🔷 Ni vyema Mgeni anapofika kwako kwa mara ya kwanza akapokelewa na utamaduni wenu
🔷 Mimi sipingi wageni kupokelewa na burudani wanapofika kwenye malango ya nchi yetu ni jembo jema Sana na la kiungwana
🔷Lakini je! Wanaowapokea wanawawakilisha utamaduni halisi wa kabila lolote la Mtanzania?
🔷 Tanzania tuna ngoma ya asili ya matarumbeta? Tanzania tuna ngoma ambayo watu wanavaa sare kama waimba kwaya?
🔷 Ngoma ninazozijua Mimi watu wanavaa mangozi, manyoya ya wanyama, maleba, njuga , sura za vinyago na kujipaka mavumbi mazizi na makorokocho ya kutisha huku wakichezea wanyama pori kama nyoka, fisi nk huku manyu akitamba mbele kwa kujirusha au kupiga ngoma kwa tumbo makalio nk hata mtoto mdogo akiona analia au Mgeni akiona anajua amefika nchi ya kiumeni Afrika.
🔷Sasa wapo wajanja wajanja wa hapo Dar eti wsnapuliza matarumbeta au wale wa chuo Cha bagamoyo wanaocheza ngoma zilizochakachuliwa na utamaduni wa wazungu wa Scandinavia ndio eti wanatambulisha utamaduni wa bongo
🔷 Doctor Mapanaa naamini upo huku unanisoma, kama uliwaimbisha wazungu kigogo huko ulaya na wakaimba na kucheza kweli unashindwa kutafuta kikundi halisi Cha ngoma Kupokea wageni wetu ? Unashindwa kweli kwenda singida Kuna wanyaturu wanaocheza Mawindi, wagogo wapo Dodoma na mbwembwe zao, shinyanga Kuna maguno ya Jeshi, Mwanza Kuna Mwanalyaku, , bujora na Ukerewe vipo vikundi halisi vya ngoma achana na vidogoli vya wajita na wakerewe wale watachelewesha mambo maana wanaongea Sana mpaka waje wskatike sio Leo. Mara Kuna watu watatikisa vichwa yule jamaa wa Kenya wa kuandamana usiku Cha mtoto
🔷Morogoro Kuna vitu vya hatari, kusini ndio usiseme Sindimba, mganda nk .
🔷 Kaskazini Kuna wamasai wanaruka juu balaa na ni marafiki wakubwa wa watalii, Tanga Kuna ngoma zao nyingi tuu, acha zile zinazochezwa na wanawake Kuna zile za wawindaji ( naukala ndima) zima mvuto wa kipekee, Wachaga achana nao wamedanganywa na dini na kuambiwa Mila na ngoma zao ni za kizamani. Wameacha ngoma zao za kuzunguka kama mduara Sasa wamekuwa kama watumwa wakienda nje wakiambiwa waonyeshe utamaduni wao wanajifanya wamasai kama mwijaku.
🔷 Hivi doctor Mapanaa na Wizara ya utamaduni hamuoni hata ngoma za wahaya wanavochenkula?
🔷Nchi likubwa kama hili tunashindwa kufanya venting ya kikundi Cha ngoma ambacho Mgeni akiona ataendelea kuota Maisha yake yote? Shida nini? Kama NDEGE tunayo tunadondwa kusafirisha vikundi vya ngoma na makorokoro Yao yote tena wakiwa kwa wingi wao na sio watu wachache tukaitamgaza nchi yetu baadaye tukapata return ya utalii wa kitamaduni? Mama naomba uteuzi Mimi avogadro kwenye Wizara ya utamaduni , Mimi nita deal na utamaduni tuu hii michezo imeimeza na ndani ya mwaka utamaduni utaamka na tutaamza kushuhudia mafurikonya watalii