Unaongea wewe ila Russia this time anajua kifuatacho ndio maana amekana kutaka kuvamia Ukraine na NATO wameshatoa msimamo kuwa Russia akiingiza mavuzi Ukraine atajutia kwa madhara atakayo yapata kutokana na uvamizi huo.... NATO wameshaanza kujiandaa na battle urusi karudisha Battery anadai hana mpango wala fikra za kuvamia Ukraine
Ndugu kitu ambacho napenda ufahamu ni kwamba Urusi Wala hakutangaza kama anataka kuivamia Ukraine.
Pili hakuna hata nchi moja ya NATO ambayo ipo tayari kuingia vitani na Urusi.Kwa sababu,
Vita Kati ya NATO na Urusi sio Vita ya bunduki,Bali ni Vita ya makombora,
Sasa nitajie nchi moja katika upande wa NATO ambayo iko tayari kutoweka katika ramani ya Dunia kwa sababu ya Ukraine tuu.?
Ambae Wala sio Mwanachama wao.
Lakini kaa ukijua linapokuja suala la ulinzi wa mipaka nchi yoyote haifanyi majaribio.sasa suala la NATo kutaka kulazimisha kujitanua ni sawa na kuruhusu adui avamie Urusi.So Urusi akiona hawaheshimu hali hiyo Wala hawezi kutishwa na NATo,yaani maana yake Yuko tayari kuingia vitani na yoyote.
Na hali hii sio kwa Urusi tu,hata Marekani au nchi yoyote haiko tayari kuhatarisha usalama wake.
Kwa hiyo ikifika wakati wa kuvamia atavamia.na nakuhakikishia NATO hawatakuwa tayari kuingia vitani na Urusi.Vuta ya NATO na Urusi na maangamizi na huenda ikawa na muonekano wa Vita ya tatu ya Dunia..
Nikupe mfano tu unafukiri kutakua na uvumilivu au subira ya kutumia silaha za maangamizi,hamna Hawa watu hawatachelewa kutumia silaha kubwa kwa sababu za kutoaminiana kwamba labda ataniwahi,labda ataniwahi mwisho wanarushiana makombora mazitomazito ya maangamizi.
Sasa nitajie vi nchi kama uingereza ambavyo ni vidogo kwa eneo vinahutaji makombora mangapi kuvifuta katika uso wa duniaa?
Je ni nchi gani ulaya iko tayari kwa hilo?
Kisa Ukraine na sbabu yenyewe ni interest za Marekani kutaka kujitanua Kijeshi?