Huwa mnadili vipi na ndugu wa aina hii?

Acha tu mkuu na wakipata za kwao hawatukumbuki kabisa
 
Unawaendekeza, japo shida Haina mwenyewe... Jifunze kusema hapana. Ukimwambia huna zaidi ya mara tatu hatokutumia Tena sms za kulia Lia njaa. wote tuna majukum bhn toa pale ambapo Kuna uhitaji wa mhimu shem langu mrembo
Asante shemeji, mama Antipas hajambo?
 
Umbali aliouweka wakati wa shida zako, Na wewe weka umbali huo mara mbili zaidi, wakati wa mafanikio yako.

Kila mtu akale alikopeleka mboga.
Binadamu huwa wanajisahau sana yaani, mimi nimeamua kuwa peke yangu kama walivyoniacha nilivyohitaji msaada wao lakini bado wananifata🥲
 
Kama alikupatia japo 30000 bado ni mtu mwema kwako kwani alikujali.
Mpatie tu kama unayo kwani kukuomba wewe inaonesha ana imani kwako. Tunza imani hiyo kwani ni baraka pia.
 
Msaidie tu Kwa kilicho ndani ya uwezo wako.
Kama Kiko nje ya uwezo wako mwambie sina.akikujibu asipojibu sawa.

Mi mwenzio nlikuwa na pesa nkasaidia pale walipokwama hata Kwa kidogo.ilipofika zamu yangu mbona nlipotaja shida tu nlikula block.
Ila binadamu ni wabinafsi sana dah, pole sana
 
Kama alikupatia japo 30000 bado ni mtu mwema kwako kwani alikujali.
Mpatie tu kama unayo kwani kukuomba wewe inaonesha ana imani kwako. Tunza imani hiyo kwani ni baraka pia.
Ni kweli mkuu nitajitahidi nimuongee apate mtaji ili aache kuomba pesa ndogo ndogo kwa watu
 
Jamani huku ni kutuchosha sasa! Yaani mtu wa hivyo unataka napo tukufundishe? Mimi nasema funika kombe mwanaharamu apite! Mrushie hiyo hela!
 
Baba yangu alikua ndiyo mtu pekee mwenye ahueni ya kimaisha kwao, wakati nakua niliona ndugu zake walivyokua wasumbufu, wana lawama na wako super entitled - nikajifunza kitu, watu wa namna hii hawatosheki hata uwasaidie vipi.

Kwangu nilivyoona mazoea yanataka kuzidi, nilibadili namba ya simu, ambao wanayo ni wale wa karibu sana na ni marufuku kutoa namba yangu kwa mtu, sitaki huu ujinga kabisa.
 
Niko mbioni kufanya hivi maana nimegeuzwa ATM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…