Huwezi Pinga Kuwa Dini (madhehebu yote) yamegeuka kuwa biashara zinangonya waumini. Kama una hoja utasikilizwa na kujibiwa

Huwezi Pinga Kuwa Dini (madhehebu yote) yamegeuka kuwa biashara zinangonya waumini. Kama una hoja utasikilizwa na kujibiwa

Tatizo ni watu sio maandiko
Mfano kwenye Biblia kuna maandiko mengi yanaonya watu wasipende pesa na hata vitu vingi vya kimwili
Badala yake inawasihii watu waridhike na mahitaji muhimu na kuwa na maoni yanayofaa kuelekea pesa.

Ila watu ndio hawataki na wanapenda vitu rahisi rahisi hapo ndio inakuwa rahisi kudanganywa.

Swala ni je utendaje wao unapatana na Biblia inavyosema au wanapingana nayo waziwazi
 
Kwenye uislamu hizi mambo hakuna nakumbuka kuna kioindi Nilipata ajali nukasalimika nilienda kutoa sadaka ya Shukrani kanisani 300k sijui ile sadaka ilifanyiwa nini ?

Hakika tuzinduke Vijana hizi dini hasa ukristo kwa sasa zinaonekana ni mawazo ya binadamu kutengeneza pesa tu.
Sadaka ya kweli mmefundishwa kwenye biblia mnajizima data tu, we kama ulinusurika chukua hiyo 300k pelekea yatima, wagonjwa na wafungwa gerezani
 
Nakwambia hivi, dini zilikuwa biashara za kumuuza Mungu ambaye hayupo tangu awali.

Mlikuwa hamjaelewa tu na mpaka sasa mkipinga dini kugeuka biashara wakati tangu zinaanza zilikuwa biashara, mnajionesha ujinga tu.

Kilichobadilika ni wingi wa watu kuzidi, vurugu kuzidi, uroho kuzidi, biashara kuzidi, lakini dini ni biashara tangu mwanzo.
Zamani tulikuwa tunapata farijiko sana ukienda kanisani saivi tunapata karaha na kuabishwa wale ambao hatutoi michango.
 
Dizain yako kuandika uwongo jambo lionekane zuri ni chap tu,hakuna mtu labda awe mwendawazimu atauza roho yake kwa issue ndogo kama hiyo.

Muulize mleta mada akikaa kimya bila kutoa hiyo anayoiita michango kuna mtu anamfata kumuamsha akatoe?
Mzeebaba sijaandika uongo. Mimi ni mkristo safi kabisa na huwa najisikia vibaya sana ninapoona mtu anaslim...ingekuwa ni lazima nikuonyeshe huyo jamaa aliyeslim ningefanya hivo......hata mi nilimuona ni mtu wa ovyo sana kubadili dini
 
Wewe bro imani yako imekufa,kama Kanisani unaenda uonekane umeenda lakini huendi kwa sababu nafsi imejitakia kwenda na sadaka unatoa uonekane which is kiimani unapata hasara tu sadaka yoyote inatakiwa kununewa sasa wewe kwa majuto haya nafasi hiyo huipati.

Hela haina mshirika haupo kwenye mfuko wa W wala B wala X ili na wewe ulazimike kutoa kwanini usisimame wewe kama wewe kwamba huna?watakulazimisha?hata kama juzi ulitoa ndiyo leo huna na ibaki hivyo huna hata kama unazo mfukoni utatoa kesho,kuwa na msimamo kiimani ukitoa uonekane unapata tu hasara
Mkuu ulisema sadaka ni Siri na kubaliana nawewe lakini vipi michango inayopangwa kabisa kwamba Kila mtu na gori lake?

Sadaka ni hiari na jua lakini michango wanakwambia ni lazima Ili kazi ya Mungu iende!
 
Wewe bro imani yako imekufa,kama Kanisani unaenda uonekane umeenda lakini huendi kwa sababu nafsi imejitakia kwenda na sadaka unatoa uonekane which is kiimani unapata hasara tu sadaka yoyote inatakiwa kununewa sasa wewe kwa majuto haya nafasi hiyo huipati.

Hela haina mshirika haupo kwenye mfuko wa W wala B wala X ili na wewe ulazimike kutoa kwanini usisimame wewe kama wewe kwamba huna?watakulazimisha?hata kama juzi ulitoa ndiyo leo huna na ibaki hivyo huna hata kama unazo mfukoni utatoa kesho,kuwa na msimamo kiimani ukitoa uonekane unapata tu hasara
.
 
Mzeebaba sijaandika uongo. Mimi ni mkristo safi kabisa na huwa najisikia vibaya sana ninapoona mtu anaslim...ingekuwa ni lazima nikuonyeshe huyo jamaa aliyeslim ningefanya hivo......hata mi nilimuona ni mtu wa ovyo sana kubadili dini
Sijakuuliza dini yako wala unavyojisikia mtu akibadilika nilichokazia mimi ni mpumbavu tu kiimani ataikana imani yake eti kwa sababu ya kitu mchango kitu ambacho ni hiyari kutoa au kutotoa.
 
Zamani tulikuwa tunapata farijiko sana ukienda kanisani saivi tunapata karaha na kuabishwa wale ambao hatutoi michango.
Zamani ulikuwa unapigwa kisirisiri na huku unapulizwapulizwa, siku hizi unapigwa kiwaziwazi huku unazodolewa.

Sasa hapo swali ni.

Je,

Unapenda kupigwa kisirisiri huku unapulizwapulizwa mpaka hujui kwamba unapigwa au kupigwa kiwaziwazi huku unazodolewa mpaka unajua kuwa unapigwa?
 
Shida yetu ukisema ukweli unaonekana eti unataka kuasi kanisa kimsingi unakuwa na hoja na unatakiwa usikilizwe na kujibiwa vyema. Mnashikana mashati halafu Hela zinaliwa ovyo tu. Ukweli michango Kwa Sasa inaogopesha sana.
Utashangaa pesa za kanisa mwamposa anaenda kujenga hotel na inakuwa yake binafsi na hata hakuna wa kuhoji
 
Tatizo ni watu sio maandiko
Mfano kwenye Biblia kuna maandiko mengi yanaonya watu wasipende pesa na hata vitu vingi vya kimwili
Badala yake inawasihii watu waridhike na mahitaji muhimu na kuwa na maoni yanayofaa kuelekea pesa.

Ila watu ndio hawataki na wanapenda vitu rahisi rahisi hapo ndio inakuwa rahisi kudanganywa.

Swala ni je utendaje wao unapatana na Biblia inavyosema au wanapingana nayo waziwazi
Jibu wanapingana nayo wazi wazi maana hakuna sehemu yoyote imeruhusu mchangaji anunuliwe gari.
 
Christianity is a business, Jesus is the Product, Church members are the Customers, Church leaders are the Beneficiaries.

Ukristo ni biashara, Yesu ni Bidhaa, Waumini ni Wateja, Viongozi wa kanisa ni Wanufaika.

Amkeni nyie mtaibiwa hadi lini?

Wake up you people!

Jikomboeni kutoka kwenye utumwa wa hizi imani za kidini.
Mkuu wasiamke kwanza ,bado mimi ndio nipo kitabu ya hosea najisomea kwanza nije kuwabamiza kisawasawa.
 
Kuna kanisa niliacha kusali baada ya kutakiwa kuchanga hela ya kununua injini ya gari la Mchungaji. Yaani natoka kanisani tumetoa sadaka na tumechanga michango kibao. Tunakuja kwenye group tunaambiwa tena tuchange?! Nikaona huu ni ufala.
Mahubiri mengi ya pasta ilikuwa mimi nimefanya hiki kanisani, mimi nimefanya hivi hapa kanisani- Umimi mwingi. Wakati ukiangalia vitu almost michango ya waumini. Kwa nini waumini hawapewi credit?
 
Mkuu samahani ukiachana na comments nyingine katika huu uzi sijataka kuzisoma zaidi ya ulichoandika wewe tu ila nina maswali kwako naomba unisaidie kuyajibu :

1. Unaamini katika Mungu na utatu mtakatifu?

2. Je unafahamu mwanzo wa madhehebu?

3. Unaamini katika kitabu cha Henoko?

Hayo tu.
 
Mzeebaba sijaandika uongo. Mimi ni mkristo safi kabisa na huwa najisikia vibaya sana ninapoona mtu anaslim...ingekuwa ni lazima nikuonyeshe huyo jamaa aliyeslim ningefanya hivo......hata mi nilimuona ni mtu wa ovyo sana kubadili dini
Huyu jamaa yetu yeye anadhani tunapopinga huu ujasiriamali unaofanywa makanisani basi anaona sisi ni waasi yaani tukubali tu kubuluzwa.

Ajue kwamba hata wakina Martine Luther,John Huss walikuwa wanahoji vitu kama Hivi tunavyo hoji hapa.

Kwani ni uongo?
 
Zamani ulikuwa unapigwa kisirisiri na huku unapulizwapulizwa, siku hizi unapigwa kiwaziwazi huku unazodolewa.

Sasa hapo swali ni.

Je,

Unapenda kupigwa kisirisiri huku unapulizwapulizwa mpaka hujui kwamba unapigwa au kupigwa kiwaziwazi huku unazodolewa mpaka unajua kuwa unapigwa?
Ndo tuko hapa kuamshana Sasa tuanze kupinga hizi biashara
 
Back
Top Bottom