Huwa nachukia sana 'Kelele' wakati wa Usiku na Asubuhi

Huwa nachukia sana 'Kelele' wakati wa Usiku na Asubuhi

AXIOM APEX VERBOSE

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
13,769
Reaction score
23,676
Nahisi nitakua nina tatizo la phonophobia.

Ninachukia sana sauti sana sana wakati wa asubuhi na nyakati za usiku yaan sipendi kabisa makelele mida hio.

Napenda sana sehemu yenye ukimya.

Napenda sana utulivu na kukaa sehemu iliyotulia muda mwingi nikiwa mwenyewe.

Sauti pekee inayonipa furaha na kunifanya nijihisi na kujisikia vizuri sana ni ile sauti ya maji yanayotiririka ndio naipenda kuisikia.

Napenda sana kutulia mwenyewe sehemu tulivu sana na km nikipata mtu wa kuzungumza nae basi asiwe zaidi ya mmoja.

Tukiwa wawili inatosha kuzungumza ila mazungumzo yetu yasiwe ya muda mrefu maana yakizidi sana pia nachoka nahitaji kua mwenyewe.

Sipendi kabisa kujiingiza kwenye mazungumzo ya watu wengi wenye makelele mengi ambao muda wote wanaongea mazungumzo yasiyo na maana au faida yoyote 'small-talk'. Inanichosha.

Sipendi makelele mengi hususani wakati wa usiku hua najipenda mwenyewe niwe sehemu tulivu zaidi na niwe peke yangu zaidi.
Au la niwe na mtu mmoja tu wa kuzungumza nae na asiwe muongeaji sana maana akiongea sana atanichosha.

Napenda kusikiliza kuliko kuongea maana kabla sijaongea hua najiuliza je hiki ninachotaka kukiongea nitakua nipo sahihi au nitakua sipo sahihi.

Napenda zaidi kuandika zaidi ya kuongea. Hua nafurahia zaidi kuandika kuliko kuongea maana nikiandika hata km nikikosea naweza kurekebisha nikaandika kitu sahihi ila najua nikiongea nimeongea siwezi kufuta kwa hio kwenye kuongea hua nakua makini sana hususani ninapoulizwa maswali nisiyopenda kuulizwa.

Siwezi kuongea na watu wengi zaidi ya mmoja kwa pamoja kwa muda mmoja na kwa muda mrefu hua inanichosha. Na muda mwingi nitaamua kujitenga na wengine wataniona tofauti wengine husema najisikia ila ndio nipo hivyo.
Siwezi kukaa na watu wengi muda mrefu.

Nachoka sababu napenda kua peke yangu. Wengine wananiona mpweke ila huo upweke wangu ndio sehemu ya furaha yangu.

Kuna muda hua nahitaji kua mwenyewe niwe peke yangu sehemu tulivu zaidi.

Nachukia kelele mara nyingi napenda niwe mwenyewe au niwe na mtu mmoja mkimya na asiependa kuzungumza sana.

Sipendi mtu mwenye mdomo mdomo mtu anaeongea sana hua ananichosha.
Napenda mtu anaependa kufanya kwa vitendo zaidi na sio kwa kuzungumza zaidi.

Sipendi kabisa wapiga makelele.
Kuna watu wao bila makelele makelele na bila kupiga kelele au kupigiwa ma
kelele hawasikii furaha.
Sipendi kelele.
 
Back
Top Bottom