Huwezi Pinga Kuwa Dini (madhehebu yote) yamegeuka kuwa biashara zinangonya waumini. Kama una hoja utasikilizwa na kujibiwa

Tatizo ni watu sio maandiko
Mfano kwenye Biblia kuna maandiko mengi yanaonya watu wasipende pesa na hata vitu vingi vya kimwili
Badala yake inawasihii watu waridhike na mahitaji muhimu na kuwa na maoni yanayofaa kuelekea pesa.

Ila watu ndio hawataki na wanapenda vitu rahisi rahisi hapo ndio inakuwa rahisi kudanganywa.

Swala ni je utendaje wao unapatana na Biblia inavyosema au wanapingana nayo waziwazi
 
Sadaka ya kweli mmefundishwa kwenye biblia mnajizima data tu, we kama ulinusurika chukua hiyo 300k pelekea yatima, wagonjwa na wafungwa gerezani
 
Zamani tulikuwa tunapata farijiko sana ukienda kanisani saivi tunapata karaha na kuabishwa wale ambao hatutoi michango.
 
Dizain yako kuandika uwongo jambo lionekane zuri ni chap tu,hakuna mtu labda awe mwendawazimu atauza roho yake kwa issue ndogo kama hiyo.

Muulize mleta mada akikaa kimya bila kutoa hiyo anayoiita michango kuna mtu anamfata kumuamsha akatoe?
Mzeebaba sijaandika uongo. Mimi ni mkristo safi kabisa na huwa najisikia vibaya sana ninapoona mtu anaslim...ingekuwa ni lazima nikuonyeshe huyo jamaa aliyeslim ningefanya hivo......hata mi nilimuona ni mtu wa ovyo sana kubadili dini
 
Mkuu ulisema sadaka ni Siri na kubaliana nawewe lakini vipi michango inayopangwa kabisa kwamba Kila mtu na gori lake?

Sadaka ni hiari na jua lakini michango wanakwambia ni lazima Ili kazi ya Mungu iende!
 
.
 
Mzeebaba sijaandika uongo. Mimi ni mkristo safi kabisa na huwa najisikia vibaya sana ninapoona mtu anaslim...ingekuwa ni lazima nikuonyeshe huyo jamaa aliyeslim ningefanya hivo......hata mi nilimuona ni mtu wa ovyo sana kubadili dini
Sijakuuliza dini yako wala unavyojisikia mtu akibadilika nilichokazia mimi ni mpumbavu tu kiimani ataikana imani yake eti kwa sababu ya kitu mchango kitu ambacho ni hiyari kutoa au kutotoa.
 
Zamani tulikuwa tunapata farijiko sana ukienda kanisani saivi tunapata karaha na kuabishwa wale ambao hatutoi michango.
Zamani ulikuwa unapigwa kisirisiri na huku unapulizwapulizwa, siku hizi unapigwa kiwaziwazi huku unazodolewa.

Sasa hapo swali ni.

Je,

Unapenda kupigwa kisirisiri huku unapulizwapulizwa mpaka hujui kwamba unapigwa au kupigwa kiwaziwazi huku unazodolewa mpaka unajua kuwa unapigwa?
 
Shida yetu ukisema ukweli unaonekana eti unataka kuasi kanisa kimsingi unakuwa na hoja na unatakiwa usikilizwe na kujibiwa vyema. Mnashikana mashati halafu Hela zinaliwa ovyo tu. Ukweli michango Kwa Sasa inaogopesha sana.
Utashangaa pesa za kanisa mwamposa anaenda kujenga hotel na inakuwa yake binafsi na hata hakuna wa kuhoji
 
Jibu wanapingana nayo wazi wazi maana hakuna sehemu yoyote imeruhusu mchangaji anunuliwe gari.
 
Mkuu wasiamke kwanza ,bado mimi ndio nipo kitabu ya hosea najisomea kwanza nije kuwabamiza kisawasawa.
 
Kuna kanisa niliacha kusali baada ya kutakiwa kuchanga hela ya kununua injini ya gari la Mchungaji. Yaani natoka kanisani tumetoa sadaka na tumechanga michango kibao. Tunakuja kwenye group tunaambiwa tena tuchange?! Nikaona huu ni ufala.
Mahubiri mengi ya pasta ilikuwa mimi nimefanya hiki kanisani, mimi nimefanya hivi hapa kanisani- Umimi mwingi. Wakati ukiangalia vitu almost michango ya waumini. Kwa nini waumini hawapewi credit?
 
Mkuu samahani ukiachana na comments nyingine katika huu uzi sijataka kuzisoma zaidi ya ulichoandika wewe tu ila nina maswali kwako naomba unisaidie kuyajibu :

1. Unaamini katika Mungu na utatu mtakatifu?

2. Je unafahamu mwanzo wa madhehebu?

3. Unaamini katika kitabu cha Henoko?

Hayo tu.
 
Mzeebaba sijaandika uongo. Mimi ni mkristo safi kabisa na huwa najisikia vibaya sana ninapoona mtu anaslim...ingekuwa ni lazima nikuonyeshe huyo jamaa aliyeslim ningefanya hivo......hata mi nilimuona ni mtu wa ovyo sana kubadili dini
Huyu jamaa yetu yeye anadhani tunapopinga huu ujasiriamali unaofanywa makanisani basi anaona sisi ni waasi yaani tukubali tu kubuluzwa.

Ajue kwamba hata wakina Martine Luther,John Huss walikuwa wanahoji vitu kama Hivi tunavyo hoji hapa.

Kwani ni uongo?
 
Ndo tuko hapa kuamshana Sasa tuanze kupinga hizi biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…