Huyu Binti Kwa kusema hivi anaweza kukamatwa?

Huyu Binti Kwa kusema hivi anaweza kukamatwa?

Dunia ya sasa siyo ya zamani..

Juzi kuna gen z mmoja nilikuwa naongea naye, aisee mambo aliyokuwa anaongea, mambo anayoyajua, anavyochambua mambo, nikajisemea hapa kweli tuko kizazi kingine kabisaaa..

Mpaka ilibidi sasa nimuambie umeshaiva, karibu Jamiiforums[emoji3][emoji3]
Kwanini ulimkaribisha JF? Kwamba JF kuna watu wenye upeo mkubwa kama yeye? Hawa hawa wakina Lucas Mwashamba
 
Wakandarasi Machawa walitaka kumnunulia Helkopita kwa ajili ya kufanyia Kampeni. Nchi ina watu wajinga hii acha tu. Huku hela Mnadai kama Wakandarasi huku kuna kikundi cha Machawa kinajipendekeza kununua Helkopita.
Wapuuzi sana tulichana sana kwenye magroup leo wenyewe wametulia tu...wametangaza kazi za barabara wamezigawa ni za labour base zionekane nyingi, walufanya hivyo mwaka jana lata hivyo bado wanadai
 
Magufuli ndiye aliye yapa kasi zaidi, zama za nyuma matukio hao hayakuwa yakilenga wakosoaji wa kisiasa kuwapoteza kabisa kama zama za magufuli ilivyo kuwa na zama za huyu mama
Hizo cheche za wakati ule ndizo zilizozalisha huo moto ! 😳 !
 
Je, Ni sawa kumtoa kafara yule mtoto? Kwanini sisi wakubwa tunaojua hatari tusijirekodi wenyewe na kujitoa muhanga?
Acha unafiki... Sisi tunaotumia majina halisi na kuikosoa CCM na Serikali ni lini mliwaza hatima yetu?

Mara ngapi mnashadadia yatupate ya kutupata?
 
Acha unafiki... Sisi tunaotumia majina halisi na kuikosoa CCM na Serikali ni lini mliwaza hatima yetu?

Mara ngapi mnashadadia yatupate ya kutupata?
Wewe ni mtu mzima mwenye elimu kubwa kuliko yule msichana.
Pia una taarifa sahihi za matukio yanayo weza kukupata hivyo tunaamini umechagua mwenyewe kujitoa muhanga(sadaka) ukiwa na ufahamu wako.
Kwanini binti mdogo (under 18) akichagua mwenyewe kufanya ngono tunasema amebakwa na mwenzie?
Unaweza kusema kitu kama hicho kwa yule binti?
Pia nilikuwa nahoji ushujaa wa yule aliyenishambulia upo wapi?
Mbona kajificha?
 
Wewe ni mtu mzima mwenye elimu kubwa kuliko yule msichana.
Pia una taarifa sahihi za matukio yanayo weza kukupata hivyo tunaamini umechagua mwenyewe kujitoa muhanga(sadaka) ukiwa na ufahamu wako.
Unaweza kusema kitu kama hicho kwa yule binti?
Pia nilikuwa nahoji ushujaa wa yule aliyenishambulia upo wapi?
Mbona kajificha?
Utu uzima wangu haufanyi uhai wangu kuwa na thamani tofauti na wa yule Binti.

Halafu ni Kwa nini mnatutisha sisi mnaodhani tutadhuriwa badala ya kuwashambulia wale wanaotaka kututendea mabaya?
 
Utu uzima wangu haufanyi uhai wangu kuwa na thamani tofauti na wa yule Binti.

Halafu ni Kwa nini mnatutisha sisi mnaodhani tutadhuriwa badala ya kuwashambulia wale wanaotaka kututendea mabaya?
Umechagua mwenyewe kama vile alivyo chagua Mandela, Tundu Lissu, Polepole au Gwajima.
It's your consent, you are prepared for the outcomes. Ready to face the consequences of your actions, can you say the same thing to a young girl like that?
 
Hivi kwa nini mnataka kumfanya yule Binti hajitambui na kurekodiwa kwake hakujua madhara yake?

Nani ameishi na yule Binti kwa maisha ya kila Siku hadi kufanya hitimisho kuwa alichofanya hajui "implications" zake?

Halafu narudia tena, Kwa nini tunaona watenda mabaya wana haki ya kutenda mabaya huku watendewa mabaya tunaona ni watu wanaojitakia?
 
Moja hili halisemwi wazi: Wanawake wengi hawapendi kuongozwa na mwanamke!
 
Nipe ushahidi wa na sababu inayo kufanya uone samia hakubaliki na Magufuli alikuwa akikubalika.
Sijajua unataka nikupe ushahidi wa aina gani ila maongezi ya wananchi kiasi kikubwa huonyesha kutomkubali Samia, hadi leo kila wanapokosoa huu uongozi wa Samia hurejea kumtaja Magufuli kipi alisema au kufanya ambapo ni tofauti na mambo yalivyo katika uongozi huu wa Samia.

Kipindi cha Magufuli wananchi walikuwa wanafuatilia hotuba za Magufuli wasikie anasema nini kuna watu hadi sasa wana clip Magufuli, ila leo hii watu hawataki hata kumsikiliza Samia na hasa wanawake wakimuona hata kwenye taarifa ya habari wanabadili na channel.
 
Back
Top Bottom