Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Huu utaratibu wa kuhubiri injili kwenye magari ya abiria ni kero kubwa, LATRA muingilie kati

Ushauri wa bure kwa mleta uzi.

Nunua gari lako.
Simama mwambie aache kuhubiri
Weka earphone masikioni.
Tembea kwa mguu usipande hizo public transports

Huwa nashangaa sana mtu hataki kusikiliza neno la Mungu anataka asikilize nyimbo za akina diamondi zainazo imba weka mate iteleze kama nyoka pangoni.

Kazi kweli kweli.
 
Inaweza ikiwa Mali ya umma au private swala la kuzingatia ni USTARABU wa watu wengine wala haliitaji kitu kiwe Chako au Cha jamii nyumba inaweza kuwa yako lakini kutudundishia mziki mkubwa saa nane za usiku ni kuharibu starehe na utulivu wa wengine.

Naomba nieleweke hapo mkuu
kukwepa hizi dhahama mkuu NUNUA GARI YAKO BINAFSI
 
huu utaratibu upo Kenya, zambia ,congo na Zimbabwe ...mabus yote huwa wanaingia watumishi na wanaomba na kusepa

hamna namna vumilia tu -kama mapepo yamechukua hatamu kichwani mwako tulia tu
Mapepo yamejaa kwa wagalatia kutwa kuchwa kudondoka makanisani
 
Jibu hoja achaa hasira za mkizi, kwani tuko hapa kujua mmiliki wa bus au Makelele ndani ya bus!!??
Mkuu ukichoka kelele za mwenye Nyumba uamuzi sahihi ni kujenga Nyumba yako vivyo hivyo kwenye usafiri wa umma
 
Ushauri wa bure kwa mleta uzi.

Nunua gari lako.
Simama mwambie aache kuhubiri
Weka earphone masikioni.
Tembea kwa mguu usipande hizo public transports

Huwa nashangaa sana mtu hataki kusikiliza neno la Mungu anataka asikilize nyimbo za akina diamondi zainazo imba weka mate iteleze kama nyoka pangoni.

Kazi kweli kweli.
Kwani kusikiliza neno la mungu ni lazima?
 
Mkuu ukichoka kelele za mwenye Nyumba uamuzi sahihi ni kujenga Nyumba yako vivyo hivyo kwenye usafiri wa umma
Kwa hiyo kisa usafiri wa Umma ndiyo kila Mtu ajifanyie anavyotaka ndani ya bus!? Mkuu kila sehemu ina utaratibu wake,tuheshemuni hilo ili kupunguza kuwakera wenzetu!!
 
Mtu unasafri zako unahitaji mapumzko anatokea mtu anajifanya analeta neno la Bwana bila kujua watu waliopo ndani wanatatizo gani wengine hawataki kelele anajifanya anahubiri dakika 3 anaomba sadaka.

Hebu tufanye kazi tusijifiche kwa kivuli cha kuhubiri na kulazimisha sadaka.
Wanakera mno!
 
Sasa tumalize ubishi mkuu NUNUA bus Alafu wapige marufuku
Hatubishani sisi hapa tunafahamishana kama watu wazima tuliostaarika ,hata nikilinunua Hilo bus Bado usumbufu hauta koma .

Tukiwa na shida ya mahubiri tunafungulia redio tuwasikilize au tutakuja kanisani kwa ridhaa zetu na kama mnataka tupate mahubiri basi andaeni semina maalumu au jengeni majukwaa watu watakuja kwa hiari zao
 
Akishamaliza mahubiri atasema, mwenye sadaka yoyote ya kumtolea bwana
 
mtoa mada


 
Acha kila mtu afurahie uhuru wake pasipo kuvunja amani

Alafu Acha shobo ukiwa na gari yako binafsi hutasumbuliwa na mhubiri yoyote
Wewe huoni anakera uhuru wa watu na kuwaingilia. Achana na porojo za mtu kuwa na gari yake hapa, haya mambo ya kuhubiri kila mahali kwenye magari ni kero sana. Pollution everywhere yani..
 
Back
Top Bottom