Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Shida ni hizo kero Imani haiwezi Kuna tatizo kwangu kwasababu natambua kila mtu anayo haki ku-practice Imani yake lakini katika kiwango kisicho leta usumbufu kwa wengine ,ndio maana tunapiga kelele sauti za mahubiri jioni na za adhana asubuh zipunguzwe na sio zitolewe ,Kila kitu kifanyike mahala pake palipo kusudiwa
mkuu usichokijua, sawa na watu wengi ni kwamba SISI ni mali ya MUNGU, yeye ndiye aliye tuumba,. Na huyu Mungu anataka kuabudiwa kila wakati na mahala popote. Mungu hawekewi mipaka wala hapangiwi muda. Shetani napotosha watu kupitia UFAHAMU na HEKIMA ya kidunia na kujiona kuwa wanaweza jipangia watakavyo wao. HEKIMA za mwanadamu ni upumbavu wa kutosha mbele za Mungu.
Walio wa SHETANI hawawezi mpenda Mungu wala hawatakubali kwasababu wamepofushwa fikra zao, hata kama iweje haiwezekani kuelewa kuwa MUNGU anapaswa kupendwa, kupewa kipau mbele, kusifiwa na kuinuliwa wakati WOOOTEEE.

ukiona kwako unatumia HEKIMA eti, injili ina mahala pake - jua tu nawe ni fungu moja na SHETANI(IBILISI). Hapo ni Huruma za Mungu zikufukike tu, kwakweli.
 
Unajichanganya. Nishakusoma tatizo lako. Jaa nguvu za Mungu hutasumbuliwa na imani ya aina yoyote.
Wala hakiwezi kuwa na msaada kwangu , Asante kwa ushauri lakini
 
Ina maana haitoshi kuhubiri kanisani au kujenga jukwaa na ukahubiri zako hadi usumbue watu kwenye mabasi
Usumbufu???


Kwani hilo bus ni mali yako Mkuu?
 
Napenda mahubiri...

Neno la Mungu ni taa na mwanga linatumulika popote tunapokwenda...
Ndio sababu kukawepo na makanisa,mm nina mawazo yangu labda naenda kwa mganga au mm sio wa imani hio unayoihubiri hapo inakuwaje?,mnakeraaa saana
 
Tena sio kidogo,kuna siku nilikuwa naelekea Tanga kufika michungwani akapanda jamaa ana bidhaa anauza baada kumaliza matangazo yake,akaanza kuhubiri sijui Yesu ni bwana mbona raia walimkimbiza[emoji23][emoji23]
Yaan utafikiri umelipia na hayo mahubiri wenyemabasi hawa wazuie
 
Kijana pepo limefika level ya kuona mahubiri ni kero.
 
Mkuu acha kiburi cha uzima. Shetani anakuwa kazini sana kipindi cha safari. Ndio maana madereva wametulia hawapati kero ila wewe abiria unaona kero.
Juzi nilikutana na Shetani,analalamika sana nyinyi wanadamu mnafanya ujinga wenu wa Kibinaadamu alafu mwisho wa siku mnamsingizia yeye kua ndiyo kasababisha! Mfano dereva akiwa mzembe kwenye gari na kupata ajali bado lawama mnazipeleka kwa Shetani, jitambuweni na mtaishi kwa amani tu bila kupiga Makelele kwa kisingizio Cha mahubiri!!!
 
Usumbufu???


Kwani hilo bus ni mali yako Mkuu?
Inaweza ikiwa Mali ya umma au private swala la kuzingatia ni USTARABU wa watu wengine wala haliitaji kitu kiwe Chako au Cha jamii nyumba inaweza kuwa yako lakini kutudundishia mziki mkubwa saa nane za usiku ni kuharibu starehe na utulivu wa wengine.

Naomba nieleweke hapo mkuu
 
Juzi nilikutana na Shetani,analalamika sana nyinyi wanadamu mnafanya ujinga wenu wa Kibinaadamu alafu mwisho wa siku mnamsingizia yeye kua ndiyo kasababisha! Mfano dereva akiwa mzembe kwenye gari na kupata ajali bado lawama mnazipeleka kwa Shetani, jitambuweni na mtaishi kwa amani tu bila kupiga Makelele kwa kisingizio Cha mahubiri!!!
Huo uzembe nao ni ushetani. Dereva mwenye hofu ya Mungu hawezi kufanya huo ushetani.
 
Mtu unasafri zako unahitaji mapumzko anatokea mtu anajifanya analeta neno la Bwana bila kujua watu waliopo ndani wanatatizo gani wengine hawataki kelele anajifanya anahubiri dakika 3 anaomba sadaka.

Hebu tufanye kazi tusijifiche kwa kivuli cha kuhubiri na kulazimisha sadaka.
Wanatuhubiria injili kwan Sisi ni Wana wa Israel?
 
Mnaomwambia mtoa mada anunue gari lake kwamba nyie mnapenda mahubiri....na nyie nunueni yenu kwan yeye pia hapendi mahubiri
 
Back
Top Bottom