Huwezi nishawishi Nyerere alikuwa Rais bora

Aliondoka madarakani alipozima mazima, ila 85 mpaka 98 bado aliwashwa washwa kwa sana tu
Hakuna kitu Kama hicho. Mwinyi si ndio alikuja na sera tofauti na nyerere. Mkapa ndio kabisaa yeye sera zake zikawa pia tofauti
Tatizo la Tanzania Ni tatizo la nchi nyingi za Africa, huko napo Wana nyerere? Kenya nchi iliyokua na sera tofauti kabisa kwa miaka yote toka uhuru, bado wamekwama
 
Tatizo ni sisi wenyewe tumejawa na hulka mbovu za ubinafsi, ufisadi kila taasisi.

Nyerere ni aibu hata kumzungumzia wakati huu ripoti ya CAG ikituumbua, ni madudu matupu yanafanyika kila mahali.
Ndio hapo sasa, Ni mtu mjinga tu ndio atasema tumeshindwa kuwa kama nchi zilizoendelea Europe sababu ya nyerere. Tatizo la Tanzania ni tatizo la nchi nyingi Africa. Uganda wamekwama, Kenya wamekwama, Malawi wamakwama, Zambia, Sudan, Congo nk. Huko kote wamekwama, Sasa sijui huko napo nyerere alikua raisi
 
Dictator.
 
Kwani we ni nani hadi watu watumie nguvu, muda na akili zao kukuaminisha? Kama huamini wewe haipunguzi au kuondoa maana kwa wengine wanao amini kuwa ni kiongozi bora. Vaa kobazi zako kanywe kahawa na alkasusu.
 
Yeye mwenyewe alikuwa mdini
Sawa. Kwa yeyote aliyeaminishwa na historia (histo-hisia) ya mwandishi wa Kimanyema (ambaye ana personal grudges against Nyerere) atasema hivyo.
Ila wapenda ukwelii tunajua Nyerere hakuwa mdini na alijitahidi sana kupromote usawa kwa wote.
 
Sawa. Kwa yeyote aliyeaminishwa na historia (histo-hisia) ya mwandishi wa Kimanyema (ambaye ana personal grudges against Nyerere) atasema hivyo.
Ila wapenda ukwelii tunajua Nyerere hakuwa mdini na alijitahidi sana kupromote usawa kwa wote.
Alikuwa mdini bana acha kutuzuga hapa, na mpaka kesho bado udini upo ila ipo siku utaondoka tu, ngoja kwanza watoto wasome
 
Asante Countrywide, kwa mara ya kwanza umeaongea hoja nzito na za msingi.
Kizazi cha leo, tunalaumu mtu ambae hayupo duniani miaka 25 iliyopita, achilia mbali kutokuwa madarakani miaka karibia 40.

Sisi ni mazuzu
 
Nyerere Kama binadamu mwingine yoyote yule, alikuwa ana mazuri yake lakini pia alikuwa ana mabaya yake, ingawaje kwa kiasi kikubwa mapungufu yake mengi yalikuwa yanavumilika ukimlinganisha na wenzake wengine wote waliomfutia.
Nikikumbuka enzi za utawala wake subuni za kuogea e.g Rexona,lifebuoy zilikuwa dili,alikuwa hana mipango mizuri ya kiuchumi
 
Kwani wewe ni nani hadi "ushawishiwe", na kwa faida ipi hasa!

Akili zilizooza ni hizo za kwako na watu wenye fikra kama hizo za kwako ambazo haziwezi kufikiri bila ya kuendeshwa na watu wengine kwa niaba yako.

Nyerere hayupo miaka mingi; lakini bado mnahangaishwa na kivuli chake; hivi hamuoni kuwa mmepungukiwa akili?
WaTanzania si hawa hapa, tumieni muda wenu nanyi kuwaonyesha kuwa nyinyi ndio bora zaidi ya mwingine yeyote; hata huyo Nyerere. Ni kipi kinacho wafanya msifanye hivyo?
Kupambana na kivuli cha Nyerere kamwe hakuwezi kuwa ndiyo njia nzuri ya kuwafanya waTanzania wawakubali nyinyi.
 
Ndio maana naamini wengi wanaotoa michango katika huu uzi ni watoto wa miaka ya 2000, wamezaliwa na kukuta Nyerere keshafariki dunia.

Ujinga wetu mwingi chanzo ni ubinafsi wa kila mtu haswa anapopata nafasi katika taasisi au shirika fulani.
 
Ebu punguza ujinga!
Nyerere alizaliwa akaishi... Akalitumikia Taifa lake kwa jinsi alivyoweza.
Mengi maovu yanayoendela hata yeye binafsi aliyaona na aliyakemea!
Binafsi waTanzania wengi hadi leo hawajui ni kwanini uhuru ulipatikana December 9, 961.
Wengi kama wewe wanafikiri ni jukumu la viongozi kuwaletea maendeleo!

Nyerere lived and did whatever he did. Swali ni je wananchi wao wamefanya Nini? Au wamebaki kuwa machawa na wapiga Makofi? Je, Hilo nalo ni tatizo la Nyerere?
 
Wajinga hawa mabwana wadogo kitu kizuri chanzo ni wao ila mabaya yote lazima anyoshewe mtu vidole, ni hulka za kibinafsi.
 
Asante Countrywide, kwa mara ya kwanza umeaongea hoja nzito na za msingi.
Kizazi cha leo, tunalaumu mtu ambae hayupo duniani miaka 25 iliyopita, achilia mbali kutokuwa madarakani miaka karibia 40.

Sisi ni mazuzu
Ni wajinga tu ambao hawajui tatizo halisi ni lipi.
 
Anakwambia raisi akishateuliwa anaapa kwa imani yake ili awajibishwe ilihali katiba aliyoiandaa na masela zake inamlinda huyo huyo raisi asiwajibishwe popote...Ni wajinga tu wenye upeo mdogo ndio watakaomuona alikua na akili sana kumbe alikua tapeli.
Ukiyasoma maneno yako na kuyaelewa, hapo ndipo utakapoona jinsi ulivyo kilaza kweli kweli.

"Anakwambia (sijui nani huyo?) raisi akishateuliwa anaapa kwa imani yake"; nimeelewa "imani ya huyo rais aliye teuliwa), ili "..awajibishwe..." kwa imani yake mwenyewe kama atakiuka hayo anayo apa kuyafuata.

Halafu unajitoa akili hapo hapo:"..ilhali katiba aliyo iandaa na masela zake inamlinda huyo huyo rais asiwajibishwe popote..."
Maana yako hapa ni kwamba Nyerere huyo huyo ndiye hao marais wengine wote waliomfuatia baada ya yeye.
Na kwamba hawa marais hata hizo imani zao hawaoni kuwa zina thamani kubwa zaidi ya hiyo "katiba" aliyo itengeneza Nyerere! Huoni kuwa mnapambana na kivuli cha Nyerere ambacho uwezo wa kukifuta hamna?

Wewe utakuwa ni mtu mwenye kufikiri sawasawa au ni msukule tu wa aina fulani ulio fundishwa kutapika maneno bila ya kutafakari maana yake?
 
Au sio... Kwahiyo unatudhalau mkuu kwamba sisi misukule na akili zetu zimeoza... haya bhana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…