Huwa mnadili vipi na ndugu wa aina hii?

Huwa mnadili vipi na ndugu wa aina hii?

Za jumapili wakuu moja kwa moja kwenye mada, hivi huwa mnadili vipi na ndugu wa namna hii yeye akikutafuta ni kukuomba hela tu,, na hakuna chochote anachokusaidia kwenye maisha yako.

Ni dada yangu mtoto wa mama angu mkubwa, kuna kipindi waliuza eneo lao kama milioni 30 hivi, wakapewa mamilioni yao na mama yao, sikuwa napigiwa simu nilitumiwaga elf30 tu, na kipindi hicho nilikuwa nahihitaji support ya pesa ya ada ila walijikausha, wakaenda kununua eneo huko maporini hatimaye kumewashinda huko wamerudi huku Dar wamepanga.

Ndiyo huyu dada sasa ni mara nyingi sana ananitumiaga meseji za mara nimkopeshe hela mara nimsaidie mimi, anadhani nimesahau walichonifanyia, naombeni ushauri wenu huwa mnafanyaje kwa ndugu kama hawa.
View attachment 3429287
Unampotezea tu. Kumbuka wewe sio Yesu wa ukoo. Kwa kufanya hivyo itachagiza wao kuchakarika kujitafutia mkate wao wa kila siku kuliko kuishi kama wakimbizi wanaosubiria UNHCR iwaletee mahitaji yao yote
 
Mueleweshe kwamba sio wakati wa shida ndio akutafute
Na sio wakat hana hela ndio akutafute


Bora ww kuna wengn wanapigiwa ni mambo ya misiba tu
Yani unajua huyu akipiga ni msiba
Bonge la msala
 
5,000 au 10,000 mbona pesa ya vocha tu hiyo si umpatie tu mwenzako amekwama?

Anyways,mtafutie shughuli ya kufanya au mwite umshauri kuwa pesa zinapatikana bila shida kwa watu wenye shughuli za kiuchumi.
 
Mwambie ni vema akafanya shughuri ya kumwingizia kipato, kwani Kuna siku utakuwa Hauna pesa ya kumsaidia,kwani siku hazifanani.Atafute mtaji nusu na we mwongezee nusu na uhakikishe anaanza kama ni biashara.Kisha mnaachana hapo ili asipate sababu ya kukulaumu! Ahsante.
Exactly hichi ndicho alitakiwa kufanya mleta mada na sio kuja humu na uzi wa kumdhalilisha ndugu yake
 
Back
Top Bottom