Huu Utitiri wa Maofisa wa Serikali kwenda Hanang, Wanaenda Kufanya Uokoaji au Kuonekana?

Ni mwendo wa kusaininposho mkuu wala usijipe tabu. Hapo alitakiwa afike mkuu wa wilaya tu na kila kitu kingeweza kuratibiwa. Dalili ya familia ya kambale ndio hii. Hadi mtoto wa siku moja ana ndevu.
 
MAOKOTO
 
Ila hii nchi inapesa aisee, hapo tu viongozi wameenda tu kwenye maafa mashangingi yameongoza kama yote
 
Wanafuata perdiem ya kodi zetu mkuu. Au huwajui hawa viumbe. Usisahau kule kuna watoto wa Kiiraq.
 
Kwa mara ya kwanza umehoji jambo la msingi !
 
Hata mimi nina mpango wa kwenda
 
Kibaya zaidi, hawaendi bure hao, posho ya safari na marupurupu mengine watapewa.
 
Fedha nyingi itatumika kulipa posho wakubwa badala ya wahanga na waokoaji
 
Ukifika kwenye ofisi za serekali huko utakuta hadithi ni ujio wa rais, na Wala sio wahanga wa tukio!
Inawezekana ni maandalizi ya maza kutua huko hao maofisa wengine wanatangulia ili kuweka mazingira sawa😀😀
 
Kibaya zaidi, hawaendi bure hao, posho ya safari na marupurupu mengine watapewa.
Yani hapo ni misafara na kuhudumiwa kwa kodi zetu ilhali wangeweza kutulia maofisini na kutoa maelekezo maana hawaendi kufanya uokozi wowote zaidi ya kuuza sura na mitambi yao kuna mmoja nimemuona ana mtumbo mkubwa km beseni
 
Ukifika kwenye ofisi za serekali huko utakuta hadithi ni ujio wa rais, na Wala sio wahanga wa tukio!
Kuna ambao wanataka kumuona rais, mwache aende akatalii
 
Lazima wakawafariji ndugu zetu
Sio mbaya maana hali sio nzuri huko na hilo tope likikauka ni mtihani mwingine
Wameenda kuongeza nguvu pia kwa mfano uwepo wa mkuu wa majeshi na wahandisi hata Boss wa zimamoto ni sawa akiwa hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…