Huyu Binti Kwa kusema hivi anaweza kukamatwa?

Huyu Binti Kwa kusema hivi anaweza kukamatwa?

Hawa jamaa hawachagui na mafwele akipewa kazi hako kabinti kanaweza hata kubakwa. Hebu ona kale ka bwana mdogo mwenyekiti wa bavicha Geita, si wameshsmteka!
Nchi hii ni kama haina wasomi.
Yaani jeshi letu la Polisi unashindwa kulitofautisha na Al shabab, Boko Haram na M23.
 
Under this regime, which is incapable of a glimmer of intellectual thought, abduction is an understatement. The Boss Lady's henchmen, will surely hack this SUKUMA piccaninny into pieces.​
 
Kwani aliye kwambia kuwa samia hakubaliki ni nani?
Magufuli alikuwa ana kubalika kwa mamilioni ya watu kwa sababu zao na pia kuna walio kuwa wanamchukia kwa sababu zao na kwa samia hivyo vivyo.
Ww kutomkubali samia haimaanishi kuwa hakubaliki kwa wengine.
Mkuu hapa hatujadili kuhusu mtu kupendwa au kuchukiwa na watu wote kitu ambacho hakiwezekani, hapa tunazungumzia kile kiasi cha kukubalika au kutokubalika kwa wananchi hatuzungumzii makundi yaliyofaidika na utawala bali kukubali kwa huo utawala.
 
Suala la kiongozi kuwa bora au kutokuwa bora hasa katika nchi kama yetu huwa ni mtazamo wa mtu binafisi kutokana na alivyo nufaika au kuathirika kipindi cha uongozi wake.
Magufuri alikuwa anapendwa na mamilioni ya watu kwa sababu zao na pia alikuwa anachukiwa na mamilioni ya watu kwa sababu zao na vilevile kwa huyu mama.
Mfano leo hii huwezi kumuambia mkulima wa kahawa kuwa Magufuri alikuwa bora kuliko samia hali ya kuwa kipindi cha Magufuri alikuwa analazimishwa kuuza kahawa zake kwa mkopo wa sh 1000 kwa kg, hali yakuwa sasa hivi kwa huyu mama anauza kahawa yake kwa sh 5000 kg kwa keshi.
Au huwezi kumuambia muhitimu kuwa Magufuri ni bora kuliko Samia alikataa kumpa ajira na akaja kupewa na samia.

Kwa hiyo suala la kutokuwa bora kwako haimaanishi sio bora kwa wengine.
Sawa ni mtazamo sahihi kwa upande wako.

Mimi nachojali ni kuwa raisi mzuri anatakiwa ahakikishe huduma za kijamii zinakuwa ni rahisi kupatikana kwa wananchi maana zinagusa maisha ya wengi.

Msingi wa serikali ni kuhudumia jamii yake. Kama kiongozi mkuu wa serikali hajishughulishi na welfare ya raia kwangu anakosa sifa ya kuwa kiongozi bora regardless ya mazuri yake yote.

Hospitali hovyo, Usafiri hovyo, Tasisi za kiserikali hovyo, Idara ya ulinzi na usalama hovyo. Hapo mtu anajiteteaje?
 
Mwanakisenza olenchagolaga Samia?
Mwanakisenza : Natenchagolaga.


Huyo Mwanakisenza anaonekana ni bibi wale wazee ambao ilikuwa huwaambii kitu kuhusu CCM, ila cha ajabu huyo bibi kasema hamchagui.
 
Haa, unaona kabisa ni mchezo wa kitoto. Pia, hao ni watumwa wa akili kwamba yenyewe hapo ilipo inachojua ni kuwa mwanamke kazi yake kuchunga ng'ombe Huku akiwa kanyolewa kipara. Hapo inasubiri muda tu iende malishoni....... pathetic!!!
Lakini bado ana haki ya kura moja mtu mmoja. Sema kwa vile mnaiba na hamheshimu hilo
 
Ila kiukweli kabisaa, sa100 hakubaliki kwa wanannchi wengi wa kati na wale wa chini...hajagusa maisha yao moja kwa moja.
Anakubalika kwa kundi dogo tu (na ndio lenye makelele mengi) la wanufaika wa utawala wake...wateule na machawas!
@lucasmwashambwa
 
Back
Top Bottom