege ungefungwa, lakini kwano nimeona ndege kwa mbali ina takeoff
  3. Huku kwetu tungeona mabunduki ya kila aina kumlinda kiongozi lakini wao wamevaa suti as if wote bu waheshimiwa
unahamisha magoli. Joe Bidden yupo ndani ya nchi huyo hakuna haja ya zulia jekundu. Hayo mengine nakuachia mwenyewe
 
Labda kama mimi mgeni humu ila wengi tunamjua Nyani wa Kikwete na wa Magufuli ni mbingu na ardhi
Wewe ni muongo. Na mzushi pia.

Magufuli nimemkosoa sana humu na ushahidi upo.
 
Back
Top Bottom