Huwezi amini Wazungu ndio wanalisha Hoteli za Kitalii Tanzania, Hii aibu kuu



Mimi silaumu serikali kwenye hili vijana nao wajiongeze na kuulizia mbinu za kuingia kwenye kilimo. Tupunguze tabia za kulalama
 
Support kama mikopo, vibali, mbolea, pembejeo za bei nafuu, vibali vya kuuza nje ya nchi, pia kuna ukiritimba ni mkubwa.

Soko la uhakika ni changamoto. Uende wewe, mzungu, mhindi au mwarabu kuomba kuwa supply wa hoteli wenye utazungushwa kuliko wenzako.

Sisemi haizewekani, inawezekana lakini usumbufu ni mkubwa.
 
Sawa inawezekana ikawa ni nzuri je wanaweka yanayotakiwa au ni yeyote?
 
Si hata sasa serikalini majitu yanaiba pesa za miradi, maendeleo yanakwama halafu wanalalamika. Ripoti ya CAG imetolewa sasa komaeni hawa wezi washikwe, yamekaa kimya yanakenua kenua meno, sasa mnataka sijui askari ndio waandamane kwa niaba ya raia.
Wakitumbuliwa utasikia sheria zifuatwe jamani vichwa hivi sijui tumebeba ubongo au matope, Kama ile meli maarufu ya meli ya Magufuli ya samaki, walichokifanya wakaanza kukata eti vyuma chakavu mpaka meli sijui ilienda wapi, eti wakaanza kulalamikia waziri aliyekamata.
 

Kuna mahali nilienda mkulima ni mtu anayeogopwa kuliko mtu yeyote, maana ndio anayeweza control supply na demand ya chakula eneo hilo

Naomba nikuchek PM
 

Wazungu wanakopesheka na mabenki kwavile waaminifu!! Wabongo wengi sio waaminifu; wanakwenda kopa benki halafu hawalipi madeni mwisho wake wanatumia janja janja yakwenda kushitaki benki Mahakamani na huko wanahonga na kushinda kesi na benki zinakula hasara.
This is true kwani nina ushahidi wa Mzee mmoja ana shamba huko West Kilimanjaro alichukua Mkopo benki halafu akashindwa kulipa kwani ule mkopo hakuutumia kama walivyokubaliana na mwishowe akawashitaki benki ili asilipe hilo deni.!
 
Mkuu,Nimependa andiko lako Swali langu kwako ni Je?Huko kwenye Mashamba vibarua ni Wazungu?Je Haya mazao uliyoweka kwenye Picha Wabongo hawalimi?Je huko kwenye Mahoteli kote ni wazungu ndio wanaohudumia?Mwisho Je Unataka wafukuzwe hao wzungu ili wabongo tuhudumie hizo hotel?

Binafsi nafikiri Tatizo letu "Tunalalamika Sana lakini hata tukipewa Fursa hatutatumia bado Tutalalamika" Ni desturi ya watu wavivu na wazembe kutafuta Visingizio.Tuambiane Tu ukweli kwamba Sisi kuweza kufanya Biashara kwa viwango bado na hata pale ambapo tunatakiwa tuzingatie viwango kama vya TBS etc tunaona tunaonewa Sasa katika hali kama hii Ni hotel gani ya Nyota Kadhaa ambayo inawalisha watu matajiri duniani itanunua bidhaa bila kujiridhisha kwamba Mkulima anazingatia Viwango vya kilimo?

Tunaweza kufika huko kwa wazungu ila kwanza tuache kulalamika na badala yake tuchukue hatua.
 

Sio wazungu, ni capital fala wewe, uache ubaguzi, Tanzania's:

1. Dont have capitals.
2. Wamiliki wa hizo Hotel wengi wazungu wanapeana biashara.

Tatizo la Tanzania ni sera mbaya za serikali, na uongozi wa hovyo wa CCM.
 

Hakuna product hapo ambazo halimi Mtanzania, Tanzania's are very super hardworking, basi tu sera mbaya za serikali, na ubaguzi wa ki Biashara.
 
Aiseee nazani uko nje ya Maada, nazungumzia kulisha ku supply, Watanzania tunapenda kutafuta sababu sana, Kenya Hoteli za kule zina lishwa na Wakenya,
 
Mimi umeona nailaumu Serikali? Sikiliza nauliza kwa nini hatuwezi? Si kwamba Watanzania hawalimi wanalima in small scale sana, hata hao ninao wataja wakizidia na Oda huwa wana ongeza za wabongo wale ambao wana quality, shida sio kulalamika wala nini shida ni kwamba kwa nini hatuwezi? Hapa Serikali haihusiki hata chembe,
 
Umeweka ushahidi wa picha, delete basi?
Hio ni picha moja sikutaka kuja humu picha ninazo nyingi sana, kwani unataka vipi? Na sijasema Watanzania hawalimi, wanalima sana na hata hao Wazungu Oda zikiwa kubwa wanachukua kwa Watanzania pia so?

Sidhani kama umeelewa bandiko langu, ni kwamba Watanzania hii kazi ya ku feed Mahoteli ilipaswa kuwa yetu kwa asilimia 90 na sio ya Wageni,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…