Huu upweke unaniathiri sana akili mpaka nayakatia tamaa maisha

Okay sawa kumbe hana shida ndogo ndogo, kwahiyo yuko wapi sahivi ๐Ÿ˜น๐Ÿ˜น ajibu pm chaaap tumalize sikukuu.....tuuaibishe upweke
 
Mbona mm nimekataliwa na madem wote niliowatongoza miaka hii minne na sijisikii upweke? Acha ujinga bwege wewe
 
Pole. Piga kazi kwa bidii hao wote watakuja. Waliokuwa karibu na wewe ni kwa sababu ya mama yako alipotoweka hakuna kiunganishi. Ingekuwa rahisi endapo mama angeacha biashara inayokuunganisha nao.

Haturithi marafiki tengeneza empire ya kwako. Ila ID yako haiendani na kukataliwa na wanawake
 
Hakuna mwanamke anayekataa mwauame, tafuta wanawake wa hadhi yako, acha kutaka wanawake wenye hadhi kuliko wewe utakufa mapema, wapo wanawake ukimpa elf tano anakushukuru siku tatu
 
Nenda vijiweni,cheza draft,uta-socialise na watu,kuhusu utelezi, hicho ni kitu chepesi kuliko mlo
 
Umejaribu kumkimbilia Yesu akashindwa kukusaidia? Yeye anasema katika Mathayo 11:28-29:
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsi zenu."
Tena ujue mke mwema mtu hupata kutoka kwa Mungu.
 
Duh ww ulikuwa na upweke wa kipato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ