Huu Utitiri wa Maofisa wa Serikali kwenda Hanang, Wanaenda Kufanya Uokoaji au Kuonekana?

Huu Utitiri wa Maofisa wa Serikali kwenda Hanang, Wanaenda Kufanya Uokoaji au Kuonekana?

Mtu tajiri aliyezungukwa na masikini wasio na idadi naye ni masikini tu. Hujiulizi kwann hao mnapwaita matajir wanamiliki mabunduki, fance za umeme na walinzi kibao tena kwenye nchi ya amani na ya mazuzu kama hii?
Matajiri kujilinda ni kawaida nenda kaulize nchi zenye uchumi mkubwa kama Marekani,ukaone budget wanazotumia akina Elon Musk,Bezo,Marc kwa ulinzi binafsi pekee.
 
Hii ni comment ya BLACK MOVEMENT kwenye uzi Hanang imeniumiza kweli.
Hivi sisi watu weusi tunashida gani?

Mdau mmoja aliopo eneo la tukio kule Hanang anasema kuna zaidi ya V8 78 za viongozi mbalimbali hadi sasa hivi, huku kukiwa hakuna vifaa maalumu ya uokoaji huku walio athiriwa wakiambiwa watafute hifadhi kwa ndugu jamaa na marafiki. Wananchi wanafanya kuhesanu V8 barabarani kwa sasa.

V8 zinafanya kupishana Hanang, huku kukiwa hakuna vifaa vya kufanya uokoaji, kukiwa hakuna mahema ya wahanga na kukiwa hakuna Chakula cha wahanga zaidi ya wahanga kwenda kuomba chakula kwa nduhu na jamaa na marafiki.

Serikali inangoja kuzika walio kufa kwa kugharamikia majeneza huku walio hai wakiendelea kutaaabika bila msaada wowote ule.Viongozi wanaenda kupiga picha kule na kuonekana walikuwepo eneo la tukio.

Raia wanahitaji misaaada na sio wingi wa viongozi kwenda kupiga picha eneo la tukio.

Jinsi sisi weusi tulivyowaajabu usishangae mods kuunganisha.
 
Sijasema wakubwa wasiende ila napenda watakaokuwa front ndio watangulie plus Mahitaji ya Waathirika badala ya kwenda kuleta taharuki nyingine.

Huko PM yupo
Mkuu wa Majeshi yupo
Mawaziri wapo

Na wengine wanaendelea kumikinika ,Sasa sijajua Kama Kasi ya wakubwa kumikinika inaendana na Kasi ya Uokoaji.

Mlioko eneo la tukio tuambieni kama mnapata mahitaji stahiki kuanzia tiba,mahema,vyakula,maji,nk?

Pia soma > Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 49

---
PICHA: BAADHI YA VIONGOZI WALIOZULU HANANG

View attachment 2833818View attachment 2833819
Na wewe nenda
 
Sometime kuna vitu unajiuliza hivi kuzaliwa africa ni mateso.Kuna mambo hua yanafanyika unaweza kufuru l.Malawi ilipopata mafuriko kuna msaada mpaka wa msosi tulipeleka sasa hapo manyara kwa nn inashindikana[emoji3062]
 
Hii ni comment ya BLACK MOVEMENT kwenye uzi Hanang imeniumiza kweli.
Hivi sisi watu weusi tunashida gani?

Mdau mmoja aliopo eneo la tukio kule Hanang anasema kuna zaidi ya V8 78 za viongozi mbalimbali hadi sasa hivi, huku kukiwa hakuna vifaa maalumu ya uokoaji huku walio athiriwa wakiambiwa watafute hifadhi kwa ndugu jamaa na marafiki. Wananchi wanafanya kuhesanu V8 barabarani kwa sasa.

V8 zinafanya kupishana Hanang, huku kukiwa hakuna vifaa vya kufanya uokoaji, kukiwa hakuna mahema ya wahanga na kukiwa hakuna Chakula cha wahanga zaidi ya wahanga kwenda kuomba chakula kwa nduhu na jamaa na marafiki.

Serikali inangoja kuzika walio kufa kwa kugharamikia majeneza huku walio hai wakiendelea kutaaabika bila msaada wowote ule.Viongozi wanaenda kupiga picha kule na kuonekana walikuwepo eneo la tukio.

Raia wanahitaji misaaada na sio wingi wa viongozi kwenda kupiga picha eneo la tukio.

Jinsi sisi weusi tulivyowaajabu usishangae mods kuunganisha.
Kufa kufaana.
 
Mdau mmoja aliopo eneo la tukio kule Hanang anasema kuna zaidi ya V8 78 za viongozi mbalimbali hadi sasa hivi, huku kukiwa hakuna vifaa maalumu ya uokoaji huku walio athiriwa wakiambiwa watafute hifadhi kwa ndugu jamaa na marafiki. Wananchi wanafanya kuhesanu V8 barabarani kwa sasa
Mdau aliyepo huko amesema.
 
Yote kwa yote tuwashukuru kwa kwenda kuwajulia hali nako Kuna faraja yake [emoji1431][emoji1431],,
 
Ni muhimu wizara na taasisi mbali mbali zishughulikie kurudisha hali ya kawaida haraka ipasavyo ili wananchi warudi katika uzalidhaji na ujenzi wa taifa.
Hili linahitaji watumishi na viongozi kua mstari wa mbele.
 
Back
Top Bottom