Huwa mnadili vipi na ndugu wa aina hii?

Iko hivi mkuu ishu siyo ukubwa wala udogo wa hiyo pesa ila hii tabia ya kuniomba omba kila mara ndiyo inayonikera
Mwambie ni vema akafanya shughuri ya kumwingizia kipato, kwani Kuna siku utakuwa Hauna pesa ya kumsaidia,kwani siku hazifanani.Atafute mtaji nusu na we mwongezee nusu na uhakikishe anaanza kama ni biashara.Kisha mnaachana hapo ili asipate sababu ya kukulaumu! Ahsante.
 
Kuna watu wao kila akikupigia simu ni kuomba hela tu bila kujali juzi ulimtumia pesa tena nyingi tu. Yaani huyo keshakuona wewe ATM yake. Muweke ignore list
Hapo nimeanzia mwishoni ila ananiombaga mara nyingi sana
 
Kama alipata more than one million hakufanya biashara yoyote unadhani hata nikimpa laki 1 anaweza kufanya biashara, ni kwamba hawezi na mimi siwezi kupoteza hela yangu kumsaidia mtu asiyekumbuka wengine akiwa nacho
 
Mimi ni mdogo wako wa kike lakini hunipagi hela.

Kazi kuhonga mashangazi yaliyochoka tu.
 
Hivi huwa hawaonagi aibu watu wa hivi, na je kila akikupigia huwa unamkopesha?
Unawaendekeza, japo shida Haina mwenyewe... Jifunze kusema hapana. Ukimwambia huna zaidi ya mara tatu hatokutumia Tena sms za kulia Lia njaa. wote tuna majukum bhn toa pale ambapo Kuna uhitaji wa mhimu shem langu mrembo
 
Wanazingua sana na wanajua muda wote una pesa kwenye simu au bank.....Ukimwambia huna yaani hapo ni kukutangaza kwa ukoo mzima kwamba una roho mbaya.

Yaani utashangaa mtu anakuomba elfu 10 wakati anaweza akabustisha au akasongesha au akachukua kwenye timiza ,mgodi au kamilisha au nivushe plus....mimi elfu 10 nampa ndugu wa damu tu ila jamaa au marafiki nawatosa coz najua hapo hahitaji ila anakupima imani ili akaongee sasa ili akaongee vizuri namtosa maana binadamu hajaribiwi.
 
Usishindwe na ubaya Bali ushinde ubaya Kwa wema

Kama unayo mpe.nae Mwenyezi atakubariki maradufu.
Na usifanye wema Kwa mtu Kwa ukiangalia amekusaidia Nini kwamba umrudishie wema wake.kama Kwa ndugu tu uko hivi vipi Kwa wahitaji?

Hata kwetu wapo
 
Usishindwe na ubaya Bali ushinde ubaya Kwa wema

Kama unayo mpe.nae Mwenyezi atakubariki maradufu.
Na usifanye wema Kwa mtu Kwa ukiangalia amekusaidia Nini kwamba umrudishie wema wake.kama Kwa ndugu tu uko hivi vipi Kwa wahitaji?

Hata kwetu wapo
Asante mkuu nitamsaidia kama nitakuwa kwa wakati huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…