Huyu Binti Kwa kusema hivi anaweza kukamatwa?

Duh! Yani unaniita sina akili kwa kosa lako mwenyewe la kushindwa kuelewa nilichosema, kwanini usingetangulia kuuuliza kwanza ili upate kuelewa?
Mkuu,

Uongozi wa Kikwete unaukumbuka vema lakini?

Ukiondoa Demokrasia iliyokuwepo kwa uwalau,

Mambo mengine ilikuwa ovyo tupu, rushwa, madawa ya kulevya, neno Mafisadi kwa mara ya kwanza lilitokea katika kipindi chake, na kiukweli, ncgi ilitafunwa haswaa

IPTL, Richmond, Escrow n.k ni yeye huyo unayesema wa kuigwa
 
Watamchagua nani mwingine?
 
Umemaliza kila kitu mkuu.
 
Suala la kiongozi kuwa bora au kutokuwa bora hasa katika nchi kama yetu huwa ni mtazamo wa mtu binafisi kutokana na alivyo nufaika au kuathirika kipindi cha uongozi wake.
Magufuri alikuwa anapendwa na mamilioni ya watu kwa sababu zao na pia alikuwa anachukiwa na mamilioni ya watu kwa sababu zao na vilevile kwa huyu mama.
Mfano leo hii huwezi kumuambia mkulima wa kahawa kuwa Magufuri alikuwa bora kuliko samia hali ya kuwa kipindi cha Magufuri alikuwa analazimishwa kuuza kahawa zake kwa mkopo wa sh 1000 kwa kg, hali yakuwa sasa hivi kwa huyu mama anauza kahawa yake kwa sh 5000 kg kwa keshi.
Au huwezi kumuambia muhitimu kuwa Magufuri ni bora kuliko Samia alikataa kumpa ajira na akaja kupewa na samia.

Kwa hiyo suala la kutokuwa bora kwako haimaanishi sio bora kwa wengine.
 
Sasa huo utawala unafanana na utawala wa nani kati Magu na Samia?
 
Kwani aliye kwambia kuwa samia hakubaliki ni nani?
Magufuli alikuwa ana kubalika kwa mamilioni ya watu kwa sababu zao na pia kuna walio kuwa wanamchukia kwa sababu zao na kwa samia hivyo vivyo.
Ww kutomkubali samia haimaanishi kuwa hakubaliki kwa wengine.
 
Kama Hawa mnao waita washamba wanapiga spana hivi nchi ya ahadi imekaribia kufikiwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…