Huwa mnawashughulikiaje watoto wanaokuwa na tabia kama hii?

Tafuta mshkaji mmoja mtaani. Kila mtaa kuna mwana mwenye taarifa za kila mtu. Mpe pesa huyo mtu kama 10,000 tu akuletee taarifa za dogo. Haitamaliza hata wiki utajua mishe zote za dogo lako.
Kwakweli itabidi tufanye hivyo mkuu
 
Yupo hatua ya kubalehe; katika hatua hii anaweza kujiunga na makundi ambayo si mazuri kama hakupewa tahadhari katika umri huo.
 
Yupo hatua ya kubalehe; katika hatua hii anaweza kujiunga na makundi ambayo si mazuri kama hakupewa tahadhari katika umri huo.
Kwahiyo tunatakiwa kufanya nini ili kumsaidia asiangukie huko kwenye hayo makundi yasiyo mazuri
 
Kwakweli itabidi tufanye hivyo mkuu
Yaani hii mbinu ni kama unafanya diagnosis...majibu utakayoyapata hapo utajua pa kuanzia yaani polisi, kuzungumza naye, hospital kupima magonjwa au kwa mwana saikolojia. Kumbuka unaweza kumuitia polisi ndo ukamkosa kabisaa. Cha kwanza ni kujua unadili na nini? Fanya hivi kwanza kabla hujachukua hatua yoyote ya kivitendo.
 
Sawa, nmekuelewa mkuu Asante kwa ushauri mzurii 😊🙏🏼
 
tatizo ni kwamba baba tumemshirikisha na hafanyi lolote anasema tumuache tu kama alivyosema mwenyewe..na bad luck nyumbani hatuna mwanaume mwingne zaidi ya yeye na baba tu
Inawezekana dingi ana plan zake pia na hiyo kitu pia inamvuruga ila anajaribu kuitafutia ufumbuz sema labda hatak kwenda naye resi ndio maana anasema mwacheni.
Je ni mtoto wa kiume peke yake?
 
Kwahiyo tunatakiwa kufanya nini ili kumsaidia asiangukie huko kwenye hayo makundi yasiyo mazuri
Mzee ndio anatakiwa awape ushirikiano, ikishindikana, fuatilieni mienendo yake pamoja na marafiki anaokutana nao, alafu mkabizini kwa ndugu yenu wakiume, wajomba n.k wamrekebishe, iwe kwa viboko au kwa ushauri.
Kwa nyie wenyewe, itakuwa ngumu; na kama alishaanza kutumia bangi/dawa za kulevya ndio tatizo zaidi.​
 
Leteni mabinti cousins wakae hapo nyumbani atatulia huyo.

Wakishindwa hao kumfanya akae nyumbani muelewe kuwa ana kampani mbaya huko nje.
 
Pole sana huyo anapitia stress kali sana,uenda kushindana kwake ndani kukamnyima fursa ya kujifunza vitu vipya.
So uenda alivamia madege yasiyoliwa.
Kujua ugonjwa gani tuma picha za dawa alizotumia tutakuambia ni ugonjwa upi
 
Inawezekana dingi ana plan zake pia na hiyo kitu pia inamvuruga ila anajaribu kuitafutia ufumbuz sema labda hatak kwenda naye resi ndio maana anasema mwacheni.
Je ni mtoto wa kiume peke yake?
Ndio wakiume yupo pekeyake tu
 
Sawa nmekuelewa mkuu
 
Leteni mabinti cousins wakae hapo nyumbani atatulia huyo.

Wakishindwa hao kumfanya akae nyumbani muelewe kuwa ana kampani mbaya huko nje.
Sawa nmekuelewa, Asante kwa ushauri 😊🙏🏼
 
Pole sana huyo anapitia stress kali sana,uenda kushindana kwake ndani kukamnyima fursa ya kujifunza vitu vipya.
So uenda alivamia madege yasiyoliwa.
Kujua ugonjwa gani tuma picha za dawa alizotumia tutakuambia ni ugonjwa upi
Sawa Asante kwa ushauri
 
Tafuteni rafiki yake wa karibu atakuambieni ana shinda wapi au anashida gani.
Kujua rafiki yake nenda shule anayosoma omba ushirikiano na Mwalimu atakuambia swahiba wake ni nani,mtie ten swahiba wake atafunguka kuhusu maisha binafsi ya shule huyo ni mtu wa aina gani shuleni
Usikute ashavurugwa na mapenzi.
Umri wa 17 yupo kwenye stage ya ujuaji.
 
Akizingua wekeni hidden cctv camera mtap maongezi yake kwa phone mtapa jibu.
Umri huo Zaid ya stress za mapenzi hakuna zingine
 
Yuko likizo anasubiri kwenda form five mwezi ujao...marafiki zake pia tumeongea nao baadhi nao wanashangaa tu hawajui kakutwa na nini
 
Akizingua wekeni hidden cctv camera mtap maongezi yake kwa phone mtapa jibu.
Umri huo Zaid ya stress za mapenzi hakuna zingine
Inawezekana labda ana stress za mapenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…