Huyu aliyebandika mabango ya Imani Upendo Miujiza ya mkutano wa dini Dar, achukuliwe hatua

Huyu aliyebandika mabango ya Imani Upendo Miujiza ya mkutano wa dini Dar, achukuliwe hatua

Tuache ushabiki wa kidini this is too much ubandikaji gani ule wa matangazo
Nadhani mpaka kipofu ataona hilo tangazo. Nilipita JANGWANI juzi nikakuta kikundi cha watu chini na ndoo za gundi na hayo mapeperushi nikajisemea wapuuzi kwenye upuuzi wao...

Mimi kama mkuu wa mkoa mstaafu nawaamuru mkutano wao wa dini utakapo isha waende wakasafishe kuta za watu

Ova
 
Matangazo yametapakaa Dar kuanzia kwenye nguzo za umeme, madaraja..mitaro n.k

Anapaswa kushughulikiwa na kuamriwa kusafisha miundombinu aliyoichafua.

=========

View attachment 1943336

View attachment 1943337
Uzio wa Yapi Merkez, eneo la Raha Leo-Dar
Acha ubaguzi!. Aliyebandika hayo matangazo atakuwa ni mtanzania mwenzako ambaye amelipwa kufanya kazi hiyo, Inaonekana kwamba yeye haoni kama ni uchafu.
 
Matapeli wakibandika matangazo ya kuibia watu kama freemasons, waganga matapeli sijui bibi bani na nguvu za kiume haupigi kelele ila neno la Mungu unaona kero
 
Cha muhimu akimaliza wayatoe maana ni too much! Yani imekuwa kero sasa! Ila ndo hivyo kafaulu kucapture attention zetu, kila mtu sasa anajua kuna mkutano wa injili
 
Vitu vingine mnavyolalanika ni kiboko matangazo ya dini ya madhara gani mnataka kuishi Dunia gani..
Lakini yalivyowekwa ni uchafu ,mwisho wa siku yakinyofoka yanajaa chini ,kwanza atajazaje vile mbona anatumie vibaya sadaka za waumini
 
Mkuu ungekuwa na gari hayo yote yasingekusumbua kuzurura na miguu kushangaa mabango

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Tender ya mabango ilikuwa kanzia Mlandizi mpaka Mbagala. Msela akala "payment in advance" . Akasubiri giza. Halafu: "Mission accomplished"!
 
Back
Top Bottom